Sitta atimuliwa nyumba ya Serikali

Sitta atimuliwa nyumba ya Serikali

Nyumba aliyokua anakaa ni yake mwenyewe kwa maana ya mmiliki, ila aliingia kama mpangaji na kodi inarudi kwake kama $4000-7000 kwa mwezi, sasa kaamia yake ya zamani karibia na valhala
 
Kama unadhani CCM wana shukurani umekosea sana. Hivi unajua CCM walivyomtumia kuchakachua maoni ya wananchi ktk bunge la katiba? Unakumbuka madai kwamba marehemu walipiga kura akiwemo mamake Zitto? Unakumbuka alitumia kila njia mpaka mahujaji waliokuwa Saudia walipiga kura?

Sasa angalia mshahara wake, ametimuliwa nyumba ya serikali baada ya serikali kukataa kumlipia pango! Alikuwa analipiwa dola 8000 kwa mwaka. Amehamia Manzese!

====================================
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, ameondolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi baada ya Serikali kugoma kumlipia kodi ya pango.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, mwanasiasa huyo mashuhuri, aliondolewa katika nyumba hiyo iliyopo Masaki, Dar es Salaam na kulazimika kuanza kuhamisha vyombo vyake tangu Ijumaa ya Julai 8, mwaka huu.

Kwa muda wote tangu akiwa Spika wa Bunge, Serikali ilikuwa inalipa kiasi cha dola 8,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 12 kwa ajili ya nyumba hiyo.

Sitta ambaye baadaye alikuwa waziri katika Wizara ya Afrika Mashariki pamoja na Uchukuzi, aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa nafasi yake.

Kwa mujibu wa kijana aliyekuwa nyumbani hapo, alisema walianza kuhama tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuhama kwa kuhamisha vitu kidogo kidogo.

“Ni kweli mzee amehama hapa, tangu Ijumaa tulikuwa tunahamisha vyombo taratibu na sijui kama Serikali imegoma kulipa kodi ama la, ila sasa amehamia jirani tu hapo Mtaa wa Manzese, hapa hapa Masaki.

“Nasikia nyumba imepata mpangaji mpya ndiyo maana wanahama,”alisema.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya, ili kuzungumzia hilo, alimtaka mwandishi kuwatafuta Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wizara ya Fedha.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa utaratibu wa malipo kwa maspika wastaafu, ikiwa ni pamoja na matunzo na nyumba wanazoishi, Owen alisema Bunge halihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria.

“Watafute Utumishi na Wizara ya Fedha, wao ndio wahusika, Ofisi ya Bunge haihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria, isipokuwa Utumishi na Wizara ya Fedha ndio wahusika,” alisema.

Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema hana taarifa hizo za kuondolewa kwa Sitta hivyo atafuatilia.

Hata hivyo, alipotafutwa tena kupitia simu yake ya kiganjani, Kairuki alimtaka mwandishi kuwatafuta Hazina, kwamba ndio wanaoweza kulisemea jambo hilo.

“Naomba uwatafute Hazina wakupe ufafanuzi, halafu baadaye urudi kwangu,” alisema Kairuki.

Alipotafutwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kupitia simu yake ya kiganjani, ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema:“Ufafanuzi kuhusu malipo kwa viongozi wastaafu unatolewa kwa viongozi husika na si kwa vyombo vya habari.”

Hali hiyo ya Sitta, imekuwa ni tofauti na aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda, ambaye Serikali kupitia Bunge iligharimia matengenezo ya nyumba yake iliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam, ambako ujenzi wake ulikumbana na lawama kali za wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.

Spika Makinda alilaumiwa na majirani zake kwa kusababisha usumbufu baada ya kuziba njia inayopita katika eneo hilo kwenda maeneo ya Sinza.

