Sitta alaani katuni ya Bunge iliyochorwa Kenya...

Sitta alaani katuni ya Bunge iliyochorwa Kenya...

makoye2009

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Posts
2,638
Reaction score
1,219
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amelaani katuni ya kuwakashifu wabunge wa Bunge la Tanzania iliyochorwa kwenye gazeti la Sunday Nation la Kenya hivi karibuni na kusisitiza kuwa hatua hiyo haikubaliki.

Sitta alitoa msimamo huo jana mjini hapa wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/2014.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni gazeti la Sunday Nation la Kenya kupitia kwa mchora katuni wao, lilichapisha katuni ikionesha wabunge wa Bunge letu wakiwa kwenye ulevi huku wamevaa nguo fupi za hovyo.

“Kitendo hicho ni kibaya, kisichoonesha ujirani mwema wala urafiki. Ni kitendo cha kihuni, kinachoweza kuchochea maelewano mabaya,” alisema.

Waziri Sitta alisisitiza kuwa wanalaani kwa nguvu zote jitihada zozote zinazojaribu kulidhalilisha Bunge hilo tukufu.

Alifafanua kuwa ni kweli mara nyingine Bunge hilo linakuwa na mjadala mkali, lakini kuwalinganisha wabunge na ulevi na nguo nusu uchi hata kama metumika michoro kujaribu kukwepesha, hiyo haikubaliki hata kidogo.

................Raya pia aligusia uhuru wa habari kwa nchi wanachama huku akinukuu taarifa ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ya Mei 20 mwaka huu ambayo ilisema kuwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameamuru kufungiwa kwa gazeti la kila siku la nchi hiyo la “The Daily Monitor”, na gazeti lingine la “Red Pepper”.

Hatua hiyo ni kutokana na kuchapisha habari iliyofichua njama za Rais Museveni za kumuandaa mtoto wake, Muhoozi Kainerugaba ambaye ni brigedia wa jeshi kuwa rais wa nchi hiyo baada ya yeye kuondoka madarakani.

Hata hivyo, baada ya kuhitimisha hotuba yake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi aliomba mwongozo wa kiti akitaka wapinzani wakemewe kwa kukiuka kanuni na kutaja majina ya viongozi wakuu wa nchi kwa dhihaka.

“Mimi sitaki kuzungumzia suala la Kinana maana hizo ni porojo wacha waendelee, lakini nazungumzia ukiukwaji wa makusudi wa kanuni na kumtaja Rais Museveni kwa mambo ambayo eti msemaji ameyasikia kwenye redio pamoja na lile la Kinana japo tumeishajibu, lakini wanaendelea kujifurahisha. Naomba ukemee jambo hili,” alisema.

Source: Tanzania Daima

----------
Ukisoma hiyo taarifa hapo juu unaweza kuona mkanganyiko wa mwazo ya Mawaziri hao 2 kutoka CCM. Sitta analaani Gazeti la Daily Nation la KENYA kwa kuchapisha KATUNI inayolidhalilisha Bunge la Tanzania kwa mchoro unaoonyesha Wabunge wa CCM wakiwa mamelewa na wengine wako nusu uchi.

Lukuvi yeye anaomba mwongozo wa Spika kukemea kauli ya msemaji wa KUB kuhusu Bajeti ya Afrika Mashariki kwa kuzungumzia kuhusu Uhuru wa vyombo vya Habari kwa kunukuu radio ya BBC kuhusu Serikali ya Uganda kuyafungia Magazeti ya Uganda, The Monitor na The Red Pepper kwa kuandika na kufichua siri za Museveni kuhusu mpango wa kumwachia Madaraka mwanae atakapostaafu!!!

Chama kimoja,serikali moja lakini mawazo tofauti. Aibu kwa ma-CCM!
 
Kwa wenye akili ndivyo wanavyoliona Bunge wakitazama TV, Six hajuwi tu kwa kuwa huwa hajioni akiwa Bungeni live. Ile katuni mimi nimeikubali kichizi.
 
ndo wanajua leo wabunge wa ccm wote walevi
 
Yaani jambo limetokea sijui miezi kadhaa ndio analaani leo?
He he he he, ama kweli hii ni kasi mpya
 
Huo ndo mtazamo wetu wengi kwa BUNGE la JMT....
 
Kwa hili la katuni Six anazidiwa na Dungai? aibu
 
asema jambo hilo si la kiuungwana wala si la kiurafiki na ujiran mwema.linaweza chochea mgogoro


Atwambie kama ni ukweli au uongo ..................... ndiyo hali halisi ya sasa ya bunge letu.

By the way aliyechora katuni ni Mtanzania ............... blood in blood out!!
 
Sitta tatizo lipo wapi? Je ni Uongo? ujirani unaharibika vipi? ndio unataka kugombea urais?
941506_411322565633180_1312344154_n.jpg
 
laana hiyo imwendee Juma Nkamia na Serukamba na sio mchora kibonzo
 
Kwa wenye akili ndivyo wanavyoliona Bunge wakitazama TV, Six hajuwi tu kwa kuwa huwa hajioni akiwa Bungeni live. Ile katuni mimi nimeikubali kichizi. We huoni wameacha kuropoks siku hizi!

"If fail to design Users design for U"

Bunge fail to portrait the manner, viewers portrait for the them.
 
Ile ni katuni na ninashangaa kwa bwana SIX kuhamaki kama vile sio msomi ambae anatakiwa aiangalie ile katuni kwa makini na kufanya analysis based na kile kinachotokea bungeni. Tatizo letu lingine ukumbi wa bunge letu una-promote fujo na watu kutokuwa serious maana unakuta wabunge wawili wanageukiana na kupiga story wakati mjadala unaendelea (kutokana na kuwa na space na viti vyao vya kuzunguuka), kwahiyo seating arrangement pekee inafanya wabunge kuwa wavivu kushiriki kikamilifu pamoja na utoro. Embu check seating arrangement ya Kenya, ukumbi upo simple na unafanya watu wanakuwa serious na discussion.

Ukumbi wetu mkubwa, mzuri kupindukia kushinda hata kumbi za mataifa mengine makubwa ajabu serikali yetu MAKUSANYO MADOGO wakati huohuo Ukumbi mfano kama wa Kenya upo simple na seating arrangement ya kubanana lakini upande wa MAKUSANYO YA SERIKALI NI MAKUBWA KULIKO SIE. Serikali yetu inafikiria kama sie raia wengi tunavyofikiria yaani "umaridadi uficha umasikini"
 
Bunge la Tanzania liwe la hovyo au liwe makini sana, bado, si sahihi kabisa kwa nchi nyingine kuchora katuni juu ya yanayoondelea kwenye nchi nyingine -huru. It is up to Tanzanians to say whatever they like about their country. Kenya, wana tabia ya kuinigilia affairs ambazo haziwahusu, na kwa hakika katuni hii inakwenda kinyume na staha za ujirani mwema.

Ni lini Tanzania ilichora katuni kuhusu bunge la Kenya? Hivi ni kweli bunge lao halina vituko? Mzee Sitta yuko sahihi. Kenya should mind their own business.
 
Mchoraji ni MTANZANIA akiitwa GODFREY MWAMPEMBA na analindwa na katiba kufanya hivyo tatizo liko wapi?
Mkuu, nimeamini kweli hakuna mtu makini CCM, kama hata SIX anaongea upuuzi huu, kweli wamefilisika kimawazo, wamefika mwisho!

:closed_2:
 
analaani nini kwani katuni si inaonyesha ukweli ulivyo, tatizo wabunge wa CCM hawajuhi lakini sie tunaowatazama kupitia luning ndio wanavyoonekana
 
Back
Top Bottom