Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

Eti ITV wanampa Saidi Kubenea awe muongoza mdahalo alafu wanarusha live, ni sawa kumpa Mnyika aongoze.
 
Siangalii kabisa mjadala wa bunge la katiba. sitaki tena hata kujua nani anasema nini. Labda nije humu niambiwa nani kasikia nini maana kuambiwa si sawa na kusikia kwani ukiambiwa bomu limelipuka si sawa na kuliona au kulisikia, unaweza kupata kiharusi. mambo yalivyo sasa hayafai kupita mbele ya macho. na Sita kusikia na kuona yanayojiri humo. na sioni baya la ITV kwani wanaoweza kusema wamekosea ni wale waliosikia kama waliambiwa yasiyofaa kuambiwa!
 
chama kinachokosa mwelekeo huzuia mambo ya msingi yasijulikane kwa wananchi, Kutojua mambo kwa wananchi ndiyo mtaji pekee wanaobaki nao.

Tusishangae kusikia vyombo vyote vya habari vikizuiwa visirushe mijadala yoyote ya katiba mpya nje ya Bunge, kwa kisingizio cha kuwachanganya wananchi kwa wakati huu.

FUSO;
Sijui pa kuanzia tena kwani umegonga jicho lao. Chama kilichopoteza mwelekeo hakijui tena cha kufanya bali kuwatisha wananchi kwa maneno ya mnapotoshwa bila kuweza kuuonesha huo upotoshwaji.
Six aliwafungia wana habari kuufuatilia huo mchakato, Six akawagawa Wabunge wa upinzani wasiweze kuketi pamoja bungeni na kusema wanakaa kama kamati kwenye makundi, hii ni ili upinzani usiungane. Walio wengi waungane wapitishe mambo yao ionekane kuwa wote walipitia.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma (ccm) amepiga marufuku mikusanyiko yeyote ya kijiweni kujadili Katiba Mpya. Iwe kuisifia au kuiponda, What the hell is this?
Tunaenda wapi?? Mbona maccm yanaogopa hata kabla hatujayaumbua na katiba ya chama chao hiyooo??? Posho halalisheni ili msije shitakiwa, na zaidi ya yote fanyeni bidii kupeana za kutosha ili hata mkisimamishwa ziwe tayari mfukoni. Lakini msitunyime hata huo uhondo tu wa kuwasikiliza uji.nga wenu mnao jadili.
Unapomnyima mtu habari, lazima aipate nusu nusu "Poarching". Habari za jinsi hiyo ni tamu ajabu kwani zinakuwaga tamu na adimu.
Six, usitunyime uhondo tafadhali. Watu watamuinua juu juu Warioba 2015
 
Sasa nimemwelewa DR.Slaa aliposema kwamba Mh. Sitta ni mnafiki numberi one. Huyu si wa kumpa uongozi wa nchi hii kamwe, watanzania tuwe makini tusifanye kosa jingine tena 2015.

Umesahau Mbowe na Wapinzani wote Bungeni walimsapoti Sitta dhidi ya Mh.Chenge, Mh. Rais akashauri tuwape mnachokitaka leo mnakula Mtapishi yenu.Hashim Rungwe alipambana na Sitta lakini hakupata hata kura za wapinzani wenzake. Unafiki ni hataree kuliko Ufisadi
 
Ama kweli mzigo mzito mpe mnyamwezi aubebe. Hivi ndivyo ilivyo na inavyoenda kuwa.

Akiwa amesheheni tambo na kila aina ya mbwembwe Sitta baada ya kutawazwa na chama chake na baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba kuwa spika bunge la katiba, Sitta wakati wa kuwashukuru wajumbe, aliwananga mahasimu wake wa kisiasa kuwa HAYA MAMBO YANAWENYEWE, alimalizia kwa kuchagiza neno la wapambe NUKSI.

Sitta aliamini kuwa kiti cha uspika wa bunge la katiba angekitumia kujijenga kisiasa hasa katika mbio za urais mwaka ujao. Sitta akiwa anajitamba akiamini amepiga bao la kisigino, mahasimu wake kisiasa wenye siasa za kisayansi walikwishajua kuwa ule ni mtego 6 hachomoki.

Hili litakuwa bayana saa chache au siku chache baada ya bunge la katiba kuahirishwa. Hakika 6 ataoneka hovyo ndani na nje ya chama chake na mbele ya macho ya watanzania. Pole 6 umevuna ulicho panda.
 
kwani mambo ya katiba ndo yamekwisha,si kwamba ngoma inaindelea baada ya maliziano tuu?
 
Sitta amejimaliza mwenyewe kisiasa!

Kadiri bunge la katiba linavyoendelea watanzania wanazidi kumfahamu sitta, kwa asili sitta ni dikteta, hapendi kusikia kile asichokitaka, hupenda kusikia yale anayoyapenda tu.

Watanzania tuwe makini na watu wa aina ya 6. Sitta anaingia katika record ya maspika waliochaguliwa kwenye bunge la katiba likiwa na wajumbe wa vyama vyote na kubaki bungeni akiongoza vikao vya chama badala ya bunge la wananchi.

Mzee huyu urais atausikia redioni tu!
 
Huko ni kubwabwaja na porojo.

Eti wanataka katiba mpya nje ya bunge la katiba!

Amma kwa hakika Tanzania hakuna upinzani ni mchezo wa kuigiza.
kwa hali iliyoönekana leo bungeni, hakuna katiba mpya bali kuna uharibifu wa rasimu! 6 anawahamasisha wanaoitwa wajumbe wa bunge la katiba kupendekeza sura mpya za rasimu. Je ile rasimu ya warioba haina sura za rasimu? Ukitafakari kwa makini kinachotafutwa ni kuhalalisha rasimu ya ccm ya serikali 2. Huu ni zaidi ya uhaini kwa taifa! Ukawa wako sahihi na wanasimamia katika kweli.
 
The writing was already on the wall! Tangu mwanzo tulishafahamu kuwa rasimu itakayojadiliwa siyo ya Judge Warioba bali ile iliyoingizwa kwa mlango wa nyuma kwa kupitia-wanasheria njaa akina Malyamkono na kukabidhiwa spika wa bunge LA JMT Mhe. Makinda.

Tayari kuna waraka wa CCM unaohimiza zitolewe nakala nyingi za rasimu hiyo ya CCM name ndio uwe mwongozo wa majadiliano ya sura zilizobaki za rasimu ya katiba.

Kwa wale wenye nakala ya rasimu ya CCM subirini muone majanga mapendekezo ya sura zote zinazohimizwa na Sitta kupelekwa ili ziongezwe ni sura zote zinazohusu mambo ya Tanganyika ambayo hayakuwemo kwenye rasimu ya Warioba kama vile mambo ya Ardhi, serikali za mitaa nk ambayo yalikuwa yameachwa kwa nchi washitika.

Baada ya mapendekezo tote ya sura za rasimu wanannchi watawaelewa UKAWA kwamba kweli CCM hawakujadili rasimu ya Warioba bali rasimu ya CCM iliyoingizwa BMK kwa mlango wa nyuma!
 
kwani mambo ya katiba ndo yamekwisha,si kwamba ngoma inaindelea baada ya maliziano tuu?

...mkuu ata picha huoni ? maridiano yashashindikana kutokana na misimamo ya pande mbili,so technically huwezi kupata katiba kwa sasa. Huu ni muda wa kuangalia namna ya kuepuka aibu...
 
The beginning of the end for sitta,alifikiri kisasi cha mzee wa mvi kimekwisha kuhusu richmond na uwaziri mkuu,tujiandae kisaikolojia kumuona spika sitta akijuzulu na spika mpya kuteuliwa kama njia ya kusafisha hali ya hewa
 
Huko ni kubwabwaja na porojo.

Eti wanataka katiba mpya nje ya bunge la katiba!

Amma kwa hakika Tanzania hakuna upinzani ni mchezo wa kuigiza.

Kuna faida gani kawa waliobaki ndani ya bunge wakati hawataki katiba mpya?
 
Back
Top Bottom