Kwa mujibu wa Margaret Sitta ambaye ni mke wa Samweli Sitta na Mbunge wa Urambo, alisema kuwa walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo ya Serikali kwa kuwa mumewe alikuwa Waziri wa Uchukuzi, lakini Baraza la Mawazili lilivunjwa tangu mwaka jana hivyo walipaswa kuhama.

Chanzo: Mtanzania
Tatizo lipo wapi? Kazi aliimaliza na alilipwa labda kama utaniambia hakulipwa alikua anajitolea. kama hakujenga nyumba basi awe homeless. Hii Thread ingekua nzuri kama ungeileta kama mada na siyo kama kichocheo cha itikadi ya chama chako. Badilikeni wajemi tusubiri 2020 Magufuri na serikali hawaendi popote kwa kuwachafua mitandaoni mpaka mwaka 2020 kwa bahati mbaya kwenu mnaomchukia.
 
Bora afukuzwe tu kweli unakaa madarakani miaka nenda rudi hujajenga Dar unatamani kuishi kwa kupanga ili upige hela za watanzania! Kwanini usijenge kama unapenda kuishi mjini?
 
Sasa kuna haja gani kuendelea kuishi kwa fedha za serikali ilihali siyo mtumishi?
 
Kani si alishajenga Nyumba na Ofisi ya Spika kule kwao Urambo? Sasa kwa nini alikuwa anaendelea kuishi Dar?
 
Hiyo habari imeandikwa kinamna tu. Halafu chakushangaza hata watu humu hawasomi mpaka mwisho. Hamna tatizo hapo.....habari imekuzwa tu kwa kutumia neno "atimuliwa" lakini ukitumia akili kidogo tu utagundua hajatimuliwa na wala yeye hajakataa kuhama. Pia hiyo "Manzese" ni mtaa wa hapo hapo Masaki.
 
Uingereza wenzetu tumeona David Cameron amekabidhi Ofisi kwa Theresa May siku moja tu anahama nyumba.

Huko kwetu mtu akitolewa nyumba ya serikali miaka baada ya kutoka kwenye ofisi kuna watu wataona kaonewa.
 
Kuna utamaduni umejengeka hao wakubwa hawaondoki nyumba hizo.
David Cameron ameondoka saa chache baada ya Kuwasilisha barua ya kujiuzuru.
Huu utamaduni lazima upigwe vita kwa nguvu zote. Wastage of tax payer's money.
 
Mtaa unaitwa Manzese uko Masaki jamani! Yule Mzee ni tajiri sana! Sikia tu!!
Aliyeyewahi kuwa Spika Na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mzee 6 ameondolewa kwenye Nyumba ya Serikali Na kuhamia Manzese.Kwa wale wenye shuda ya kumwona au kumtembelea Mzee wetu watampata Manzese.
 
Nahisi mtoa mada una yako binafsi, utumishi ukiisha unategemea wengine waishi wapi
 
Aliyeyewahi kuwa Spika Na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mzee 6 ameondolewa kwenye Nyumba ya Serikali Na kuhamia Manzese.Kwa wale wenye shuda ya kumwona au kumtembelea Mzee wetu watampata Manzese.
Hivi ni mtaa wa Manzese Masaki? au Manzese tiptop?
 
Kama unadhani CCM wana shukurani umekosea sana. Hivi unajua CCM walivyomtumia kuchakachua maoni ya wananchi katika bunge la katiba? Unakumbuka madai kwamba marehemu walipiga kura akiwemo mamake Zitto? Unakumbuka alitumia kila njia mpaka mahujaji waliokuwa Saudia walipiga kura?

Sasa angalia mshahara wake, ametimuliwa nyumba ya serikali baada ya serikali kukataa kumlipia pango! Alikuwa analipiwa dola 8000 kwa mwaka. Amehamia Manzese!

====================================
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, ameondolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi baada ya Serikali kugoma kumlipia kodi ya pango.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, mwanasiasa huyo mashuhuri, aliondolewa katika nyumba hiyo iliyopo Masaki, Dar es Salaam na kulazimika kuanza kuhamisha vyombo vyake tangu Ijumaa ya Julai 8, mwaka huu.

