Sitamani kuzaa mtoto wa kike

Sitamani kuzaa mtoto wa kike

Watoto wakike niwazuri sana tena hawana shida sema2 sehemu zao za siri ni hatarishi kwao ndo mana wanaaibika.
 
Molembe

Naomba nikushauri kuwa mtoto ni mtoto, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. unaweza kuwa na watoto wa kiume mia moja wakakupa mateso matupu, hujasikia watu wana watoto mashoga? je ungependa hilo zaidi badala ya kuwa na mtoto wa kike mwenye tabia nzuri?

Vipi je ungefurahia kuwa mzazi wa mtoto wa kiume aliyepost picha za binti mtandaoni? au ungefurahia kuwa na mtoto wa kiume aliyempa binti mimba, kwa sababu tu ni mtoto wa kiume.

Muombe mungu upate hata huyo mtoto kwanza, kuna watu wanaiba watoto, wewe hata huna mtoto tayari unapanga na kukataa wengine. Jifikirie tena na muombe Mungu akikujalia akupe mtoto yeyote na wewe jukumu lako ni kumlea kwenye uelekeo unaofaa, akiamua yeye kufanya anavyofanya basi ni yeye.
Je wewe leo hii hapo mzazi wako anakufuatilia unafanya nini? utamfuatilia mwanao wa miaka 25 alie chuo kikuu?.

Ni hayo tu.
 
Last edited by a moderator:
magode

Huyu jamaa na atubu kabisa, hakika atakuwa na uzao jike pekee jinsi nitakavyo mtoto wa kike wengine hawawataki, nina midume ishaanza kunikunjia ngumi,mashati yangu wanavaa mda si mrefu shaving machine tutashare natamani sana katoto ka kike.
 
Last edited by a moderator:
Jiwe limerushwa gizani.....

hapana , nilivyoelewa mm ni kwamba anashangaa mleta mada kuwapondea watoto wa kike wakati kwake yeye anaona wana faida kuliko hao wa kiume ambao wengi wao wameharibikiwa kwa kufanya mambo ya kusikitisha.
 
Wazazi ndio tatizo. Wameshindwa lea watoto wanawaachia wafanyakazi, ndugu na boarding.
Wanaachia bila kuwafundisha madhara ya vile wafanyavyo.
Hawawaelezi ukweli kuhusu maisha na kumcha Mungu.
Zaidi tuombe Mungu atuokoe
 
huyu jamaa na atubu kabisa, hakika atakuwa na uzao jike pekee,,,,, jinsi nitakavyo mtoto wa kike....wengine hawawataki,,, nna midume ishaanza kunikunjia ngumi,,,mashati yangu wanavaa.... mda si mrefu shaving machine tutashare......natamani sana katoto ka kike....

Mkuu pole sana ila hapo kwenye red inawezekana huwajali watoto wako au unajipenda kupita kiasi jaribu kuwanunulia nguo nzuri kama zako uone kama watavaa zako.
 
Wazazi ndio tatizo. Wameshindwa lea watoto wanawaachia wafanyakazi, ndugu na boarding.
Wanaachia bila kuwafundisha madhara ya vile wafanyavyo.
Hawawaelezi ukweli kuhusu maisha na kumcha Mungu.
Zaidi tuombe Mungu atuokoe

Mkuu Root asante kwa ushauri lakini tukumbuke kuwa wakati mwingine haya ufanywa kwa mabinti ambao ni watu wazima hebu fikria mdada ambae ni daktari mtarajiwa anapiga picha za uchi na hapa tuwalaumu wazazi kweli?
 
Last edited by a moderator:
Wewe sie unaepanga uje kupata mtoto wa jinsia fulani au ile jinsia ambayo unayoitaka wewe.

Kwahiyo tuliza boli, wewe jitahidi kutoa malezi bora/mema kwa kadri uwezavyo pamoja na kumuomba Mungu wako, mambo mengine ni matokeo tu.

Unaweza ukapata mtoto wa kiume baadae akaja kuwa teja(anatumia madawa ya kulevya) je huoni hapo ni hasara tayari?

Au naweza ukapata mtoto wa kiume baadae unakuja kusikia anagongwa na wanaume wenzake(choko) je huoni hapo ni hasara kubwa?
 
Wanaume ni wachache sana siku hizi,wajinga wengi wanafikiri kuning'iniza pumbu ndio uanaume

Dah! Colagen tutake radhi wanaume wote humu JF.
Si wanaume wote ambao wako humu JF wamefurahia hii maada hapo juu. Wengi wetu tuna watoto wa kike na hawa wa kiume pia. Lakini wengi wameeleza kuwa tabia nyingi za binadamu ziko reflected na malezi ya wazazi na hata jamii inayomzunguka. Kamwe hakuna mzazi ambaye angetamani mtoto wake awe wa hovyo! Lakini inapotokea mtoto hakulelewa katika misingi mizuri hasa ya kutomwogopa Mungu basi hupotea na kuwa wa hovyo.

Mzazi mwenye utu inapotokea anamwona binti yake ambaye amemlea pengine kwa kutumia gharama nyingi lazima imuume sana. Lakini hata inapotokea mtoto wa kiume akawa shoga si jambo la kufurahia. Ingawa nasita kuwabeza wale wanaofanya ukahaba kwa sababu za shida zao, ambao pengine hata wanasomesha watoto wao na kuwasaidia wazazi wao! Kimaadili haikubaliki lakini kama mtu anafanya kwa shida zake na hana njia nyingine, kwangu sina tatizo.

Kwahiyo sisi wanaumena nanyi wanawake tuna nafasi sawa kabisa za hisia kuhusu mtoto ambaye amepoteza mwelekeo, wako watoto wa kike wengi sana ambao ni mifano katika jamii. Wako watoto wa kike wengi ambao wanatunza wazazi wao hata familia zao, lakini watoto wa kiume au wazizi wa kiume (kina-baba) wakawa wa hovyo! Mifano iko mingi mno kuhusu hilo, angalia majirani na marafiki zako wengi tu utaona wa aina hiyo.

Mwisho wa siku namalizia kwa kusema kuwa WATOTO WOTE NI SAWA, ni muhimu sana kuwalea katika misingi mizuri yenye kumpendeza mungu.
 
Last edited by a moderator:
Jey Efu bana...hakuna aliye bora zaidi ya mwingine na hakuna mtoto mzuri kama wa kike...
Bora miye niliye bias wazi wazi...kwangu hakuna watoto wazuri kama watoto wangu...

Wewe jitahidi kwenye malezi tu hakuna mtoto aliye bora kuliko mwingine, Kila siku huwa naambia watu hakuna mtoto mzuri kama wa kike na ni kweli iko hivyo, Ni muda wa mpito tu akiupita huwa hakuna tatzo lingne zaidi kulinganisha na hao wa kiume mnaowasema eti ni bora.
 
Molembe
Hiyo mimba anakuwa kapewa na mtoto wa kike mwenzie? Nakuombea kwa Mungu upate matoto ya kiume. Moja liwe jambazi, likuibie mpaka wewe. Jingine liwe teja na jingine liwe kibaka wananchi walitie kibiriti. Labda ndo utajua watoto wa kike wana thamani kama mama yako mzazi alivyo na thamani kwako.
Shy land
Amina. Mungu akubariki upate toto la kiume liwe shoga. Wanaume wenzie walitafune mpaka kwenye masofa ya sebuleni kwako mchana kweupe.
Heaven on Earth
Umeona eh? Nadhani hawajazaliwa na mama hawa wana watoka pabaya.
sister
Hapana, waache wajaliwe watoto wa kiume ambao watawatoa machozi na kujutia makauli yao machafu kama vyoo vya stendi ya Sumbawanga.


Hahahaaaaa...umeniacha hoi kwa hayo majibu yako. Ila umempa ukweli, yaani Molembe kuliko aone uchi wa binti yake bora mvulana wake afanywe mwanamke... mimi hii kitu inaniogopesha sana aiseee.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu pole sana ila hapo kwenye red inawezekana huwajali watoto wako au unajipenda kupita kiasi jaribu kuwanunulia nguo nzuri kama zako uone kama watavaa zako.

hapana mkuu,,,, wao wanasikia raha tuu,,, duh nawapenda sana wanangu, ni kwamba kipimo hicho cha upendo huwezi kukitambua....they knw themself.....natamani sana kungekuwa na mixer ya gal.....
 
Uko kama mimi, naomba Mungu anibariki nisipate mtoto wa laana kama Mtoto wa kike.
Jifunze kusema rafiki! Mama yako ni mtoto wa kike!!!!!!!!!!!!!! Badilisha kauli sema mungu nisaidie mtoto wangu wa kike asiniangushe!
 
Watt wa kiume wanatia huruma mjini huku acha tu..tamaa mbaya zinawaponza
 
Back
Top Bottom