Sitta alaani katuni ya Bunge iliyochorwa Kenya...

Sitta alaani katuni ya Bunge iliyochorwa Kenya...

Namwomba Gayo achore katuni nyingine ya Sita akilia Bungeni huku kashika chupa ya mvinyo na suruali kavaa Kata k

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Aibu tupu. Naona CCM wamelewa madaraka na sasa wanaanza kuvuka mipaka na kuingilia uhuru wa vyombo vya habari vya mataifa mengine!
 
Acha mdharauliwe nyie ni mafisadi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Bunge kamwe haliwezi kudhalilishwa na katuni bali bunge la Tanzania linadhalilishwa na Wabunge wa magamba. Sitta naye aache usanii aseme ukweli kama ambavyo unajulikana na Watanzania wengi kuhusu Bunge hili lenye kututia aibu kubwa.
 
Ninge muelewa Mr Six kama angemshauri spika jinsi ya kuliongoza bunge kikanuni na taratibu sio kulalamika wananchi kuwasilisha fikra zao jinsi bunge liluvyo kituko kwa sasa.
 
Sijui kwanini hawa watu hawapendi kuambiwa na kuuona ukweli. Hivi mchoraji ndo kaliaibisha bunge au mwenendo wa bunge ndo unaliaibisha bunge? Alichokifanya mchoraji ni kudepict yanayoendelea mjengoni.

Mshindwe kumlaumu Serukamba, J. Ngamia oh sorry I meant J. NKAMIA, Makinda and Co. Mumlaumu mchoraji?
 
Mbona Ndugai alisema anampongeza mchoraji?

Kwa jinsi tunavyojipendekezaji, nauhakika angekua ni mchoraji wa Tz kachora bunge la Kenya na Wabunge wa Kenya kulaani bungeni, basi huyo mchoraji angepata shida sana kwa hao viongozi tulionao kwa kile kitachokua kimeitwa kuvuruga ujirani mwema.
Na si ajabu ingeundwa tume ya kwenda kuomba msamaha.
 
Samuel Sitta ni CCM pure. Kama kawaida huwa wanakemea mambo ambayo hayana madhara kwa taifa na kuacha kukemea mambo ambayo yanalihujumu taifa. Badala ya kukemea ufisadi wa taifa na uongozi mbaya bungeni yeye anamkemea mchora katuni. Katuni kazi yake kuchekesha, yeye alitaka mchora katuni achore kitu gani.
 
ha ha ha sasa analaani nini katuni inayodepict ukweli mtuuuuupu wa utendaji mbovu wa moja ya chombo chetu kikubwa jamani??.......
 
[h=2]Sitta ang’aka, aionya Kenya [/h]
[h=5]WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki, Samuel Sitta, ameionya Kenya kutokana na mipango yake ya siri ya kuichafua Tanzania. Sitta alisema mipango hiyo ya Kenya imedhihiri baada ya gazeti la Sunday Nation kuchora katuni ambayo ililifananisha Bunge la Tanzania na klabu ya pombe[/h]
 

Attachments

  • BUNGE.jpg
    BUNGE.jpg
    15.9 KB · Views: 486
Sita aache kuyumbisha mambo wakenya wako sahihi maana bunge chini ya uongozi wa Makinda ni zaidi ya hiyo katuni,Sita anasemaje juu ya Serukamba kumtukana mbunge mwenzake"---- you" na spika hakumwadhibu, hivyo hiyo katuni inasema ukweli
 
Kuna uhuru wa maoni Kenya. Msanii akichora katuni isiyomfurahisha Sitta sio kosa la serikali ya Kenya. Ni lini hawa wazee watakomaa kimawazo?
 
hahaha nimeamua kuisave kabisa hii cartoon
 
Aonge na waziri wa sheria ili muswada wa kuwafungie uwe tayari.Si nasikia hawana geshi supa kama la kwetu.Nasikia wana askari polisi tuu.na wale wanaowadhibu all shabab ni wa kukodi.


Membe yupo wapi atoe tamko?Na mara moja yafungiwe.

Ila hata mimi nikiangalia akina ndugai naona kapiga kinywaji, nikimwangalia mama napat ataabu jua kama atamaliza session, nikimwangalia mhagama kama yupo ktk kilabu cha ulazi halafu kaporwa mume.

Hao wengine utandahi wameshiba maharagwe ktk joto kali.

Kweli artist wa Kenya ni soo(Ingawa anaweza kuwa ni gayo) ila kafiti kenya.Perfect observation.
 
, Mlanje, Asnam, R.B, Isaac JK,

..mchoraji wa hizo katuni ni Mtanzania.

..kipaji chake cha uchoraji ndicho kilichomtoa Bongo kwenda kufanya kazi Kenya.

..jina lake ni Geofrey Mwampembwa au "GADO."

..tusubiri atakuja na jibu/katuni gani kufuatia onyo la Mzee Sitta.
 
Last edited by a moderator:
Sita aache kuyumbisha mambo wakenya wako sahihi maana bunge chini ya uongozi wa Makinda ni zaidi ya hiyo katuni,Sita anasemaje juu ya Serukamba kumtukana mbunge mwenzake"---- you" na spika hakumwadhibu, hivyo hiyo katuni inasema ukweli

Anapoteza ufahamu baaada ya kupewa wizara isiyo na tija wala maana
 
Sitta ang'aka, aionya Kenya


WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki, Samuel Sitta, ameionya Kenya kutokana na mipango yake ya siri ya kuichafua Tanzania. Sitta alisema mipango hiyo ya Kenya imedhihiri baada ya gazeti la Sunday Nation kuchora katuni ambayo ililifananisha Bunge la Tanzania na klabu ya pombe

Tafadhali tutake radhi sisi tunaoenda kwenye vilabu vya pombe. Kwenye vilabu vya pombe hakuna utovu wa nidhamu kama tulivyoshuhudia kwenye bunge linaloendelea...
 
Back
Top Bottom