Sitta atimuliwa nyumba ya Serikali

Sitta atimuliwa nyumba ya Serikali

Hivi kama serikali isingesitisha kumlipia kodi, Sitta angeendelea kukaa kwenye hiyo nyumba mpaka lini?

Halafu cha ajabu huyo mzee alikataa kukaa kwenye nyumba za mawaziri badala yake akalazimisha serikali imlipie zaidi ya milioni 10 kila mwezi ili aponde maisha kwenye hekalu huko Masaki!
 
Huyo Mzee ata wangemtaifisha mali zake ingekuwa poa sana.Alituimbia mno nakuchakachua maoni yetu ya katiba mpya.
 
Kwanza aswala hapa yako mengi. Kwa nini aishi kwenye nyumba ya kupanga? Au nyumba zilizouzwa zimekwisha? Madhumuni ya kuziuza ni yapi? Ni nani hasa aliyehusika ktk huo uuzwaji? Bado yuko hai? Siyo jipu kweli?
 
Tatizo naloliona hapa mtoa maada hakusoma uchumi na hajasoma kitu kinaitwa Commnication Economy,Angekuwa amesoma hivyo vitu asingeweza kuandika habari hii inayoonekana imekaa kiuchonganishi.Nchi yoyote ile hapa mtumishi wa umma unapostaafu huwa unapaswa kuhama kwenye nyumba ya serikali immediatrly baada ya kukabidhi ofisi.Tanzania hata Rais anapostaafu huwa anaondoka ikulu na kurudi nyumbani kwake haraka.Lakini kwa Samweli sita ana miaka zaidi ya arobaini anatumikia Tanzania alitakiwa awe amejenga makazi yake binasfi .Na Ninaamini atakuwa alifanya hivyo.Hapo mwandishi kabla ya kuandika alipaswa kufikilia nini anaandika.
 
Kama sio mtumishishi tena wa serikali, ni sahihi kuwapisha wengine. Pia mzee sitta si ana nyumba nyingi tu.na sikia hata za hapa juu kilima nyege karibu na Didis pub ni za kwake
 
Ndugu Nyumba za serikali ziliuzwa na serikali yenyewe wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi,swala kama ni jipu fuatilia wanasheria watakusaidia
 
Kama unadhani CCM wana shukurani umekosea sana. Hivi unajua CCM walivyomtumia kuchakachua maoni ya wananchi katika bunge la katiba? Unakumbuka madai kwamba marehemu walipiga kura akiwemo mamake Zitto? Unakumbuka alitumia kila njia mpaka mahujaji waliokuwa Saudia walipiga kura?

Sasa angalia mshahara wake, ametimuliwa nyumba ya serikali baada ya serikali kukataa kumlipia pango! Alikuwa analipiwa dola 8000 kwa mwaka. Amehamia Manzese!

====================================
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, ameondolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi baada ya Serikali kugoma kumlipia kodi ya pango.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, mwanasiasa huyo mashuhuri, aliondolewa katika nyumba hiyo iliyopo Masaki, Dar es Salaam na kulazimika kuanza kuhamisha vyombo vyake tangu Ijumaa ya Julai 8, mwaka huu.

Kwa muda wote tangu akiwa Spika wa Bunge, Serikali ilikuwa inalipa kiasi cha dola 8,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 12 kwa ajili ya nyumba hiyo.

Sitta ambaye baadaye alikuwa waziri katika Wizara ya Afrika Mashariki pamoja na Uchukuzi, aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa nafasi yake.

Kwa mujibu wa kijana aliyekuwa nyumbani hapo, alisema walianza kuhama tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuhama kwa kuhamisha vitu kidogo kidogo.

“Ni kweli mzee amehama hapa, tangu Ijumaa tulikuwa tunahamisha vyombo taratibu na sijui kama Serikali imegoma kulipa kodi ama la, ila sasa amehamia jirani tu hapo Mtaa wa Manzese, hapa hapa Masaki.

“Nasikia nyumba imepata mpangaji mpya ndiyo maana wanahama,”alisema.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya, ili kuzungumzia hilo, alimtaka mwandishi kuwatafuta Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wizara ya Fedha.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa utaratibu wa malipo kwa maspika wastaafu, ikiwa ni pamoja na matunzo na nyumba wanazoishi, Owen alisema Bunge halihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria.

“Watafute Utumishi na Wizara ya Fedha, wao ndio wahusika, Ofisi ya Bunge haihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria, isipokuwa Utumishi na Wizara ya Fedha ndio wahusika,” alisema.

Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema hana taarifa hizo za kuondolewa kwa Sitta hivyo atafuatilia.

Hata hivyo, alipotafutwa tena kupitia simu yake ya kiganjani, Kairuki alimtaka mwandishi kuwatafuta Hazina, kwamba ndio wanaoweza kulisemea jambo hilo.

“Naomba uwatafute Hazina wakupe ufafanuzi, halafu baadaye urudi kwangu,” alisema Kairuki.

Alipotafutwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kupitia simu yake ya kiganjani, ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema:“Ufafanuzi kuhusu malipo kwa viongozi wastaafu unatolewa kwa viongozi husika na si kwa vyombo vya habari.”

Hali hiyo ya Sitta, imekuwa ni tofauti na aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda, ambaye Serikali kupitia Bunge iligharimia matengenezo ya nyumba yake iliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam, ambako ujenzi wake ulikumbana na lawama kali za wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.

Spika Makinda alilaumiwa na majirani zake kwa kusababisha usumbufu baada ya kuziba njia inayopita katika eneo hilo kwenda maeneo ya Sinza.

Kwa mujibu wa Margaret Sitta ambaye ni mke wa Samweli Sitta na Mbunge wa Urambo, alisema kuwa walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo ya Serikali kwa kuwa mumewe alikuwa Waziri wa Uchukuzi, lakini Baraza la Mawazili lilivunjwa tangu mwaka jana hivyo walipaswa kuhama.

Chanzo: Mtanzania
Wacheni kututia vidole vya masikio na pamba ya macho. Samwel SItta si maskini wa nyumba wala kipato wa kuonewa huruma.
 
Kwani hiyo nayo ni habari? Ni nyumba ya serikali na yeye si mtumishi wa serikali apishe tu wapewe watumishi wengine wa serikali wanaostahili kupewa nyumba hiyo kwa mujibu wa sheria/ utaratibu.

Kuna mchangiaji amesema madhambi aliyowafanyia watanzania kwenye bunge la katiba kwa maslahi yake na chama chake ndiyo yanayomtafuna nami nasema ni kweli na yatazidi kumwandama.Huu ni uongozi tofauti kabisa na waliyoyazoea huko nyuma.Hata hivyo walimwacha kwa muda mrefu alitakiwa arushwe nje toka alipopigwa chini kwenye nafasi hiyo.Sasa ina maana wananchi tulikuwa tunamgharamikia Makinda nae?Taifa la viongozi wapigaji.Yaani yeye majumba yake apangishe tena kwa dollar huku yeye akikaa bure kwenye nyumba za serikali?Kinachomweka Dar ni nini asirudi Urambo?Kwani hata jimbo la mkewe lipo Dar?
 
Mjanja ni yule aliyeamua kufuga nyuki...Heshima yake itaendelea kuwepo kwa miongo kadhaa....hivi hakujenga?
anyway arudi mboka standard and speed aka mwendo kasi
 
Leo hili la Samweli Sitta ambaye alikwisha lipwa mafao kwa kazi zake Zote linaonekana kubwa kuliko wazee wetu waliolitumikia taifa kwa uadilifu mpaka uzee unawakuta tena katika maZingira magumu sana.

Sifahamu huchukua muda gani kwa wabunge kulipwa mamilioni ya kiinua mgongo baada ya kazi 'ngumu' kupita zote duniani ya kulitumikia taifa kwa muda mrefu wa miaka mitano, lakini sina hakika kama wao husubiri kwa muda wa japo robo mwaka.

Kivumbi kinakuja kwa wavuja jasho hawa ambao wengi hawajawahi kuwa na posho za kukaa/kusimama, mishahara inayotosheleza mahitaji wala fursa nono za mikopo. Wazee hawa licha ya magumu waliyopitia mara nyingi huwalazimu kusubiri hadi zaidi ya mwaka mzima kulipwa vijisenti vyao vya mafao. Wengi huishia kufariki kwa msongo wa mawazo kabla ya kuyaona hayo mafao na wengine mafao huwakuta wakiwa wateja wa kudumu wa Mirembe.

Leo hii kigogo aliyemaliza muda wake anaondoka kwenye nyumba ya serikali tunamhurumia na kuigeuza habari kubwa mno, ukizingatia vimaslahi vidogo alivyokuwa akipata enzi za utumishi wake pamoja na vimafao ambavyo havikumwezesha kumudu kujenga japo kakibanda.
 