Kwa muda wote tangu akiwa Spika wa Bunge, Serikali ilikuwa inalipa kiasi cha dola 8,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 12 kwa ajili ya nyumba hiyo.

Sitta ambaye baadaye alikuwa waziri katika Wizara ya Afrika Mashariki pamoja na Uchukuzi, aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa nafasi yake.

Kwa mujibu wa kijana aliyekuwa nyumbani hapo, alisema walianza kuhama tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuhama kwa kuhamisha vitu kidogo kidogo.

“Ni kweli mzee amehama hapa, tangu Ijumaa tulikuwa tunahamisha vyombo taratibu na sijui kama Serikali imegoma kulipa kodi ama la, ila sasa amehamia jirani tu hapo Mtaa wa Manzese, hapa hapa Masaki.

“Nasikia nyumba imepata mpangaji mpya ndiyo maana wanahama,”alisema.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya, ili kuzungumzia hilo, alimtaka mwandishi kuwatafuta Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wizara ya Fedha.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa utaratibu wa malipo kwa maspika wastaafu, ikiwa ni pamoja na matunzo na nyumba wanazoishi, Owen alisema Bunge halihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria.

“Watafute Utumishi na Wizara ya Fedha, wao ndio wahusika, Ofisi ya Bunge haihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria, isipokuwa Utumishi na Wizara ya Fedha ndio wahusika,” alisema.

Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema hana taarifa hizo za kuondolewa kwa Sitta hivyo atafuatilia.

Hata hivyo, alipotafutwa tena kupitia simu yake ya kiganjani, Kairuki alimtaka mwandishi kuwatafuta Hazina, kwamba ndio wanaoweza kulisemea jambo hilo.

“Naomba uwatafute Hazina wakupe ufafanuzi, halafu baadaye urudi kwangu,” alisema Kairuki.

Alipotafutwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kupitia simu yake ya kiganjani, ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema:“Ufafanuzi kuhusu malipo kwa viongozi wastaafu unatolewa kwa viongozi husika na si kwa vyombo vya habari.”

Hali hiyo ya Sitta, imekuwa ni tofauti na aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda, ambaye Serikali kupitia Bunge iligharimia matengenezo ya nyumba yake iliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam, ambako ujenzi wake ulikumbana na lawama kali za wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.

Spika Makinda alilaumiwa na majirani zake kwa kusababisha usumbufu baada ya kuziba njia inayopita katika eneo hilo kwenda maeneo ya Sinza.

Kwa mujibu wa Margaret Sitta ambaye ni mke wa Samweli Sitta na Mbunge wa Urambo, alisema kuwa walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo ya Serikali kwa kuwa mumewe alikuwa Waziri wa Uchukuzi, lakini Baraza la Mawazili lilivunjwa tangu mwaka jana hivyo walipaswa kuhama.

Chanzo: Mtanzania
Mbona haya mambo ni ya kawaida kiutumishi? Unapostaafu au kuondoka kwenye utumishi zile privileges kama nyumba , gari, wafanyakazi wa nyumbani nk nk haviwezi kuendelea kwani huo siyo ufalme jamani na msiingize siasa kwenye mambo haya
 
Ni halali kabisa kutimuliwa kwenye nyumba ya serikali. Serikali imetimiza wajibu wake
 
Kuna mtaa upo masaki unaitwa manzese karibu na George and Dragon bar
 
Mke wake ni mbunge hivyo anapewa pesa ya nyumba kama wabunge wengine, au wanaishi mbalimbali?
 
image.jpeg
Kwanini asihamie kwenye hekalu lake Mbweni au jengo la bunge alilojijengea jimboni kakwe akijua atakuwa spika wa maisha!!

Ulafi na tamaa ni tatizo kubwa kwa viongozi Tanzania.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom