ACT Wazalendo: Wanachama 11 wametia nia kugombea nafasi tatu zilizotangazwa kuwa wazi, ikiwemo ya Mwenyekiti

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mnamo tarehe 17/2/2020 Chama chetu kiliondokewa na aliyekuwa Mwenyekiti wake wa Taifa hayati Maalim Seif Sharif Hamad. Kwa mujibu wa ibara za 84(4) na116(4) za Katiba ya ACT Wazalendo (Toleo la 2020) nafasi hiyo inapaswa kujazwa ndani ya miezi kumi na mbili (12).

Tayari Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia kikao chake cha tarehe 31/10/2021 na kwa kuzingatia mamlaka yake chini ya ibara za 69(2) na 84(4) za Katiba ya Chama, ilipitisha azimio la kuitishwa Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi kujaza nafasi ya Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti Zanzibar na Mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka Tanzania Bara ifikapo tarehe 29/1/2022 na kuteua Kamati Maalum kusimamia uchaguzi huo.

Kamati ya Uchaguzi ilitangaza kalenda ya kuchukua na kurejesha fomu kwa wanachama wenye nia ya kuwania nafasi hizo kuwa ni kuanzia tarehe 4/1/2022 hadi 17/1/2022.

Mpaka saa 10.00 jioni ya tarehe 17/1/2022 jumla ya wanachama 11 wametia nia kugombea nafasi tatu zilizotangazwa kuwa wazi kwa mchanganuo ufuatao:-

Uenyekiti
1. Ndugu Juma Duni Haji – kutoka Mjini Magharibi (Unguja)
2. Ndugu Hmad Masoud Hamad – kutoka jimbo la Ole (Kaskazini Pemba)

Makamu Mwenyekiti (Zanzibar)
1. Ndugu Othman Masoud Othman – kutoka jimbo la Pandani (Kaskazini Pemba)
2. Ndugu Juma Said Sanani – kutoka Mjini Magharibi (Unguja)

Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Tanzania Bara)
1. Ndugu Chrisant Joseph Msipi – Shinyanga
2. Ndugu Ester Thomas – Dar es salaam
3. Ndugu Fungo Godlove Benson – Dar es salaam
4. Ndugu Johnson Mauma Gagu – Arusha
5. Ndugu Msafiri Mtemelwa – Tabora
6. Ndugu Jafet Mark Masawe – Kilimanjaro
7. Ndugu Fidwl Hemed Christopher – Tabora

Kinachoendelea baada ya hatua hiyo:-
1. Kamati ya Uchaguzi itakaa tarehe 19/1/2022 kuandaa taarifa ya mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu kwa ajili ya kikao cha Sekretariet ya Kamati Kuu.

2. Sekretariet ya Kamati Kuu itakaa tarehe 22/1/2022 kupokea taarifa ya watia nia toka Kamati ya Uchaguzi na kuandaa kikao cha Kamati Kuu.
3. Kamati Kuu itaketi tarehe 27/1/2022 kuandaa mapendekezo ya uteuzi kwa Halmashauri Kuu ya Taifa.

4. Halmashauri Kuu ya Taifa itaketi tarehe 28/1/2022 kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa Uenyekiti, Umakamu Mwenyekiti na Ujumbe wa Halmashauri Kuu Taifa.

5. Kamati ya Uchaguzi baada ya kupata majina ya rasmi, itawatangaza kupitia mdahalo wa wazi tarehe 28/1/2022. Wagombea watapata fursa kujieleza, kuulizwa maswali na kujitangaza kuhusiana na madhumuni ya kugombea nafasi hizo.

6. Tarehe 29/1/2022 Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi utaketi katika Ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam kupiga kuwa kuchagua Mwenyekiti wa Chama, Makamu Mwenyekiti Zanzibar na Mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya Taifa

Kwa hiyo mchakato wa kuwapata viongozi wa Kitaifa kwa ajili ya kujaza nafasi zilizowazi ndani ya Chama utahitimishwa tarehe 29/1/2022.

Kamati ya Uchaguzi inapenda kuwahakikishia wanachama wote kuwa imejizatiti kuhakikisha kuwa uchaguzi unaendeshwa kwa uhuru, haki na uwazi na kuwa wa kuaminika.

Kamati ya Uchaguzi inatoa wito kwa Viongozi wa Chama wote, Wajumbe wa Mkutano Mkuu, watia nia wote na wanachama kwa ujumla kuhakikisha kuwa wote kwa pamoja tunatunza maadili ya Chama kwa kwa minajili ya kuhakikisha kuwa wanapatikana viongozi tutakaoshirikiana nao kukijenga na kukiimarisha Chama kwa mustakabli mwema wa demokrasia nchini.

Imetolewa na Kamati ya Uchaguzi

Joran Bashange
Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi
18 Januari, 2022

Zitto anajidaigi mpenda demokrasia na mchukia udikteta, lakini amekaa kama kiongozi wa chama dikteta?!!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
tunawatakia kila la heri, jambo la msingi Demokrasia itawale ktk mchakato mzima hadi uchaguzi.
 
View attachment 2086545
Hivi Kiongozi wa Chama na Mwenyekiti, nani mkubwa????
 
Ikitokea hao hapo juu ndio wakawa pekee waliojitokeza kuchukua fomu mpaka zoezi linafungwa, nakiri kusema uongozi mzima wa hicho chama kwa maana ya kiongozi wa chama, mwenyekiti na makamu wake na katibu mkuu wote watakuwa ni waislamu.
 
kwani kitakua na tofauti gani na Chadema?
 
Kuna kitu nakiona katika hiki chama , kina mfumo kama wa Iran , Ayatula yupo katika hiki chama
 
Back
Top Bottom