Sista, "Kazi ni Kazi" tu sio shida. Mama ataka Polisi waje, kisa mwanae Jobless kununua Benz lake $50,000

dalalitz

JF-Expert Member
Sep 6, 2013
3,332
1,862
Kwa wengine hii ingekuwa furaha, shangwe, nderemo na vifijo.
Kwa mama huyu wa KiNaigeria yeye anaona 'mapichapicha' tu.
.
Huku akibubujikwa na machozi mithili ya mtu aliefikwa na msiba na akihanikiza na kushinikiza Polisi wahusike kuchunguza imekuwaje mwanae ambae ndio kwanza kamaliza masomo ya Sekondari,
Leo hii eti mtoto anatimba nyumbani huku akiendesha Gari mpya bora ingekuwa ya kuazima,
dogo anajimwayamwaya huku akidai kuwa hiyo ni Mali yake yeye na ambayo ameinunua kwa Pesa zake mwenyewe. Gari husika si si Gari tu bora Gari, unaambiwa ni Ni MERCEDES BENZ.
Dingi yeye nae amestaajabu na kukosa cha kuongea.

Niitieni Polisi jamani,
Hapana hapana hapana haiwezekani"
Anaongea kwa hisia za kumaanishaanachokisema na huku akigaragara.

Kumbuka sio Sinema hii.

Unadhani mama yupo sahihi?
 
Attachments

  • -210710507.mp4
    14.4 MB
Kwa wengine hii ingekuwa furaha, shangwe, nderemo na vifijo.
Kwa mama huyu wa KiNaigeria hali hali zote hizo ni hasi kabisa kwa anavyojisikia.
Huku akibubujikwa na machozi mithili ya mtu aliefikwa msiba, akihanikiza na akishinikiza Polisi wahusike kuchunguza imekuwaje mwanae ambae ndio kwanza kamaliza masomo ya Sekondari. Anavyojua mama mvulana wake hajapata hata pa kujishikiza Pesa.
Leo hii eti mtoto anatimba nyumbani huku akiendesha Gari mpya na akidai kuwa ni Mali yake yeye aliyoinunua kwa Pesa zake mwenyewe.
Huku Gari husika si si Gari bora Gari,
Ni MERCEDES BENZ.

"Haiwezekani,
Mama anasema.
Niitieni Polisi jamani, hapana hapana hapana haiwezekani"
Nakugaragara.

Kumbuka sio Sinema hii.

Unadhani mama yupo sahihi?
Uchawi wa Mwafrika ni wa kutiana adabu na kuoneshana umwamba
 
Kwa wengine hii ingekuwa furaha, shangwe, nderemo na vifijo.
Kwa mama huyu wa KiNaigeria yeye anaona 'mapichapicha' tu.
.
Huku akibubujikwa na machozi mithili ya mtu aliefikwa na msiba na akihanikiza na kushinikiza Polisi wahusike kuchunguza imekuwaje mwanae ambae ndio kwanza kamaliza masomo ya Sekondari,
Leo hii eti mtoto anatimba nyumbani huku akiendesha Gari mpya bora ingekuwa ya kuazima,
dogo anajimwayamwaya huku akidai kuwa hiyo ni Mali yake yeye na ambayo ameinunua kwa Pesa zake mwenyewe. Gari husika si si Gari tu bora Gari, unaambiwa ni Ni MERCEDES BENZ.
Dingi yeye nae amestaajabu na kukosa cha kuongea.

Niitieni Polisi jamani,
Hapana hapana hapana haiwezekani"
Anaongea kwa hisia za kumaanishaanachokisema na huku akigaragara.

Kumbuka sio Sinema hii.

Unadhani mama yupo sahihi?
Ingekuwa Tanzania mama angetamba kwa majirani zake, hata hivyo nyumba ya wazazi wake na gari havifanani sijui atakuwa analilaza msikitini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom