Elly official
JF-Expert Member
- Sep 16, 2018
- 727
- 976
Mkuu hayo ni mawazo yako, ila wwengine tunamuunga mkono, afadhali zitumike kuwabeba watanzania zifanye biashara nchi ipate pesa kuliko kuzipaki pale airport. Bado kuna ndege moja ya rais. Itatumiaka hiyo kwa safari zakeHii ni ' dharau ' kubwa kwa Marais waliopita kuanzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwa Mtu mmoja leo kuamua kwa ' Kukurupuka ' tu kuwa Ndege za Rais Forker 50 na Forker 28 ziwe ' Branded ' kama ' Commercial Planes ' za ATCL.
Hili halipo na halijawahi kutokea nchi yoyote ile duniani na naamini hata tungekuwa Mbinguni Kwake Mwenyezi Mungu hata Yeye pia asingefanya hiki ' Kituko ' ambacho GENTAMYCINE nakiita ni cha Kufungulia mwaka huu ambao bado ni mbichi kabisa wa 2019.
Hoja kwamba zipakwe rangi kisha zichuke Abiria kwakuwa huwa zinakuwa ' grounded ' tu na kwamba hata mwenye Kuhusika nazo huwa hazitumii kwakuwa hasafiri mara kwa mara kutolewa na ' PhD Holder ' kidogo ni kutaka Kuwadhalilisha ' Intellectuals ' wote nchini Tanzania.
Wasaidizi wa Rais hebu fanyeni Kazi zenu vyema Kwake kwa Kumshauri mnaogopa nini? Hivi Sekta ya Anga ya leo au ATCL ya leo inahitaji kweli hadi hata Ndege za Marais nazo ziwe ' branded ' na zijumuishwe kama Ndege za Biashara na Kubeba Abiria? Je kuna hilo hitaji kweli?
Ningeambiwa au ningesikia Hoja kwamba labda Ndege hizo ziuzwe na ibaki moja kisha hizo Hela zitumike Kuimarisha Sekta ya Kilimo ambayo inahitaji msaada na ungalizi mkubwa ningemwelewa Mheshimiwa Rais na ningekubaliana nae kwa 100% ila kwa hii Hoja yake ya leo nampinga na naona ni kama vile ' Tusi ' kwa Watangulizi wake.
Wengine tumeumbwa kuwa wakweli na wawazi hivi hivyo mtusamehe tu na tuvumiliane. Tuache Kukurupuka na kuwa na ' Mihemko ' isiyo na Tija wala Mantiki. Halafu akina Donald Trump ' wakitutukana ' Waafrika huwa tunalalamika na kuona labda anatuonea wakati kumbe huwa yuko sahihi tena kwa 100% zote kutokana na ' Madhaifu ' yetu ya asili.
Nimesikitika!
Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app