Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,244
Katika kile kinachooneka ni kujiweka kwenye fikra za watu, aliyekuwa spika wa bunge la Tanzania ndgu. Samwel Sitta ameibuka Rasmi na kutangaza waziwazi nia yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema vigezo vyote anavyo na anakubalika kwa wananchi hivyo amekitaka chama chake cha CCM kama kinataka kushinda katika uchaguzi mkuu wa 2015 basi hawana budi kumsimamisha yeye.

Pia alitoa angalizo ya kuwa ccm wasipokuwa makini kumtafuta mtu makini na wakachagua mtu asiyekubalika itatoa nafasi kwa UPINZANI KUCHUKUA NCHI KIRAHISI SANA.

Lakini pia alisema hayo yatafanikiwa kwake kwa kutegemea UPEPO WA KISIASA NCHINI UTAVUMAJE WAKATI HUO.

CHANZO MAGAZETI YA LEO.

IKUMBUKWE HUYU ALIVULIWA USPIKA KWA KILE KIGEZO CHA LAZIMA WAKATI HUU NAFASI IWE KWA JINSIA YA KIKE.
WADAU MNAOMFAHAMU MTANZANIA HUYU JE ANAFAA KUWA RAIS KWA VIGEZO VYA WATU WANAOTAKA MABADILIKO?
MAANA KASHATANGAZA NIA.

MAULID NJEMA WOTE.

=================
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema kwamba anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania na anafikiria kugombea 2015, iwapo dhamira yake itaridhika na mazingira na upepo wa kisiasa wa wakati huo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili juzi, Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri.

Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong'ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

"Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri nigombee," alisema Sitta ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge.

Hata hivyo, alisema hana mkakati wowote sasa wa kuendesha harakati za kutafuta nafasi hiyo kwa udi na uvumba kama baadhi ya wengine (bila kuwataja), wanavyofanya... "Sina sababu za kuanza kutafuta support (kuungwa mkono) wala uundaji wa kamati za ushawishi kwa watu sasa," alisema Sitta.

Badala yake alisema atasubiri hadi muda wa kuchukua fomu za kugombea utakapofika ndipo atakapojitathmini na kusema endapo atabaini kuwa Watanzania wengi wanamuunga mkono, atachukua uamuzi wa kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Aitahadharisha CCM
Waziri huyo aliwahadharisha wanachama wa CCM kwamba wasipokuwa makini, wanaweza kuipoteza nafasi hiyo ya urais na kwenda kwa vyama vya upinzani.

Alionya kuwa iwapo watamteua mtu asiye mwadilifu, Watanzania hawatamchagua na badala yake watampa nafasi hiyo mgombea yeyote kutoka vyama vya upinzani.

Alisema Watanzania wengi wana werevu wa kutosha kujua watu ambao ni mafisadi na ambao wamekuwa wakitumia fedha zao chafu kwa ajili ya kutaka wakubalike mbele ya macho ya Watanzania. Alisema suala la uadilifu ni moja ya vigezo muhimu ambayo CCM wanapaswa kuvizingatia ili kupata ushindi wa kiti cha urais mwaka 2015.

"Ndiyo maana nilipokuwa mbele ya Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba niliweka wazi kwamba Tanzania tunahitaji kuwa na jopo la kuhoji viongozi na wananchi wawe na fursa ya kuwachambua," alisema Sitta.

Alisema kinachohitajika Tanzania ni mfumo ambao utajenga mazingira ya kuwa na viongozi waadilifu katika ngazi zote.

Alisema hali hiyo itaepusha mfumo unaoonekana sasa wa viongozi kwenye ngazi mbalimbali kuishi kiujanjaujanja, kujinufaisha na kutojali athari kwa uchumi wa nchi na Watanzania kwa ujumla.

Alitoa mfano wa uzembe uliofanywa na viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambao umesababisha Bandari ya Dar es Salaam kupoteza uaminifu kwa nchi mbalimbali zinazopakana na Tanzania.

Alisema uzembe huo umeifanya Bandari ya Dar es Salaam kuingiza Sh38 bilioni kwa mwezi tofauti na Mombasa ambayo inaingiza Sh300 bilioni.

