Ama kweli mzigo mzito mpe mnyamwezi aubebe. Hivi ndivyo ilivyo na inavyoenda kuwa. Akiwa amesheheni tambo na kila aina ya mbwembwe Sitta baada ya kutawazwa na chama chake na baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba kuwa spika bunge la katiba, Sitta wakati wa kuwashukuru wajumbe, aliwananga mahasimu wake wa kisiasa kuwa HAYA MAMBO YANAWENYEWE, alimalizia kwa kuchagiza neno la wapambe NUKSI.
Sitta aliamini kuwa kiti cha uspika wa bunge la katiba angekitumia kujijenga kisiasa hasa katika mbio za urais mwaka ujao. Sitta akiwa anajitamba akiamini amepiga bao la kisigino, mahasimu wake kisiasa wenye siasa za kisayansi walikwishajua kuwa ule ni mtego 6 hachomoki.
Hili litakuwa bayana saa chache au siku chache baada ya bunge la katiba kuahirishwa. Hakika 6 ataoneka hovyo ndani na nje ya chama chake na mbele ya macho ya watanzania. Pole 6 umevuna ulicho panda.