Kauli za Spika wa Bunge la Katiba mnafiki Samwel Sitta kulalamikia Kituo cha ITV kukubali kuendesha Mijadala ya Kikatiba ya kuwaelimisha wananchi kuhusu Maudhui na mambo mengi yanayolenga kufichwa na kundi la CCM ili wananchi wasiyajue ni ishara nyingine ya jinsi Sitta asivyofaa kusimamia kiti, amewekwa kulinda genge la CCM na mkakati wake lilivyokusudia kuudhulumu umma haki na uwazi unaotakiwa ktk kuielewa Rasimu ya 2 ya Katiba yao Mpya. Hii ni dalili wazi kuwa CCM ipo pabaya, Samwel Sitta anahaha kulinda tamaa zake kuelekea Urais hivyo analazimishia umma unyamaze kimya kumwachia na kundi la CCM wajiendee bila kuhojiwa!! Wanachokifanya akina Warioba ktk Mjadala wa Kigoda cha Mwalim ni somo ambalo wangetakiwa walitoe ndani ya Bunge endapo wadhalimu hao CCM wasingeivunja tume na kuifungia Tovuti ya Tume. Ni Makosa ya makusudi. Hivyo hakuwa kundi la kuwazuia akina warioba kama Watanzania, wananchi huru kuwaelimisha umma wa watanzania kuhusu Rasimu yao kwa sasa. Yafaa walindwe kwa njia yoyote.
My take:
Kauli ya Sitta ni ishara na Dokezo kamili kwa Wanaharakati, Wanasheria na makundi ya kulinda ustawi wa taaluma na Uhuru wa habari wachukuwe tahadhari kubwa kwa maneno ya Samwel Sitta, na endapo ITV itakemewa (na Waziri Fenella) au kutishwa, au kuzuiwa kuendesha Midahalo ya kuwaelimisha wananchi ukweli, iwe ni mwanzo wa kuchukua hatua, hata ikibidi kufungua kesi kuzuia Mijadala ya Bunge ambalo linatakiwa liwe kwa maslahi ya Umma na sio kundi la CCM. Ndio maana mwada wa Habari nao Serikali inaufichaficha, inachelewesha!! Tusikubali, tusikubali, tusikubali kamwe!