Chanzo: Mwananchi
 
tatizo lake hana msimamo kwani anatetea uchama zaidi kuliko maslahi ya taifa na yupo kimaslahi binafsi zaidi. Alivyokuwa spika alijaribu kuonyesha msimamo wa kutoyumbishwa lkn alivyoondolewa uspika amakuwa akinyenyekea mafisadi kwa wasiwasi wa kutemwa 2015
 
Anakosa sifa moja kubwa, amekuwa mtiifu kwa wakubwa pamoja na chama huku akipuuza sauti za wanyonge. yaani kulinda maslahi ya chama na wakubwa kuliko ya watanzania tulio wengi kimatendo.

Katika kile kinachooneka ni kujiweka kwenye fikra za watu, aliyekuwa spika wa bunge la Tanzania ndgu. Samwel Sitta ameibuka Rasmi na kutangaza waziwazi nia yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema vigezo vyote anavyo na anakubalika kwa wananchi hivyo amekitaka chama chake cha CCM kama kinataka kushinda katika uchaguzi mkuu wa 2015 basi hawana budi kumsimamisha yeye.
Pia alitoa angalizo ya kuwa ccm wasipokuwa makini kumtafuta mtu makini na wakachagua mtu asiyekubalika itatoa nafasi kwa UPINZANI KUCHUKUA NCHI KIRAHISI SANA.
Lakini pia alisema hayo yatafanikiwa kwake kwa kutegemea UPEPO WA KISIASA NCHINI UTAVUMAJE WAKATI HUO.
CHANZO MAGAZETI YA LEO.

IKUMBUKWE HUYU ALIVULIWA USPIKA KWA KILE KIGEZO CHA LAZIMA WAKATI HUU NAFASI IWE KWA JINSIA YA KIKE.
WADAU MNAOMFAHAMU MTANZANIA HUYU JE ANAFAA KUWA RAIS KWA VIGEZO VYA WATU WANAOTAKA MABADILIKO?
MAANA KASHATANGAZA NIA.

MAULID NJEMA WOTE.
 
Jamani kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa Mzee 6 ni mwanzirishi wa CCJ wakiwa na mlopokaji Nape. Sasa iweje aseme CCM wakichagua mtu asiyekubalika upinzani utachukua nchi kiurahisi au asipochaguliwa kuwa mpeperushaji wa bendera ya CCM atakimbilia CCJ kupeperusha? Huyu Mzee anazeeka vibaya sijui tatizo lake lilitokana na walipomletea mizengwe ya kuwa mgombea wa Uspika lazima awe mwanamke hivyo kwa kuwa muda ulikuwa mdogo kwa yeye kujibadilisha anaona ni bora kuwavuruga tu sasa ili tukose wote...
 
Kama ni kura nasema hapana hana msimamo. Anatafuta ulaji tu. Angetupa kidogo maono yake kuhusu nchi yetu na jinsi atakavyoimarisha ulinzi.
 
Jamani kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa Mzee 6 ni mwanzirishi wa CCJ wakiwa na mlopokaji Nape. Sasa iweje aseme CCM wakichagua mtu asiyekubalika upinzani utachukua nchi kiurahisi au asipochaguliwa kuwa mpeperushaji wa bendera ya CCM atakimbilia CCJ kupeperusha? Huyu Mzee anazeeka vibaya sijui tatizo lake lilitokana na walipomletea mizengwe ya kuwa mgombea wa Uspika lazima awe mwanamke hivyo kwa kuwa muda ulikuwa mdogo kwa yeye kujibadilisha anaona ni bora kuwavuruga tu sasa ili tukose wote...

Ndiyo maana akasema ataangalia upepo utakavyokuwa hii ni kwamba asipopitishwa yeye basi lazima atamegukia UPINZANI. WAKIWEKA KILE KIGEZO CHA JINSIA IMEKULA KWAKE KIKWETE HASHINDWI.
 
Huyu tangu enzi za Mwalimu ni waziri. Aaaaaaaaaah! Naye apumzike bwana labda akiombwa na chama chake na sio kuanza "kuchitongozesha tongozesha". Atulie kama anafaa chama chake kitaamua kwa wakati na sio kupayuka payuka.
 
Sitta kilaza tu hawezi kutuongoza na tukawa happy asitake kujisafisha hapa....Hatumtaki mtu yoyote kutoka magamba...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ila naona safari hii hajaropoka kuhusu CDM ile ngumi ya tumbo na kichwa aliyopigwa na Dr Slaa ilitosha.
 
mnyonge mnyongen haki yake mpeni. aliongoza bunge lenye viwango, ni shupavu. anajiamini. naona anafaa 100%.
Mafisadi walimuogopa. Walitaka kumvua uanachama ndipo akapoa.
 
Back
Top Bottom