Sishauri Forker 50 na Forker 28 ziwe 'Branded' kama Ndege za Kibiashara za ATCL

Sishauri Forker 50 na Forker 28 ziwe 'Branded' kama Ndege za Kibiashara za ATCL

si jakuelewa unamaanisha nini??ni za kizamani sana?au ni kwa sbb marais waliotangulia hawakufanya hivyo au shida kwako ni ipi,je ni bora zikae tu hapo chini zizidi kuharibika au ni bora zipige kazi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi wa kwako mwenye halafu unakosa nguvu ya hoja ya kuutetea unaishia kutukana hovyo kama mtoto mdogo.

Rudi kwenye mada na ujibu hoja za watu sio kujishaua na kuandika ujinga. Rais kasema yeye ndege moja inatosha kwani haendi nje mara kwa mara, hizo nyingine zikabebe abiria ili zizalishe. Wewe unakuja na hoja za kibishi ambazo huwezi kuzitetea.

Unataka nitetee vipi Hoja yangu wakati kila Kitu nimekiandika / nimekielezea katika ' thread content ' yangu #1? Halafu nikikuita / nikiwaiteni ' Wapumbavu ' mliotukuka mnalalamika.
 
Kimsingi mheahimiwa rais kakosea Sana kutoa hiyo kauli. Kwa mfano makamu wake rais je atasafiria Nini?
Kesho akiachia madaraka hizo ndege zinarudi Tena kwa rais Kama second hand?

Sababu ya yeye kutokutumia ndge isimfanye akaonekana Kama joka la mdimu. Ndimu halili na hata mwenzie naye asikule.

Halafu nafikir mheshimiwa Ben MKapa aliposema rais aache kauli za kusema "Mimi, Mimi au serikali yangu, serikal yangu" bado hakumuelewesha vzr mheshimiwa rais.

Kama serikal ninya CCM Basi lazima serikal hii ijue Mali za rais siyo Mali za mtu bali ni za taifa. Any change of use lazima ifwate process na siyo kauli tuu ya mtu mmoja
ulimsikia vizuri rais au unakurupuka kuandika tu,alisema kwa wakati ambao viongozi wa serikali hawazitumii basi zibebe abiria,nongwa kwako ni ipi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada na wote wanaokusapoti mmetumwa na 'mbowe'

(Kwa hisani ya buku 7 FC)

Sent using Jamii Forums mobile app

Nafurahi kusikia leo Mtu ambaye anachukiwa na hapendwi kabisa na wana CHADEMA hapa Jamvini GENTAMYCINE hatimaye anahusishwa nao moja kwa moja. Nilikuwa sijui kumbe GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ni Mwanachama wa CHADEMA? Acheni tu niwe ' nawadharau ' Watu hapa.
 
Tatizo lako hujaelewa kauli ya Rais amesema zipo ndege tatu za rais hivyo kuliko kuwa zimepaki tu ni bora atowe hizo mbili zipakwe rangi na zifanye kazi kuliko kuwa zimepaki.hivyo basi imebaki moja kwaajili ya matumizi ya rais na wasaidizi wake.na ndio sababu alizitolea ufafanuzi na kuzitaja no zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafurahi kusikia leo Mtu ambaye anachukiwa na hapendwi kabisa na wana CHADEMA hapa Jamvini GENTAMYCINE hatimaye anahusishwa nao moja kwa moja. Nilikuwa sijui kumbe GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ni Mwanachama wa CHADEMA? Acheni tu niwe ' nawadharau ' Watu hapa.
Kwani boss umejuaje Mimi kuwa mwanachama was Ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye akili timamu huwa haoni ufahari kugombana na watu, huona fahari kuwa na marafiki wengi. Rudi kwenye mada achana na huu upuuzi uliouanzisha.

This is GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE Mkuu. Nitawateseni sana na nitawanyoosheni mno ' Mapopoma ' wachache kama Wewe.
 
Sio mara ya kwanza ndege za serilali au ndege za raisi kusafirisha abiria wa ATC.Mimi nimeipanda kutokea Mombasa kupitia Zanzibar kuja Dar-es-salaam mwaka wa 2000.
Siku hizi kumeibuka watu kuandika makala ya ndege hususani ATC bila kuwa na upeo wa mambo yanayohusu ndege.
 
Hii ni ' dharau ' kubwa kwa Marais waliopita kuanzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwa Mtu mmoja leo kuamua kwa ' Kukurupuka ' tu kuwa Ndege za Rais Forker 50 na Forker 28 ziwe ' Branded ' kama ' Commercial Planes ' za ATCL.

