Ana miaka zaidi 50 ktk utumishi wa umma tena kama kiongozi mwandamizi mkubwa ktk nafasi nyeti nyeti zenye mishahara na mrupu rupu makubwa, awe hajajenga nyumba yake binafsi tu tena ya maana ili aje aishi uzeeni?
Inakuwaje iwe ishu kuuuuubwa hii ya kujadili?
Mimi ni mtumishi wa umma pia na kamshahara kangu hakafiki hata milioni moja kabla ya makato mengine na kodi, lakini Mungu wa Israel ni mwema sana kwani kanibariki kwa kamshahara hakohako jumlisha na vimkopo vya benki kwa dhamana ya mshahara wangu nimejijengea kajumba kangu, naishi na mke na mtoto wangu na kiukweli hata fitina za watu wa Magufuli na serikali yake zinipitie, wala sitapata taabu, sitalalamika...nitasema asante YESU kristo....nitaishi zangu raha mustarehe na maisha hayatasimama ...... yataendelea!!
Sembuse hawa kina Samwel Sitta and the likes ambao wamestaafu na walikuwa wanajua kuwa watastaafu, kwa nini hawakujiandaa? Wanalalamikia nini eti?......Au ni tamaa tu ya kutaka kuhudumiwa na serikali?