Anyway mwache atimuliwe maana sio mtumishi tena wa serikali kama alikua analipiwa na serikali. Kama ni ... walikua wanamlipia na wamemtimua acha wamtimue maana hawana kazi nae tena.
Kila cheo cha utumishi wa umma huja na marupurupu yake ikiwemo kupangiwa nyumba, matibabu, mshahara posho, bima ya matibabu, pensheni baada ya kustaafu na kadhalika.
Utumishi unapokoma maana yake marurupu nayo yanakoma kwa muhusika. Kwa upande mwingine anaajiriwa mtumishi mwingine ambaye anapokea mafao kama hayo.
Hili nalo ni eneo ambalo waliokuwa watumishi wa zamani au walistaafu waling'ang'ania kwenye marupurupu hayo na KUENDELEA KULIBEBESHA TAIFA MZIGO.
Sidhani kama Mh. Sitta hakubaliani na hoja ya kuachia baadhi ya marupurupu ili watumishi wapya nao wayapate.. Ndio maana anahama na hakuna mkwara au kuaibisha kwani cheo ni dhamana!
 
Kama unadhani CCM wana shukurani umekosea sana. Hivi unajua CCM walivyomtumia kuchakachua maoni ya wananchi katika bunge la katiba? Unakumbuka madai kwamba marehemu walipiga kura akiwemo mamake Zitto? Unakumbuka alitumia kila njia mpaka mahujaji waliokuwa Saudia walipiga kura?

Sasa angalia mshahara wake, ametimuliwa nyumba ya serikali baada ya serikali kukataa kumlipia pango! Alikuwa analipiwa dola 8000 kwa mwaka. Amehamia Manzese!

====================================
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, ameondolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi baada ya Serikali kugoma kumlipia kodi ya pango.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, mwanasiasa huyo mashuhuri, aliondolewa katika nyumba hiyo iliyopo Masaki, Dar es Salaam na kulazimika kuanza kuhamisha vyombo vyake tangu Ijumaa ya Julai 8, mwaka huu.

Kwa muda wote tangu akiwa Spika wa Bunge, Serikali ilikuwa inalipa kiasi cha dola 8,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 12 kwa ajili ya nyumba hiyo.

Sitta ambaye baadaye alikuwa waziri katika Wizara ya Afrika Mashariki pamoja na Uchukuzi, aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa nafasi yake.

Kwa mujibu wa kijana aliyekuwa nyumbani hapo, alisema walianza kuhama tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuhama kwa kuhamisha vitu kidogo kidogo.

“Ni kweli mzee amehama hapa, tangu Ijumaa tulikuwa tunahamisha vyombo taratibu na sijui kama Serikali imegoma kulipa kodi ama la, ila sasa amehamia jirani tu hapo Mtaa wa Manzese, hapa hapa Masaki.

“Nasikia nyumba imepata mpangaji mpya ndiyo maana wanahama,”alisema.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya, ili kuzungumzia hilo, alimtaka mwandishi kuwatafuta Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wizara ya Fedha.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa utaratibu wa malipo kwa maspika wastaafu, ikiwa ni pamoja na matunzo na nyumba wanazoishi, Owen alisema Bunge halihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria.

“Watafute Utumishi na Wizara ya Fedha, wao ndio wahusika, Ofisi ya Bunge haihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria, isipokuwa Utumishi na Wizara ya Fedha ndio wahusika,” alisema.

Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema hana taarifa hizo za kuondolewa kwa Sitta hivyo atafuatilia.

Hata hivyo, alipotafutwa tena kupitia simu yake ya kiganjani, Kairuki alimtaka mwandishi kuwatafuta Hazina, kwamba ndio wanaoweza kulisemea jambo hilo.

“Naomba uwatafute Hazina wakupe ufafanuzi, halafu baadaye urudi kwangu,” alisema Kairuki.

Alipotafutwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kupitia simu yake ya kiganjani, ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema:“Ufafanuzi kuhusu malipo kwa viongozi wastaafu unatolewa kwa viongozi husika na si kwa vyombo vya habari.”

Hali hiyo ya Sitta, imekuwa ni tofauti na aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda, ambaye Serikali kupitia Bunge iligharimia matengenezo ya nyumba yake iliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam, ambako ujenzi wake ulikumbana na lawama kali za wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.

Spika Makinda alilaumiwa na majirani zake kwa kusababisha usumbufu baada ya kuziba njia inayopita katika eneo hilo kwenda maeneo ya Sinza.

Kwa mujibu wa Margaret Sitta ambaye ni mke wa Samweli Sitta na Mbunge wa Urambo, alisema kuwa walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo ya Serikali kwa kuwa mumewe alikuwa Waziri wa Uchukuzi, lakini Baraza la Mawazili lilivunjwa tangu mwaka jana hivyo walipaswa kuhama.

Chanzo: Mtanzania
hapo mwisho.... Kumbe lilivunjwa!!....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom