Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

Kauli za Spika wa Bunge la Katiba mnafiki Samwel Sitta kulalamikia Kituo cha ITV kukubali kuendesha Mijadala ya Kikatiba ya kuwaelimisha wananchi kuhusu Maudhui na mambo mengi yanayolenga kufichwa na kundi la CCM ili wananchi wasiyajue ni ishara nyingine ya jinsi Sitta asivyofaa kusimamia kiti, amewekwa kulinda genge la CCM na mkakati wake lilivyokusudia kuudhulumu umma haki na uwazi unaotakiwa ktk kuielewa Rasimu ya 2 ya Katiba yao Mpya. Hii ni dalili wazi kuwa CCM ipo pabaya, Samwel Sitta anahaha kulinda tamaa zake kuelekea Urais hivyo analazimishia umma unyamaze kimya kumwachia na kundi la CCM wajiendee bila kuhojiwa!! Wanachokifanya akina Warioba ktk Mjadala wa Kigoda cha Mwalim ni somo ambalo wangetakiwa walitoe ndani ya Bunge endapo wadhalimu hao CCM wasingeivunja tume na kuifungia Tovuti ya Tume. Ni Makosa ya makusudi. Hivyo hakuwa kundi la kuwazuia akina warioba kama Watanzania, wananchi huru kuwaelimisha umma wa watanzania kuhusu Rasimu yao kwa sasa. Yafaa walindwe kwa njia yoyote.

My take:
Kauli ya Sitta ni ishara na Dokezo kamili kwa Wanaharakati, Wanasheria na makundi ya kulinda ustawi wa taaluma na Uhuru wa habari wachukuwe tahadhari kubwa kwa maneno ya Samwel Sitta, na endapo ITV itakemewa (na Waziri Fenella) au kutishwa, au kuzuiwa kuendesha Midahalo ya kuwaelimisha wananchi ukweli, iwe ni mwanzo wa kuchukua hatua, hata ikibidi kufungua kesi kuzuia Mijadala ya Bunge ambalo linatakiwa liwe kwa maslahi ya Umma na sio kundi la CCM. Ndio maana mwada wa Habari nao Serikali inaufichaficha, inachelewesha!! Tusikubali, tusikubali, tusikubali kamwe!
 
Spika wa BMK ameishauri serikali kupitia kwa waziri wa habari Mh Fenela kuwashughulikia ITV kwa kuendesha mijadala na makongamano. Spika sitta amekereka kwa watu kutoa maoni yao kuhusu mchakato wa kuijadili rasimu ya katiba ambayo ni haki ya msingi kwa kila Mtanzania .Je akiwa Rais ataruhusu demokrasia nchini kweli?
hata asingetoa hiyo kauli, Sitta hana qualities za kuwa rais
 
Lowassa ana nafuu kuliko Sitta by far japo wote ni kundi lile lile.
 
Anasema

"kuna chombo kimoja kinajifanya chenyewe ndio kinajua sana kuitisha midahalo,kazi yao ni kushambulia,kupambana na mbaya zaidi wahudhuriaji wengi ni wa upande mmoja wanashambulia,wanazomea na kushangilia.Sasa serikali muangalie hili nadhani waziri Fenela Mkangara upo hapa .Maana haiwezekani wafanye haya kisa ni chombo binafsi tu"
 
Mods chukueni hio nukuu hapo pandisheni juu kwenye main thread!
 
Mtanzania yoyote anae mfikiria 6 kuwa mrithi wa Jk hamjui vyema 6 nibora aongeze jitihada ya kumjua 6 na nivyema anzie kufuatilia jimbo lake la ubunge la urambo.
Ukienda urambo ktk jibo la 6 utapata huruma kubwa uwaonapo wapiga kura wake walivyo na jimbo lilivyo nyuma ktk sekta zote za kijamii. Wananchi wa urambo wanatia huruma nyuso zao zime inama hawana lakujivunia.
 
Sitta amekwishajimaliza kama ana ndoto za urais ajue tumekwisha mfuta, huwezi kuwa na rais mwenye sura mbili (double standard person).
Ila kwa upande mwingine huo ni mpango wa Mungu wa kuwaumbua ccm ili 2015 waondoke kwa urahiiisi!
 
Kwani midahalo si ya wazi kila mtu anarusiwa kushiriki? Nani kamnyima na yeye asishiriki. Mijitu ina kila aina ya laana hadi laana ya wivu. Nyambaf
 
Mkuu unadandia watu pasipo sababu sitta yuko sahihi utalaumu bure.
 
Sitta amekwishajimaliza kama ana ndoto za urais ajue tumekwisha mfuta, huwezi kuwa na rais mwenye sura mbili (double standard person).
Ila kwa upande mwingine huo ni mpango wa Mungu wa kuwaumbua ccm ili 2015 waondoke kwa urahiiisi!
Mchague kakobe mgombea wako wa urais.
 
Ina maana watufunge hata sisi tunaojadili mitaani? Sasa uhuru wakuongea uko nyumbani kwa 6 tu?
 
hata me niliona leo amenishangaza sana lile somo la jana limewauma sana walikuwa hawataki tujue ukweli wa mambo. viva itv endeleeni hivyo hivyo
 
Anasema "kuna chombo kimoja kinajifanya chenyewe ndio kinajua sana kuitisha midahalo,kazi yao ni kushambulia,kupambana na mbaya zaidi wahudhuriaji wengi ni wa upande mmoja wanashambulia,wanazomea na kushangilia.Sasa serikali muangalie hili nadhani waziri Fenela Mkangara upo hapa .Maana haiwezekani wafanye haya kisa ni chombo binafsi tu"

maneno ya sitta hayo! unategemea nini toka kwake!
expect nothing less but the real samwel sitta!
 
Back
Top Bottom