Ni kweli kuna uwezekano mkubwa sana kuwa hii ni fiction. Ukisoma comment yangu ndefu kwenye ule uzi wake
Mentor utaona kuwa nilionyesha mashaka yangu kuhusu ukweli wa habari yake. Nilitoa mfano wa Diagnosis iliyokuwa documented kwenye ile form yake haikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na HIV/AIDS.
Hata hivyo, niliendelea kumpa ushauri kwa kumpa benefit of doubt.
Nafikiri nifupishe tu maelezo yangu kuwa kama kweli ile ni story ya kutunga, then amefanya kosa kubwa sana. He is very misinformed. Huyu Jamaa ni miongoni mwa watu ambao nimekuwa nikiwaona wanajitambua hapa JF. Nilimheshimu. Kwa hili, I repeat, kama ni utunzi, then nimemdharau sana. Intelligent people hawafanyi makosa ya kijinga kama hayo. Lakini kama ni mtu muelewa huwezi kutumia HIV/AIDS kama uchochoro wako wa kutokea. Alitakiwa ajue kuwa UKIMWI ni ugonjwa ambao bado global community ina-struggle kuondoa tatizo la unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU. Obviously, ana ufahamu mdogo na hakujishughulisha kufanya homework ili asipotoshe watu.
Mentor atakuwa ni mbaguzi kwa PLHA. Iko obvious na it seems that has subconsciously motivated him kuja na aina ile ya uzi.
If indeed he was playing with people's minds, then anatakiwa aombe msamaha. With his writing, amefanikiwa kuumiza hisia za watu, ikiwa ni pamoja na wale ambao tayari wanaishi na VVU. Kimsingi ni pigo kwenye mapambano ya UKIMWI. It is a disincentive!!
Naweka full stop hapa kwa kuomba kuwa wakuu tuweni makini na tunzi zetu. Tuwe tunafikiria nje ya box. Hata kams wakati mwingine nia zetu ni kufurahisha watu, basi tijitahidi tu tunzi zetu ziwe constructive na sio destructive.
Cheers!!!