Mpaka sasa 6 hajajua kuwa anajikaanga mwenyewe
Anajikaanga kweli, yawezekana hajajibaini ngoja kuche.
Mpaka sasa 6 hajajua kuwa anajikaanga mwenyewe
Ama kweli mzigo mzito mpe mnyamwezi aubebe. Hivi ndivyo ilivyo na inavyoenda kuwa. Akiwa amesheheni tambo na kila aina ya mbwembwe Sitta baada ya kutawazwa na chama chake na baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba kuwa spika bunge la katiba, Sitta wakati wa kuwashukuru wajumbe, aliwananga mahasimu wake wa kisiasa kuwa HAYA MAMBO YANAWENYEWE, alimalizia kwa kuchagiza neno la wapambe NUKSI.
Sitta aliamini kuwa kiti cha uspika wa bunge la katiba angekitumia kujijenga kisiasa hasa katika mbio za urais mwaka ujao. Sitta akiwa anajitamba akiamini amepiga bao la kisigino, mahasimu wake kisiasa wenye siasa za kisayansi walikwishajua kuwa ule ni mtego 6 hachomoki.
Hili litakuwa bayana saa chache au siku chache baada ya bunge la katiba kuahirishwa. Hakika 6 ataoneka hovyo ndani na nje ya chama chake na mbele ya macho ya watanzania. Pole 6 umevuna ulicho panda.
Sitta anajua kwamba bila katiba mpya kupita na Urais 2015 ndo bye bye. Ndio maana yuko desperate. Lakini kwa mwenendo wake katika kuongoza BMK ni wazi kwamba kazi ya Urais haiwezi.
Tsoxo, angetulia kwa nafasi aliyonayo angekokotoa, lakini masikini kakokota gunia la mainterahamwe,kaacha wapiga kura tumeduwaa, hata tuliomuamini na kumshabikia hatuamin kama ni yeye ama fotokopi, kwakifupi njozi zake za kukaa magogoni kwishney!
Sitta amejimaliza mwenyewe kisiasa! Kadiri bunge la katiba linavyoendelea watanzania wanazidi kumfahamu sitta, kwa asili sitta ni dikteta, hapendi kusikia kile asichokitaka, hupenda kusikia yale anayoyapenda tu. Watanzania tuwe makini na watu wa aina ya 6. Sitta anaingia katika record ya maspika waliochaguliwa kwenye bunge la katiba likiwa na wajumbe wa vyama vyote na kubaki bungeni akiongoza vikao vya chama badala ya bunge la wananchi. Mzee huyu urais atausikia redioni tu!
wewe ulitaka wafanyaje? au unaamini hakuna kinachowezekana nje ya bunge? mbona si mara ya kwanza watu kushinikiza mambo nje ya bunge na yakafanikiwa? ulionaje kule arabuni?
Dume hilo limeweka avatar ya kike
Kweli dada. Hawa wanabwabwaja tu kama yule Dr Harith Ghassany anayebwabwaja kumsema Baba yetu wa Taifa miaka kumi baada ya kifo cha Baba yetu mpendwa wa Taifa. Mapambano yananoga yanapokuwa uso kwa uso. Ndo maana hawa wanaobwabwaja wanapenda sana kumquote mbwabwaji mwenzao Dr Harith Ghassany. Eti Kassim Hanga aliuawa, wakati chama chetu kinajua hakika jamaa alikufa kwa malaria kali. auwawe kwani chama chetu ni interahamwe? UKAWA wazushi sana hawa.
Huyu naye vipi wenzako wanaongelea Birian wewe unaongelea makande! wa wapi weyeHuko ni kubwabwaja na porojo.
Eti wanataka katiba mpya nje ya bunge la katiba!
Amma kwa hakika Tanzania hakuna upinzani ni mchezo wa kuigiza.
Mkuu wala usiende mbali mpaka Uarabuni, juzi hapa tu raia wamepiga kelele kwenye ajira za uhamiaji mbona jamaa walisitisha? Hata nje inawezekana! Six kwishney!!
Huyu naye vipi wenzako wanaongelea Birian wewe unaongelea makande! wa wapi weye
CCM wamemmaliza kisiasa bila yeye kujijua!!Mimi nilikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanamuamini sana Mheshimiwa huyu hasa pale alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania. Lakini tangu ameteuliwa kuwa Spika wa Bunge maalumu la katiba amekuwa mtu tofauti kabisa.
Siwasemei wengine lakini kwangu mimi nadhani amepoteza hadhi ya kuwa kiongozi kwenye ngazi yoyote ile inayohusisha watu wenye mitazamo tofauti. Ameshindwa kubalance mitazamo na wala kukubali kukosolewa pale anapokoea.
Nasikitika kusema rasmi nimejitoa kuwa shabiki wako kama kiongozi.
Huko ni kubwabwaja na porojo.
Eti wanataka katiba mpya nje ya bunge la katiba!
Amma kwa hakika Tanzania hakuna upinzani ni mchezo wa kuigiza.