Sitta atimuliwa nyumba ya Serikali


M

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Messages
3,120
Likes
2,314
Points
280
M

mpk

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2012
3,120 2,314 280
Kama unadhani CCM wana shukurani umekosea sana. Hivi unajua CCM walivyomtumia kuchakachua maoni ya wananchi katika bunge la katiba? Unakumbuka madai kwamba marehemu walipiga kura akiwemo mamake Zitto? Unakumbuka alitumia kila njia mpaka mahujaji waliokuwa Saudia walipiga kura?

Sasa angalia mshahara wake, ametimuliwa nyumba ya serikali baada ya serikali kukataa kumlipia pango! Alikuwa analipiwa dola 8000 kwa mwaka. Amehamia Manzese!

==========

ALIYEKUWA Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, ameondolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi baada ya Serikali kugoma kumlipia kodi ya pango.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, mwanasiasa huyo mashuhuri, aliondolewa katika nyumba hiyo iliyopo Masaki, Dar es Salaam na kulazimika kuanza kuhamisha vyombo vyake tangu Ijumaa ya Julai 8, mwaka huu.

Kwa muda wote tangu akiwa Spika wa Bunge, Serikali ilikuwa inalipa kiasi cha dola 8,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 12 kwa ajili ya nyumba hiyo.

Sitta ambaye baadaye alikuwa waziri katika Wizara ya Afrika Mashariki pamoja na Uchukuzi, aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa nafasi yake.

Kwa mujibu wa kijana aliyekuwa nyumbani hapo, alisema walianza kuhama tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuhama kwa kuhamisha vitu kidogo kidogo.

“Ni kweli mzee amehama hapa, tangu Ijumaa tulikuwa tunahamisha vyombo taratibu na sijui kama Serikali imegoma kulipa kodi ama la, ila sasa amehamia jirani tu hapo Mtaa wa Manzese, hapa hapa Masaki.

“Nasikia nyumba imepata mpangaji mpya ndiyo maana wanahama,”alisema.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya, ili kuzungumzia hilo, alimtaka mwandishi kuwatafuta Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wizara ya Fedha.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa utaratibu wa malipo kwa maspika wastaafu, ikiwa ni pamoja na matunzo na nyumba wanazoishi, Owen alisema Bunge halihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria.

“Watafute Utumishi na Wizara ya Fedha, wao ndio wahusika, Ofisi ya Bunge haihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria, isipokuwa Utumishi na Wizara ya Fedha ndio wahusika,” alisema.

Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema hana taarifa hizo za kuondolewa kwa Sitta hivyo atafuatilia.

Hata hivyo, alipotafutwa tena kupitia simu yake ya kiganjani, Kairuki alimtaka mwandishi kuwatafuta Hazina, kwamba ndio wanaoweza kulisemea jambo hilo.

“Naomba uwatafute Hazina wakupe ufafanuzi, halafu baadaye urudi kwangu,” alisema Kairuki.

Alipotafutwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kupitia simu yake ya kiganjani, ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema:“Ufafanuzi kuhusu malipo kwa viongozi wastaafu unatolewa kwa viongozi husika na si kwa vyombo vya habari.”

Hali hiyo ya Sitta, imekuwa ni tofauti na aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda, ambaye Serikali kupitia Bunge iligharimia matengenezo ya nyumba yake iliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam, ambako ujenzi wake ulikumbana na lawama kali za wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.

Spika Makinda alilaumiwa na majirani zake kwa kusababisha usumbufu baada ya kuziba njia inayopita katika eneo hilo kwenda maeneo ya Sinza.

Kwa mujibu wa Margaret Sitta ambaye ni mke wa Samweli Sitta na Mbunge wa Urambo, alisema kuwa walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo ya Serikali kwa kuwa mumewe alikuwa Waziri wa Uchukuzi, lakini Baraza la Mawazili lilivunjwa tangu mwaka jana hivyo walipaswa kuhama.


Chanzo: Mtanzania
 
malimingiii

malimingiii

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2013
Messages
814
Likes
665
Points
180
malimingiii

malimingiii

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2013
814 665 180
Anyway mwache atimuliwe maana sio mtumishi tena wa serikali kama alikua analipiwa na serikali. Kama ni ... walikua wanamlipia na wamemtimua acha wamtimue maana hawana kazi nae tena.
 
M

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Messages
3,120
Likes
2,314
Points
280
M

mpk

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2012
3,120 2,314 280
Kama unadhani Ccm wana shukurani umekosea sana. Hivi unajua Ccm walivyomtumia kuchakachua maoni ya wananchi ktk bunge la katiba? Unakumbuka madai kwamba marehemu walipiga kura akiwemo mamake Zitto? Unakumbuka alitumia kila njia mpaka mahujaji waliokuwa Saudia walipiga kura?

Sasa angalia mshahara wake, ametimuliwa nyumba ya serikali baada ya serikali kukataa kumlipia pango!

Chanzo: Majira
CC: Dr Tulia, Makonda, Mwigulu, Mangu na wengine kama hao
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
22,760
Likes
49,647
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
22,760 49,647 280
Kama unadhani Ccm wana shukurani umekosea sana. Hivi unajua Ccm walivyomtumia kuchakachua maoni ya wananchi ktk bunge la katiba? Unakumbuka madai kwamba marehemu walipiga kura akiwemo mamake Zitto? Unakumbuka alitumia kila njia mpaka mahujaji waliokuwa Saudia walipiga kura?

Sasa angalia mshahara wake, ametimuliwa nyumba ya serikali baada ya serikali kukataa kumlipia pango!

Chanzo: Majira
Huyo hata akija ukawa atatimuliwa tu, ni msaliti
 
NAPITA

NAPITA

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
5,076
Likes
194
Points
160
NAPITA

NAPITA

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
5,076 194 160
Kwani hiyo nayo ni habari? Ni nyumba ya serikali na yeye si mtumishi wa serikali apishe tu wapewe watumishi wengine wa serikali wanaostahili kupewa nyumba hiyo kwa mujibu wa sheria/ utaratibu.
 
M

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Messages
2,291
Likes
1,224
Points
280
M

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2016
2,291 1,224 280
Aliyeyewahi kuwa Spika Na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mzee 6 ameondolewa kwenye Nyumba ya Serikali Na kuhamia Manzese.Kwa wale wenye shuda ya kumwona au kumtembelea Mzee wetu watampata Manzese.
 
zinginary

zinginary

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2015
Messages
2,298
Likes
1,387
Points
280
zinginary

zinginary

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2015
2,298 1,387 280
Duuh..mazense.sehem gan mkuu??
 
L

Luushu

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2012
Messages
667
Likes
292
Points
80
L

Luushu

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2012
667 292 80
Ndio maisha hayo nae aonje utamu wa manzese
 
Katavi

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Messages
40,332
Likes
4,819
Points
280
Katavi

Katavi

Platinum Member
Joined Aug 31, 2009
40,332 4,819 280
Si mtumishi wa serikali hivi sasa hakuna tatizo kwa yeye kutimuliwa
 
P

Pohamba

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Messages
18,273
Likes
29,998
Points
280
P

Pohamba

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2015
18,273 29,998 280
Nyumba aliyotimuliwa ni ile anayoishi Mh. Mkewe au Mh. Naibu Mkewe wa Pale Hananasif Kinondoni
 
Mgirik

Mgirik

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2013
Messages
11,336
Likes
4,269
Points
280
Mgirik

Mgirik

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2013
11,336 4,269 280
Kama unadhani Ccm wana shukurani umekosea sana. Hivi unajua Ccm walivyomtumia kuchakachua maoni ya wananchi ktk bunge la katiba? Unakumbuka madai kwamba marehemu walipiga kura akiwemo mamake Zitto? Unakumbuka alitumia kila njia mpaka mahujaji waliokuwa Saudia walipiga kura?

Sasa angalia mshahara wake, ametimuliwa nyumba ya serikali baada ya serikali kukataa kumlipia pango!

Chanzo: Majira
CC: Dr Tulia, Makonda na IGP Mangu
Punguza unafiki ww, nyumba si inatakiwa ikaliwe na waliopo kazn?
Au mmezoea maisha ya fadhira na umiungu watu
 
M

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Messages
3,120
Likes
2,314
Points
280
M

mpk

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2012
3,120 2,314 280
Punguza unafiki ww, nyumba si inatakiwa ikaliwe na waliopo kazn?
Au mmezoea maisha ya fadhira na umiungu watu
Ok, sikujua. Sasa yeye mnamlipa nini kwa kuchakachua katiba?
 
B

BUMIJA MOSSES

Member
Joined
Dec 5, 2012
Messages
67
Likes
18
Points
15
B

BUMIJA MOSSES

Member
Joined Dec 5, 2012
67 18 15
Waliipenda, wanune wapasuke, wanaipenda milele. Wapinzani wacha waisome namba eehee CCM Mbele kwa mbele.

Mhe Sita naye leo anaisoma namba.
 

Forum statistics

Threads 1,236,902
Members 475,327
Posts 29,271,842