Muone huyu naye! Anatamani kuwa setla!! Yaani unatamani ubwana ili uwe na watwana chini yako. Mtu yeyote aliyejikomboa kifikra hatamani kuwa setla bali anatamani kuwa mshiriki wa maendeleo na si bwana wa kuabudiwa. Achana na usetla. Chagua kilicho bora katika maisha. Jichanganye na raia wenzako, toa mchango wako wa maendeleo, chapa kazi kwa bidii, utayabadili mazingira yako na kuwa mahali pema pa kuishi si wewe tu bali jamii nzima. Huo nidyo utu na heshima. Usetla hauna tija kwani ni ukandamizaji, unyanyasaji, ubaguzi wa kimadaraja (kimapato), ulimbukeni uliojaa majivuno na kujiona.