Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

...mkuu ata picha huoni ? maridiano yashashindikana kutokana na misimamo ya pande mbili,so technically huwezi kupata katiba kwa sasa. Huu ni muda wa kuangalia namna ya kuepuka aibu...

Kwa asilimia ngapi una uhakika na unacho kisema.?
 
The beginning of the end for sitta,alifikiri kisasi cha mzee wa mvi kimekwisha kuhusu richmond na uwaziri mkuu,tujiandae kisaikolojia kumuona spika sitta akijuzulu na spika mpya kuteuliwa kama njia ya kusafisha hali ya hewa

nimemwogopa zaid alipotoa amri ya kidikteta kuwa ITV IFUTWE
 
Ila tuseme kweli, kama 6 ana nia njema ajiuzulu sasa, ili abaki na heshima mbele ya watanzani, 6 hakuwa na jinsi ya kujinusua kwenye mtego huo zaidi ya kujiondo kwenye issue ya kugombea uspika. Kile kiti kina pande 2 ukikidhi matakwa ya chama wananchi watakulaum, lakini pia ukikidhi matakwa ya wananchi chama kitakulaum.
 
Tafadhali husika na kichwa cha hapo juu.

Mimi kama raia wa kawaida wa nchi hii,najitokeza kukushauri wewe Samwel Sitta kama Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Nafanya hivi kwasababu mbalimbali.Mosi, watanzania tunatambua,kupenda na kufuatilia mambo yote ya kisiasa yanayoendelea hapa nchini. Pili,kwakuwa nchi yetu ni nchi ya utawala wa sheria,sheria ni kila kitu. Tatu,kwakuwa wewe ni Mwanasheria mwenzangu, ushauri wangu utakuwa rahisi kueleweka.

Mh.Sitta, unajua fika kuwa Bunge Maalum la Katiba ambalo unaliongoza linaongozwa na Sheria. Sheria zenyewe ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 (kama ilivyorekebishwa mara kwa mara), Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,2011 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake pamoja na Kanuni za Bunge Maalum la Katiba ambazo mmeendelea kuzirekebisha jana. Hizo tu ndiyo sheria zinazokuongoza na kuongoza Bunge Maalum la Katiba.

Mh.Sitta, unajua kuwa matendo yako,maneno yako,teuzi zako,amri zako na adhabu zako lazima zielezwe na Sheria tajwa hapo juu. Haiwezekani ukatoa kauli au kufanya lolote nje ya sheria. Hadi sasa,umeteleza mara mbili.Kwanza,pale ambapo uliteua Kamati ya Maridhiano nje ya Bunge Maalum la Katiba. Kiukweli,hukuwa na nguvu na uwezo wa kufanya hivyo. Pili, pale ulipotaka kukomeshwa kwa midahalo kupitia vyombo vya habari jana. Naamini sheria zote nilizozitaja hazijakupa uwezo huo.

Napenda kukushauri kutenda na kusema kwa mujibu wa sheria. Ni hayo tu Mh.Sitta


Wako mtiifu,

P.E.Mselewa

Kijana wa kitanzania
 
Well

Wabaya wa Sitta wanachekelea. Mashabiki wa Sitta bila shaka wamenuna. Vipi kuhusu wapambe nuksi?
 
Nadhani Lowasa anamfahamu zaidi 6 kuliko kila mtu, sasa na sisi bahati nzuri BMK limefichua makucha ya unafiki wake. HAFAIIIIIIIIII HATA KIDOGOOOOOO KUWA KIONGOZI WA KITAIFA. Nimeelewa pia kwanini R. Azzizi aliamua kumuweka Ana Makinda kuwa spika badala ya 6. Hakika ananichefua.
 
Umri umeenda kwa haka kazee sasa hana option nyingine ktk kukubali hilo zaidi ya kutumia ubabe p.u.m.b.avu kwenye mambo ya msingi.
Anazuia midahalo kwani kwa sheria IPI??
Atunge sheria ya kuwafunga watu midomo wasiongee. Idiot
 
Huko ni kubwabwaja na porojo.

Eti wanataka katiba mpya nje ya bunge la katiba!

Amma kwa hakika Tanzania hakuna upinzani ni mchezo wa kuigiza.

Kweli dada. Hawa wanabwabwaja tu kama yule Dr Harith Ghassany anayebwabwaja kumsema Baba yetu wa Taifa miaka kumi baada ya kifo cha Baba yetu mpendwa wa Taifa. Mapambano yananoga yanapokuwa uso kwa uso. Ndo maana hawa wanaobwabwaja wanapenda sana kumquote mbwabwaji mwenzao Dr Harith Ghassany. Eti Kassim Hanga aliuawa, wakati chama chetu kinajua hakika jamaa alikufa kwa malaria kali. auwawe kwani chama chetu ni interahamwe? UKAWA wazushi sana hawa.
 
6 hana mpya zaidi ya kusubiri kupaa kwa baba Ndiyo maana ameamua kujitoa ufahamu jumla
 
Masikini 6 wenziwe walimtega kwa mtego wa mbali akaingia mzima mzima wao wakacheka
 
Mzee six unafiki unamponza, anakosa heshima mbele ya jamii
 
Wakati Wa kujadili hili swala la katiba mpya Jueni kwamba katiba mpya si kwa ajili ya ccm Bali ya watanzania ccm ina wanachama milioni tano nchi nzima wapinzani wapo milioni kama sita nchi nzima ila Tanzania ina watu mil.45 sasa ccm (Mimi ni ccm) tusidhani tumepata au tutapata ushindi kwa kupata katiba isioyo ya maridhiano na makundi yote madogo madogo na makubwa makubwa

Hayo madogo ndio yakikuwa tabu yake ni kubwa sana.Tuache kujitoa ufahamu kwa uchu Wa madaraka hii nchi si ya vyama vyetu ni ya watanzania.
 
Sitta alipochukua uamuzi wa kufuja rasilimali za nchi kwa kujenga ofisi ndogo ya bunge urambo nilijua ameleleza tu.Kumbe sivyo, jana katangaza kuwa bunge litakaa siku 90 badala ya 60 zilizokisheria tena kupitia Government Notice.

Madai ya kusema siku za jumamosi hazihesabiki leo ndiyo anakumbuka na amesahau kuwa tayari walitumia siku 70 kwa mtindo huu wa kutojali siku za jumamosi.

Sitta namuona kama DIKTEKA wa aina yake Afrika.
 
UDIKTETA WA SITTA HUU HAPA KWA JANA PEKEE;
  • Kubadili kanunu 13 kwa manufaa yake
  • Kutoa amri ITV idhibitiwe
  • Kutoa Amri Tume ya mabadiliko ya katiba idhibitiwe
  • Kutoa maelekezo kuwa siku zabunge zitakuwa 90 badala ya 60 zilizotangazwa kupitia Gazeti la serikali

.......................na mengine.6 hatariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom