unachosema mkuu acheche kina ukweli, nakumbuka 2007 nilikuwa najitolea kufundisha shule flani kijijini kwetu, mwenge ukaja kuzindua jengo la bweni la wasichana, nilipewa assignment ya kuandaa ndoo ya mchanga na kuupeleka staff room, baada ya mwenge kufika ulioelekwa ofisini kisha ukazungukwa na wanajeshi, then ulizimwa halafu wakamwaga majivu na(mchanga?) kwenye mfuko, kisha wakaweka tena mchanga kidogo kutoka kwenye ile ndoo kwenye ule mwenge, ukawashwa shuguli za uzinduzi zikaendelea. nilipouliza hakuna aliyenipa jibu zaidi ya kusema kuwa baada ya kuhitimisha mbio za mwenge mchanga ule na majivu yale yaliyokusanywa nchi nzima huwekwa kwenye chombo kimoja na kusemewa vineno hv, then hutupwa baharini, ati ili kudumisha muungano...