Sitta atimuliwa nyumba ya Serikali

Sitta atimuliwa nyumba ya Serikali

Mshahara wa dhambi ni mauti... msiba huu hauna kilio ... bora kodi zetu zimepona ...
Kama unadhani CCM wana shukurani umekosea sana. Hivi unajua CCM walivyomtumia kuchakachua maoni ya wananchi katika bunge la katiba? Unakumbuka madai kwamba marehemu walipiga kura akiwemo mamake Zitto? Unakumbuka alitumia kila njia mpaka mahujaji waliokuwa Saudia walipiga kura?

Sasa angalia mshahara wake, ametimuliwa nyumba ya serikali baada ya serikali kukataa kumlipia pango! Alikuwa analipiwa dola 8000 kwa mwaka. Amehamia Manzese!

====================================
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, ameondolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi baada ya Serikali kugoma kumlipia kodi ya pango.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, mwanasiasa huyo mashuhuri, aliondolewa katika nyumba hiyo iliyopo Masaki, Dar es Salaam na kulazimika kuanza kuhamisha vyombo vyake tangu Ijumaa ya Julai 8, mwaka huu.

Kwa muda wote tangu akiwa Spika wa Bunge, Serikali ilikuwa inalipa kiasi cha dola 8,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 12 kwa ajili ya nyumba hiyo.

Sitta ambaye baadaye alikuwa waziri katika Wizara ya Afrika Mashariki pamoja na Uchukuzi, aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa nafasi yake.

Kwa mujibu wa kijana aliyekuwa nyumbani hapo, alisema walianza kuhama tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuhama kwa kuhamisha vitu kidogo kidogo.

“Ni kweli mzee amehama hapa, tangu Ijumaa tulikuwa tunahamisha vyombo taratibu na sijui kama Serikali imegoma kulipa kodi ama la, ila sasa amehamia jirani tu hapo Mtaa wa Manzese, hapa hapa Masaki.

“Nasikia nyumba imepata mpangaji mpya ndiyo maana wanahama,”alisema.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya, ili kuzungumzia hilo, alimtaka mwandishi kuwatafuta Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wizara ya Fedha.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa utaratibu wa malipo kwa maspika wastaafu, ikiwa ni pamoja na matunzo na nyumba wanazoishi, Owen alisema Bunge halihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria.

“Watafute Utumishi na Wizara ya Fedha, wao ndio wahusika, Ofisi ya Bunge haihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria, isipokuwa Utumishi na Wizara ya Fedha ndio wahusika,” alisema.

Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema hana taarifa hizo za kuondolewa kwa Sitta hivyo atafuatilia.

Hata hivyo, alipotafutwa tena kupitia simu yake ya kiganjani, Kairuki alimtaka mwandishi kuwatafuta Hazina, kwamba ndio wanaoweza kulisemea jambo hilo.

“Naomba uwatafute Hazina wakupe ufafanuzi, halafu baadaye urudi kwangu,” alisema Kairuki.

Alipotafutwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kupitia simu yake ya kiganjani, ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema:“Ufafanuzi kuhusu malipo kwa viongozi wastaafu unatolewa kwa viongozi husika na si kwa vyombo vya habari.”

Hali hiyo ya Sitta, imekuwa ni tofauti na aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda, ambaye Serikali kupitia Bunge iligharimia matengenezo ya nyumba yake iliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam, ambako ujenzi wake ulikumbana na lawama kali za wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.

Spika Makinda alilaumiwa na majirani zake kwa kusababisha usumbufu baada ya kuziba njia inayopita katika eneo hilo kwenda maeneo ya Sinza.

Kwa mujibu wa Margaret Sitta ambaye ni mke wa Samweli Sitta na Mbunge wa Urambo, alisema kuwa walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo ya Serikali kwa kuwa mumewe alikuwa Waziri wa Uchukuzi, lakini Baraza la Mawazili lilivunjwa tangu mwaka jana hivyo walipaswa kuhama.

Chanzo: Mtanzania
 
huu ni ujinga uliovuka kiwango yaan miaka yote hiyo unashindwa kujenga nyumba?
Aise pole yake.
Huku mtaan kwetu konda wa dala dala anakajumba kake. Akili ni mali
 
Kama unadhani CCM wana shukurani umekosea sana. Hivi unajua CCM walivyomtumia kuchakachua maoni ya wananchi katika bunge la katiba? Unakumbuka madai kwamba marehemu walipiga kura akiwemo mamake Zitto? Unakumbuka alitumia kila njia mpaka mahujaji waliokuwa Saudia walipiga kura?

Sasa angalia mshahara wake, ametimuliwa nyumba ya serikali baada ya serikali kukataa kumlipia pango! Alikuwa analipiwa dola 8000 kwa mwaka. Amehamia Manzese!

==========

ALIYEKUWA Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, ameondolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi baada ya Serikali kugoma kumlipia kodi ya pango.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, mwanasiasa huyo mashuhuri, aliondolewa katika nyumba hiyo iliyopo Masaki, Dar es Salaam na kulazimika kuanza kuhamisha vyombo vyake tangu Ijumaa ya Julai 8, mwaka huu.

Kwa muda wote tangu akiwa Spika wa Bunge, Serikali ilikuwa inalipa kiasi cha dola 8,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 12 kwa ajili ya nyumba hiyo.

Sitta ambaye baadaye alikuwa waziri katika Wizara ya Afrika Mashariki pamoja na Uchukuzi, aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa nafasi yake.

Kwa mujibu wa kijana aliyekuwa nyumbani hapo, alisema walianza kuhama tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuhama kwa kuhamisha vitu kidogo kidogo.

“Ni kweli mzee amehama hapa, tangu Ijumaa tulikuwa tunahamisha vyombo taratibu na sijui kama Serikali imegoma kulipa kodi ama la, ila sasa amehamia jirani tu hapo Mtaa wa Manzese, hapa hapa Masaki.

“Nasikia nyumba imepata mpangaji mpya ndiyo maana wanahama,”alisema.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya, ili kuzungumzia hilo, alimtaka mwandishi kuwatafuta Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wizara ya Fedha.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa utaratibu wa malipo kwa maspika wastaafu, ikiwa ni pamoja na matunzo na nyumba wanazoishi, Owen alisema Bunge halihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria.

“Watafute Utumishi na Wizara ya Fedha, wao ndio wahusika, Ofisi ya Bunge haihusiki na stahiki zozote za wastaafu kwa mujibu wa sheria, isipokuwa Utumishi na Wizara ya Fedha ndio wahusika,” alisema.

Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema hana taarifa hizo za kuondolewa kwa Sitta hivyo atafuatilia.

Hata hivyo, alipotafutwa tena kupitia simu yake ya kiganjani, Kairuki alimtaka mwandishi kuwatafuta Hazina, kwamba ndio wanaoweza kulisemea jambo hilo.

“Naomba uwatafute Hazina wakupe ufafanuzi, halafu baadaye urudi kwangu,” alisema Kairuki.

Alipotafutwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kupitia simu yake ya kiganjani, ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema:“Ufafanuzi kuhusu malipo kwa viongozi wastaafu unatolewa kwa viongozi husika na si kwa vyombo vya habari.”

Hali hiyo ya Sitta, imekuwa ni tofauti na aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda, ambaye Serikali kupitia Bunge iligharimia matengenezo ya nyumba yake iliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam, ambako ujenzi wake ulikumbana na lawama kali za wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.

Spika Makinda alilaumiwa na majirani zake kwa kusababisha usumbufu baada ya kuziba njia inayopita katika eneo hilo kwenda maeneo ya Sinza.

Kwa mujibu wa Margaret Sitta ambaye ni mke wa Samweli Sitta na Mbunge wa Urambo, alisema kuwa walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo ya Serikali kwa kuwa mumewe alikuwa Waziri wa Uchukuzi, lakini Baraza la Mawazili lilivunjwa tangu mwaka jana hivyo walipaswa kuhama.

Chanzo: Mtanzania
Wamefanya vizuri. Hana tena qualification ya kukaa nyumba ya serikali.
 
Kila cheo cha utumishi wa umma huja na marupurupu yake ikiwemo kupangiwa nyumba, matibabu, mshahara posho, bima ya matibabu, pensheni baada ya kustaafu na kadhalika.
Utumishi unapokoma maana yake marurupu nayo yanakoma kwa muhusika. Kwa upande mwingine anaajiriwa mtumishi mwingine ambaye anapokea mafao kama hayo.
Hili nalo ni eneo ambalo waliokuwa watumishi wa zamani au walistaafu waling'ang'ania kwenye marupurupu hayo na KUENDELEA KULIBEBESHA TAIFA MZIGO.
Sidhani kama Mh. Sitta hakubaliani na hoja ya kuachia baadhi ya marupurupu ili watumishi wapya nao wayapate.. Ndio maana anahama na hakuna mkwara au kuaibisha kwani cheo ni dhamana!
Tatizo wanajiachia sana na kusahau km baada ya muda wataachana na uongoz. Yy alifikiri miaka yote mpaka anafikisha miaka ya kingunge atakuwa serikalini.
Hiyo nafac ningeipata ndani ya miaka 5 tu inanitosha kbs kuwa na kila kitu.
 
Huyu Sitta ndiye alijitapa kipindi Fulani tukiwa naye kwamba, yeye hadi wakati huo (ilikuwa mwaka jana) alikuwa na viwanja na nyumba karibu nchi nzima, ni mikoa 3 au 4 hivi ndio hakuwa na viwanja na nyumba, sasa swali, ina maana Sita hataki kuhamia kwenye nyumba yake huko Dar? anataka serikali imlipie?
 
Karibu manzese mzee wangu , jiandae kuibiwa simu yako , haya kwetu ni maisha ya kawaida tu , ndiyo maana kila mtu ana tecno ya tochi au itel , Usaliti ni laana mbaya sana , NADHANI UNAKUMBUKA NA NIMEKUONYA MARA NYINGI SSANA KWAMBA MALIPO NI HAPAHAPA LAKINI UKAKAIDI.
 
Ina maana ye hakununua Nyumba hata moja zile za serekali...anyway karibu uswazi,kwa uzoefu wako wa kwenye siasa nadhani atatusaidia kukaa chini na madee na ney atusaidie mmoja wao amwachie mwenzie urais Wa manzese maana kila mmoja anajiita rais Wa pande hii
Ungesoma habari yote ungejua kuwa Masaki kuna eneo linaitwa Manzese na ndilo linaloongelewa, sio hiyo Manzese ya barabara ya Morogoro!!
 
Serikali hii inaongoza kwa uzembe pengine dunia nzima.
Sitta uwaziri wake ulikoma tokea October mwaka jana na December mawaziri wengine wakateuliwa. Hapo unakuta kwa miezi yote 7 serikali inalipa kodi ya pango na huku inawalipia viongozi wengine gharama za hotel kwa vile nyumba hakuna.
Tumeona UK bw Cameroon siku hiyohiyo ana resign na anafungasha mizigo yake kumpisha mtu mwingine makazi.
Sie kuhama miezi 7?
 
David Cameron alihama Down street 10 masaa machache tu baada ya Theresa May kuwa confirmed na Malkia kuwa waziri mkuu sasa huyu mzee miaka yote hiyo baada ya baraza kuvunjwa bado anangangania nyumba y serikali?
 
Kwani hiyo nayo ni habari? Ni nyumba ya serikali na yeye si mtumishi wa serikali apishe tu wapewe watumishi wengine wa serikali wanaostahili kupewa nyumba hiyo kwa mujibu wa sheria/ utaratibu.
Sahihi mkuu. Kwanza kama ile nyumba ilikuwa ya hadhi ya spika basi ilikuwa makosa huyu mzee kuendelea kukaa humo wakati yeye si spika tena. Makosa haya ndo yanasababisha watu waone sasa katimuliwa. Hawajiulizi hiyo ni nyumba ya serikali sasa huyu mzee ana cheo gani sasa?
 
David Cameron alihama Down street 10 masaa machache tu baada ya Theresa May kuwa confirmed na Malkia kuwa waziri mkuu sasa huyu mzee miaka yote hiyo baada ya baraza kuvunjwa bado anangangania nyumba y serikali?
Halafu mleta mada anataka kutuaminisha kafukuzwa, kwani ilikuwa yake mzee?
 
Tatizo naloliona hapa mtoa maada hakusoma uchumi na hajasoma kitu kinaitwa Commnication Economy,Angekuwa amesoma hivyo vitu asingeweza kuandika habari hii inayoonekana imekaa kiuchonganishi.Nchi yoyote ile hapa mtumishi wa umma unapostaafu huwa unapaswa kuhama kwenye nyumba ya serikali immediatrly baada ya kukabidhi ofisi.Tanzania hata Rais anapostaafu huwa anaondoka ikulu na kurudi nyumbani kwake haraka.Lakini kwa Samweli sita ana miaka zaidi ya arobaini anatumikia Tanzania alitakiwa awe amejenga makazi yake binasfi .Na Ninaamini atakuwa alifanya hivyo.Hapo mwandishi kabla ya kuandika alipaswa kufikilia nini anaandika.
Nawewe ni mnafiki na mwenye kujipendekeza hizo sheria unazozisema zilikuwa wapi siku zote maana S.Sitta ameondoka kwenye utumishi siku nyingi.Unachotakiwa kusema ni kwamba sitta hana msaada tena kwenye chama kazi aliyotumwa imekwisha sawa na ganda la muwa au kalai la la kubebea zege
 
Kwa kawaida nyumba za wakubwa siyo za kudumu kwa mhusika. Pindi anapomaliza muda wake inabidi aondoke ili mrithi wake aitumie.

Kinachowauma nyumbu ni Serikali kuwawahi kwa kuwafilisi hoja maana Jumatatu ndugu yangu Vuta Nikuvute angekuja na hoja ya Mhe. kutohama kwenye nyumba.

Kwa suala hili maprofessional wa kulalamika lazima wangezama kwenye fani zao za ulalamishi kwa hali yoyote ile.
 
Kama amestaaf kutumwa na serikali ni muhimu kupisha watumwaji wengine ili tujenge Taifa letu Tanzania
 
Haaa haaaa laana ya kuwatusi maaskofu inaendelea kumtafuna.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom