Sitta alaani katuni ya Bunge iliyochorwa Kenya...

Sitta alaani katuni ya Bunge iliyochorwa Kenya...

Ile katuni imechorwa na Mwampembwa mtu wa Mbeya lakini kikazi yupo based Kenya, kwahiyo ni katuni iliyochorwa na Mtanzania aliyechoshwa na Bunge hili hasa la ana makinda (Jina la Speaker wetu siku zote naliandika kwa herufi ndogo)

unapoandika hivi uwe na uhakika kama kenya hakuna kikosi cha kung'oa kucha na meno bila ganzi ambacho kinafungamana na ccm, au uwe umejiridhisha kuwa angalau wanatumia ganzi.
 
Mchoraji ni MTANZANIA akiitwa GODFREY MWAMPEMBA na analindwa na katiba kufanya hivyo tatizo liko wapi?

gado.png
Tatizo linaanzia kwamba "Mkenya" ndiye kachora hivyo.
Wengine,tokea mwanzo tulijua ni Mtanzania aliyechora,LAKINI:
Kwa sababu siku hizi Watanzania wengi tumejitoa Ufahamu wa kuchanganua mambo kutegemea akili yetu,basi tumekuwa watu wa kusubiri "tulishwe maneno" kama vile "MAJANGA","DHAIFU","UDINI", ili tuanze na sie kuyaimba,huku hatujui nini hasa kinasemwa.

Wamarekani Weusi,wao wenyewe kwa wenyewe wanaona FAHARI sana kuitana NIGER(NEGRO_BLACK)
LAKINI huwa wanakuwa wakali kama MBOGO,pale MZUNGU/WHITE anapowaita kwa jina hilohilo:NIGER

Mambo mangapi na habari ngapi zichukizazo ama kukera,zinazoandikwa na Waandishi ama SISI wananchi,against Tanzania na Viongozi wetu,lakini hawahamaki kwa style hiyo?
Acha tuitane na tuchorane wenyewe kwa wenyewe(tusichukie),lakini inpotokea Mkenya anatuchora,Je sisi tukiwachora ya kwao patakalika?Fikiria kipindi kile cha Uchaguzi 2008,sie huku tungekuwa tunachora vikatuni vya tume zinavyofanya kule na wanasiasa wafanyavyo,hasa baada ya Uchaguzi.....Je wangefurahi?
(Najua aliyechora hii picha ni mtz...lakini hapo ninadiscuss kwamba kwanini Watanzania tusingefurahi kama ni kweli ni mkenya aliyechora)
 
Samwel Sita Watanzania wa Leo sio wale wa miaka ya 60!
 
Yaani jambo limetokea sijui miezi kadhaa ndio analaani leo?
He he he he, ama kweli hii ni kasi mpya
Alikuwa hajapata jukwaa la kukamulia ujumbe huo. Je ujumbe una ukweli au la? Siyo kukanusha tu.
 
Maneno yakitafsiriwa kwenda kwenye pic/katuni..tunabaki uchi.!

Ndiyo maana wazungu wasema "A picture is worth a thousands words" pale kaonyesha kila kitu. Kwani Seru-kamba alitukana tusi kubwa lakini wala hakuchukuliwa hatua ila yule aliyeomba MWONGOZO ndo maana mama SIPIKA (sijakosea hapa) amelala fofofo^2000
 
hivi mtaanza kutetea taifa lenu mpaka siku cdm itakapoingia madarakani au na huku mnajiita wazelendo au mko likizo sasa
kwa hiyo kwa bunge limekaa kama lilivyo(kiccm) kwa mtu yyt kutoka njee ya mipaka yetu ndio atutusi kwa anavyotaka yy
hata kama ndio lakini tusiruhusu mtu au kikundi kuingilia masuala ya ndani kama tu hayako nje na haki za kibanadamu....ila dharau na kejeli tusishabikie atakama anayesemwa ni ninani
 
asema jambo hilo si la kiuungwana wala si la kiurafiki na ujiran mwema.linaweza chochea mgogoro

kinachomsumbua Sitta ni unafiki! Akiwa pembeni anaponda utendaji wa Anna Mkinda!! Hadharani anagugumia rohoni!
 
Nakumbuka enzi za Punch ya ukweli UDSM. Lakini labda Mh Sitta hakuwahi kuona Punch.
 
tatizo watanzania hawapendi kuambiwa ukweli ,mambo yanayoendelea humo bungeni yanashabihiana na hiyo katuni.Kwani aliyo fanya Serukamba yanatofautiana vipi na picha yake.
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amelaani katuni ya kuwakashifu wabunge wa Bunge la Tanzania iliyochorwa kwenye gazeti la Sunday Nation la Kenya hivi karibuni na kusisitiza kuwa hatua hiyo haikubaliki.
Sitta alitoa msimamo huo jana mjini hapa wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/2014.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni gazeti la Sunday Nation la Kenya kupitia kwa mchora katuni wao, lilichapisha katuni ikionesha wabunge wa Bunge letu wakiwa kwenye ulevi huku wamevaa nguo fupi za hovyo.
“Kitendo hicho ni kibaya, kisichoonesha ujirani mwema wala urafiki. Ni kitendo cha kihuni, kinachoweza kuchochea maelewano mabaya,” alisema.
Waziri Sitta alisisitiza kuwa wanalaani kwa nguvu zote jitihada zozote zinazojaribu kulidhalilisha Bunge hilo tukufu.
Alifafanua kuwa ni kweli mara nyingine Bunge hilo linakuwa na mjadala mkali, lakini kuwalinganisha wabunge na ulevi na nguo nusu uchi hata kama metumika michoro kujaribu kukwepesha, hiyo haikubaliki hata kidogo.

................Raya pia aligusia uhuru wa habari kwa nchi wanachama huku akinukuu taarifa ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ya Mei 20 mwaka huu ambayo ilisema kuwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameamuru kufungiwa kwa gazeti la kila siku la nchi hiyo la “The Daily Monitor”, na gazeti lingine la “Red Pepper”.
Hatua hiyo ni kutokana na kuchapisha habari iliyofichua njama za Rais Museveni za kumuandaa mtoto wake, Muhoozi Kainerugaba ambaye ni brigedia wa jeshi kuwa rais wa nchi hiyo baada ya yeye kuondoka madarakani.
Hata hivyo, baada ya kuhitimisha hotuba yake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi aliomba mwongozo wa kiti akitaka wapinzani wakemewe kwa kukiuka kanuni na kutaja majina ya viongozi wakuu wa nchi kwa dhihaka.
“Mimi sitaki kuzungumzia suala la Kinana maana hizo ni porojo wacha waendelee, lakini nazungumzia ukiukwaji wa makusudi wa kanuni na kumtaja Rais Museveni kwa mambo ambayo eti msemaji ameyasikia kwenye redio pamoja na lile la Kinana japo tumeishajibu, lakini wanaendelea kujifurahisha. Naomba ukemee jambo hili,” alisema.

Source: Tanzania Daima

Ukisoma hiyo taarifa hapo juu unaweza kuona mkanganyiko wa mwazo ya Mawaziri hao 2 kutoka CCM. Sitta analaani Gazeti la Daily Nation la KENYA kwa kuchapisha KATUNI inayolidhalilisha Bunge la Tanzania kwa mchoro unaoonyesha Wabunge wa CCM wakiwa mamelewa na wengine wako nusu uchi.

Lukuvi yeye anaomba mwongozo wa Spika kukemea kauli ya msemaji wa KUB kuhusu Bajeti ya Afrika Mashariki kwa kuzungumzia kuhusu Uhuru wa vyombo vya Habari kwa kunukuu radio ya BBC kuhusu Serikali ya Uganda kuyafungia Magazeti ya Uganda, The Monitor na The Red Pepper kwa kuandika na kufichua siri za Museveni kuhusu mpango wa kumwachia Madaraka mwanae atakapostaafu!!!

Chama kimoja,serikali moja lakini mawazo tofauti. Aibu kwa ma-CCM!


[TD="bgcolor: #ffffff"]
Sitta: Hatutakubali Bunge lidhalilishwe
Edson Kamukara, Dodoma

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
amka2.gif
[/TD]

Angekiri kuwa kuna udhaifu mkubwa wa bunge unaolitia hasara taifa letu, na aahidi kupigania kulirudishia hadhi bunge kwa kuadvocate kutetea wananchi na si mafisasi, HUYU MZEE ANAJIDHALILISHA SASA
 
Mwaka jana sabasaba nilisoma gazeti moja hivi silikumbuki jina la Mwaka 1964, linasema kijana wa TANU anaeitwa Samweli Sitta ameende marekani alikoende kuiwakilisha nchi kwenye mambo muhimu huko....!!

Ajabu, Sitta toka mwaka 1964 ni kiongozi nchi...mfululizo...amaefanya nini cha maana kuikomboa nchi kutoka katika mikono ya mafiisadi wakiongozwa na watawala wenyewe?

Anetetea tu tumbo lake ....ili aendelee kula makuku ya ulaya aliyozoea kuyala toka akiwa na miaka 18 hadi sasa anakaribia 80!!
 
Hivi Sunday Nation la Kenya ndiyo wanadhalilisha bunge au Serukamba na wenzake ndiyo wanalidhalilisha? Bila Serukamba na wenzake...Sunday Nation la Kenya wangepata wapi mawazo ya kuwachora wabunge wa Tanzania wakilidhalilisha Bunge..!?
 
Mwaka jana sabasaba nilisoma gazeti moja hivi silikumbuki jina la Mwaka 1964, linasema kijana wa TANU anaeitwa Samweli Sitta ameende marekani alikoende kuiwakilisha nchi kwenye mambo muhimu huko....!!
Ajabu, Sitta toka mwaka 1964 ni kiongozi nchi...mfululizo...amaefanya nini cha maana kuikomboa nchi kutoka katika mikono ya mafiisadi wakiongozwa na watawala wenyewe?
Anetetea tu tumbo lake ....ili aendelee kula makuku ya ulaya aliyozoea kuyala toka akiwa na miaka 18 hadi sasa anakaribia 80!!


Ukitaka kuona ujinga wa nchi yetu ni kama hivi, yaani viongozi hawapendi changamoto hata kidogo. Jiulize huyu mtu toka mwaka 1964 yeye bado yupo tu madarakani na hajawahi kufanya chochote cha maana, why is he still there na analilia madaraka bado? Sitashangaa akija gombania urais in his 90's.
 
mbona hakusema wakati linadhalilishwa kwa kuchaguliwa spika kwa kigezo cha jinsia tu.
 
Huy mzee ningemwelewa kama angewaambia wabunge wenzake athari za kutumia lugha za matusi bungeni ni kuwapa fursa hata majirani zetu kututukana. Kama mzee angewaasa watu kama Lusinde na Serukamba kutumia lugha za staha.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Sitta na ccm wengine ni mfano wa mbuni anayeficha kichwa chini ya mchanga bila kujali mwili wote unaonekana vema.

Cartoon ilichorwa ku-potray matusi aliyotukana serukamba, nkamia, nchemba nk.

Huyu samuel sitta anaingilia kazi ya sanaa inayowasilishwa kwenye jamii kwa njia ya cartoon tena yenye nia njema ya kukanya na kukemea waheshimiwa wanaobadili matumizi ya bunge.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Sitta amefanya kosa la kiufundi maana hiyo kauli yake itabaki kwenye vitabu vya bunge, pia kipande cha gazeti hilo chenye katuni hiyo kitatunzwa kama kielelezo. Kumbe, alichokifanya ni kutunza historia ya uhuni ulifanywa na wabunge wa ccm chini ya uspika wa Makinda.
 
Back
Top Bottom