Uchaguzi 2020 Sitaki kuwa mnafiki. WanaCCM awamu hii tunaburuzwa na Mwenyekiti

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,408
Anachokitaka ndicho huwa. Na anafanya mambo kwa manufaa yake ya kisiasa. Kwanini nasema haya??

1. Angalia namna mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea urais wa JMT ulivyokuwa na figisu. Eti wanaCCM wengine hawaruhusiwi kuchukua fomu. Ni yeye tu.

2. Angalia chaguzi za marudio ktk majimbo ambayo wabunge wapinzani "waliunga mkono juhudi". WanaCCM tulinyimwa kushindana nao. Na hata ktk uchaguzi huu tumepigwa marufuku kushindana nao.

3. Angalia upigaji kura ktk mkutano mkuu, ukusanyaji wa kura ulikuwa wa kimikoa (hii mbinu imewekwa ili iwe rahisi kutufuatilia wale ambao tungepiga kura ya hapana).

4. Kwa kinywa chake mwenyewe amesema kura za maoni za watia nia wa ubunge hazina maaana. Yeye amesema anaweza kumchukuwa hata mtu wa mwisho. Yaani badala ya wagombea kutafuta ridhaa ya wananchi, Sasa wanasubiri maamuzi binafsi ya mwenyekiti.

Demokrasia imezikwa rasmi ndani ya CCM. WanaCCM tunapelekwa pelekwa tu.
 
Na ile kauli yake ya kuwaambia Wapinzani hawatashinda uchaguzi wa mwaka huu nayo ina ukakasi na inatukatisha tamaa wapenda mabadiliko.

Mzee huwa anaongea tu kila kinachomjia mdomoni mwake. Hana utaratibu wa kuchuja kwanza ili kuondoa mkanganyiko usio na tija.
 
Na ile kauli yake ya kuwaambia Wapinzani hawatashinda uchaguzi wa mwaka huu nayo ina ukakasi na inatukatisha tamaa wapenda mabadiliko.

Mzee huwa anaongea tu kila kinachomjia mdomoni mwake. Hana utaratibu wa kuchuja kwanza ili kuondoa mkanganyiko usio na tija.
Nenda kapige kura, then watuoneshe kwa vitendo hiyo kauli yao, talking is always cheap.
 
Tuliwaonya huyu ni dikteta, mkafikiri udikteta utaishia kubagua wapinzani.

Nyerere alisema dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huachi.

Magufuli kasema bila aibu kwamba atamkata mtia nia yeyote, si kwa katiba, si kwa miongozo, si kwa taratibu, si kwa utamaduni,bali kwa jinsi takavyojisikia alivyoamka siku hiyo.

Yani kasema wazi yeye ni dikteta.

Kuna vikao ya kumfukuza Membe, anasema hajapeleka mjadala kwenye kikao aliogopa mjadala wa kikao, kamaliza habari mwenyewe katangaza tu. Haoni hata aibu.

Huyu dikteta ataiharibu sana hii nchi.
 
Back
Top Bottom