Sitta alaani katuni ya Bunge iliyochorwa Kenya...

Sitta alaani katuni ya Bunge iliyochorwa Kenya...

[h=2]Sitta ang’aka, aionya Kenya [/h]
[h=5]WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki, Samuel Sitta, ameionya Kenya kutokana na mipango yake ya siri ya kuichafua Tanzania. Sitta alisema mipango hiyo ya Kenya imedhihiri baada ya gazeti la Sunday Nation kuchora katuni ambayo ililifananisha Bunge la Tanzania na klabu ya pombe[/h]

kwani kilichokosewa ni kitu gani?
mchoraji wa cartoon yupo sahihi kabisa.
sita aache kujidharirisha kwa kutetea upuuzi ambapo kila mwenye macho na masikio huona na kusikia kiendeleacho kwenye bunge hovyo la sasa.
 
Sitta ang'aka, aionya Kenya


WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki, Samuel Sitta, ameionya Kenya kutokana na mipango yake ya siri ya kuichafua Tanzania. Sitta alisema mipango hiyo ya Kenya imedhihiri baada ya gazeti la Sunday Nation kuchora katuni ambayo ililifananisha Bunge la Tanzania na klabu ya pombe

Naamini Mh. 6 anapoteza fahamu. Kuna nini ambacho sio cha kweli kwenye kile KIKARAGOSI? Mbona kila kitu ni kweli tupu!!! Juma Nkamia alisema nini? Lusinde alisema nini? Na Serukamba alisema nini?

UKIUZA UTUMBO USIKIMBIE NZI. Mzee 6 asifanye kutojua kwamba hawezi kulinganisha Bunge la Kenya na Bunge la Makinda na Ndugai. Kila kilicho chorwa pale ni ukweli mtupu kwani ile ni lugha ya picha hivyo kila mtu anapata tafsiri yake.

Tusi la Serukamba halina tofauti na kile anacho kifanya kwenye kile Kikaragosi. Nani asiye juwa kwamba Malavidavi yana endekezwa kwa sana na hawa waheshimiwa! Nani asiye jua kwamba waheshimiwa hawa kukesha kwao kwenye kumbi za starehe wanaishia kuuchapa usingizi ndani ya ukumbi wa Bunge!

Nani asiye sikia lugha na kauli anazo zitumia Spika hazilingani na heshima ya kile kiti! (Spika anapo sema tusitafutane, na maneno mengine kadha wa kadha ana maana gani kulingana na heshima ya kile kiti?).

Mh. 6 asikatae aibu yao. Na hii ni fedheha kwa waTanganyika wote.
 
, Mlanje, Asnam, R.B, Isaac JK,

..mchoraji wa hizo katuni ni Mtanzania.

..kipaji chake cha uchoraji ndicho kilichomtoa Bongo kwenda kufanya kazi Kenya.

..jina lake ni Geofrey Mwampembwa au "GADO."

..tusubiri atakuja na jibu/katuni gani kufuatia onyo la Mzee Sitta.


gado.png


gado.jpg


av.1.godfrey.mwampembwa.cnn.640x360.jpg


DSC01940.JPG



http://edition.cnn.com/2009/WORLD/africa/11/04/africanvoices.gado/index.html


 
Nimestaajabu sana na kauli ya Sitta. Kwani kila maoni ya Mkenya au mtu anayefanya kazi Kenya ndiyo maoni ya Kenya? What a ridiculous and preposterous notion!
 
Mchoraji wa hiyo katuni ni mtanzania mwenzetu anaitwa Mwampembwa. Huenda anaguswa na kinachoendelea bungeni nchini kwake. Lakini mbona hata hapa hapa nyumbani kuna wimbo ulitungwa wa 'Bunge Kariakoo' uliokuwa na tafsiri ya bunge la ovyo ovyo??. Mimi naona ni maoni tu ya watu ambayo sio maoni ya wote. Hata hivyo, wachoraji wetu nao si wanaweza kuchora chochote kutoka nchi za jirani? Mbona viko vingi tu kama vya ukabila, unyonyaji na vingine vingi tu na tukawapiga dongo zito tu?. Asante
 
Tafadhali tutake radhi sisi tunaoenda kwenye vilabu vya pombe. Kwenye vilabu vya pombe hakuna utovu wa nidhamu kama tulivyoshuhudia kwenye bunge linaloendelea...

Klab ya pombe hatutoi watu kucha
 
Tafadhali tutake radhi sisi tunaoenda kwenye vilabu vya pombe. Kwenye vilabu vya pombe hakuna utovu wa nidhamu kama tulivyoshuhudia kwenye bunge linaloendelea...
Pamoja sana... Ata'dabu!
 
Sita aache kuyumbisha mambo wakenya wako sahihi maana bunge chini ya uongozi wa Makinda ni zaidi ya hiyo katuni,Sita anasemaje juu ya Serukamba kumtukana mbunge mwenzake"---- you" na spika hakumwadhibu, hivyo hiyo katuni inasema ukweli

Kwa taarifa yako, Sitta na wengine.... aliyechora katuni hiyo ni Mtanzania anyeishi na kufanya kazi Nairobi, jina lake ni Godfrey Mwampembwa a.k.a Gado!
 
Ukifanya upuuzi unadhani wa nje hawauoni? Mbona kuna katuni za Ukeketaji wanawake zilichorwa na watu wa nje kwa nini hawakulalamika?
 
Sitta ni bure.
Mzee mnafiki tu yule, haonyeshi busara tofauti na mwigulu.
 
Sisi wenyewe tulisema Ukiwa na mtoto huwezi kutazama bunge,sasa wakenya pia wanaangalia,na wanaona uhuni unaofanywa na wabunge wetu,CDM wajirekebishe wanatuaibisha.
 
nae sitta kafirisika kimawazo kwenye ukweli acha usemwe ukweli.katuni kaona ni aibu kwa bunge mbona ufisadi wa chama chake hasemi kuwa ni aibu kwa wananchi wa tz.kumbe ukweli unauma siku zote.
 
Sisi wenyewe tulisema Ukiwa na mtoto huwezi kutazama bunge,sasa wakenya pia wanaangalia,na wanaona uhuni unaofanywa na wabunge wetu,CDM wajirekebishe wanatuaibisha.

he! yamekuwa hayo tena!
ni kweli kabisa CHADEMA inawanyima usingizi.
 
Ndio ukweli wenyewe.... Wazee wa mipasho.
 
Kazi yake kupambana na kioo!!anaogopa taswira yake mwenyewe?Sitta muda umekupita ungepumzika ulee wajukuu sasa,hii nchi sio yako pekeyako na bila wewe nchi itaenda tu!uwike usiwike kutakucha tu!hana jipya!
 
What is Sitta Talking about Mnafiki mkubwa huyu, kwanza atoke kwenye nyumba ya spika aliyoing'angania mchumi tumbo mkubwa, mwizi wa fedha zetu anataka tuanze kutoa vimemo vyake vyote vya wizi aliokua anaufanya na Tom Kashilila pale bungeni? eti wamedhalilishwa hivi yeye anatufanya wajinga sana sisi? kodi zetu hizo wanazoendelea kuzichoma bila kufanya kazi yoyote kajaa majungu, mnafiki mkubwa ndio maana hata chama chake kimemuweka kando, ngoja Lowassa arudi atakoma atakanvyonyonyolewa manyoya
 
Katuni ililenga kuonesha jinsi bunge lilivyokuwa limezidi kwa matusi na maneno 'mbofumbofu', badala ya kujadili hoja za msingi. Watu wasikwepe kukosolewa kwa mwanvuli wa mahusiano ya kidiplomasia!Pamoja na yote, mchora katuni, 'Gado',Mwampemba ni Mtanzania anayefanya shughuliza zake Kenya!
 
Back
Top Bottom