Hili halipo na halijawahi kutokea nchi yoyote ile duniani na naamini hata tungekuwa Mbinguni Kwake Mwenyezi Mungu hata Yeye pia asingefanya hiki ' Kituko ' ambacho GENTAMYCINE nakiita ni cha Kufungulia mwaka huu ambao bado ni mbichi kabisa wa 2019.

Hoja kwamba zipakwe rangi kisha zichuke Abiria kwakuwa huwa zinakuwa ' grounded ' tu na kwamba hata mwenye Kuhusika nazo huwa hazitumii kwakuwa hasafiri mara kwa mara kutolewa na ' PhD Holder ' kidogo ni kutaka Kuwadhalilisha ' Intellectuals ' wote nchini Tanzania.

Wasaidizi wa Rais hebu fanyeni Kazi zenu vyema Kwake kwa Kumshauri mnaogopa nini? Hivi Sekta ya Anga ya leo au ATCL ya leo inahitaji kweli hadi hata Ndege za Marais nazo ziwe ' branded ' na zijumuishwe kama Ndege za Biashara na Kubeba Abiria? Je kuna hilo hitaji kweli?

Ningeambiwa au ningesikia Hoja kwamba labda Ndege hizo ziuzwe na ibaki moja kisha hizo Hela zitumike Kuimarisha Sekta ya Kilimo au nyinginezo ambazo zinahitaji msaada na ungalizi mkubwa ningemwelewa Mheshimiwa Rais na ningekubaliana nae kwa 100% ila kwa hii Hoja yake ya leo nampinga na naona ni kama vile ' Tusi ' kwa Watangulizi wake.

Wengine tumeumbwa kuwa wakweli na wawazi hivi hivyo mtusamehe tu na tuvumiliane. Tuache Kukurupuka na kuwa na ' Mihemko ' isiyo na Tija wala Mantiki. Halafu akina Donald Trump ' wakitutukana ' Waafrika huwa tunalalamika na kuona labda anatuonea wakati kumbe huwa yuko sahihi tena kwa 100% zote kutokana na ' Madhaifu ' yetu ya asili.

Nimesikitika!

Nawasilisha.
hapa hujatoa hoja yako ya msingi ila umelalamika tuu,kwa kutokubaliana na hoja ya PhD holder ungetoa hoja zako Kwanini hukubaliani naye,una sababu za kiusalama,kijamii,kidiplomasia,kitamaduni au kitaaluma ambazo zinaweza zikaleta athari kwa taifa wazo likitekelezwa????
 
This is GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE Mkuu. Nitawateseni sana na nitawanyoosheni mno ' Mapopoma ' wachache kama Wewe.
Tatizo unajiona Uko perfect wakati Hakuna lolote uliloeleza kuhusu athari za ndege hizo kutumika kibiashara. Umeleta Mada yako kimihemko Sana wakati kwa Mtu anayejiona anaweledi angeeleza madhara ya kuzitumia ndege hizo kibiashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi mheahimiwa rais kakosea Sana kutoa hiyo kauli. Kwa mfano makamu wake rais je atasafiria Nini?
Kesho akiachia madaraka hizo ndege zinarudi Tena kwa rais Kama second hand?

Sababu ya yeye kutokutumia ndge isimfanye akaonekana Kama joka la mdimu. Ndimu halili na hata mwenzie naye asikule.

Halafu nafikir mheshimiwa Ben MKapa aliposema rais aache kauli za kusema "Mimi, Mimi au serikali yangu, serikal yangu" bado hakumuelewesha vzr mheshimiwa rais.

Kama serikal ninya CCM Basi lazima serikal hii ijue Mali za rais siyo Mali za mtu bali ni za taifa. Any change of use lazima ifwate process na siyo kauli tuu ya mtu mmoja
Akili tunduizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nonsense halafu hapo hapo bado tena unamfuatilia huyo huyo mwenye nonsense. Sasa hapa kati yangu na wewe nani ndiyo Rais / Kiongozi wa hiyo ' Nonsense ' yako?
Ninasoma thread yoyote nikijisikia, nikiona nonsense nasema tu umeandika nonsense!

Unasema akili kubwa mdomo huku mdomo hauna break?
 
hapa hujatoa hoja yako ya msingi ila umelalamika tuu,kwa kutokubaliana na hoja ya PhD holder ungetoa hoja zako Kwanini hukubaliani naye,una sababu za kiusalama,kijamii,kidiplomasia,kitamaduni au kitaaluma ambazo zinaweza zikaleta athari kwa taifa wazo likitekelezwa????
Achana naye huyo. Ameleta Mada kimihemko Sana bila kueleza kwanini anapinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom