Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 23,144
- 26,645
hivi kwenye rasimu ya katiba umezungumziwa?
Nilifundishwa kazi za mwenge ni kulika maadui wetu wakubwa kama ujinga, maradhi na rushwa sasa nashanga vyote vinazidi kukua inamaana mwenge umeshindwa kuvimulika mika yote 51? kama umeshindwa ni bora ukawekwe makumbusho tutauenzi kwa kushindwa kwake kufanya kazi iliyo kusudiwa.Hauna jipya zaidi ya kuabudu mashetani. Kuna taarifa rasmi kuwa Mwenge huo unapofika Rombo-Kilimanjaro hufanyiwa tambiko mbalimbali ili kulinda viongozi wa nchi.
Taarifa zinaonesha kuwa kuna Wazee maalum wameandaliwa kule Rombo kwa ajili ya matambiko haya kila mwaka.Mmoja wa wazee hao aitwaye Mzee Malamsha amenithibitishia hicho.
Kwenye matambiko hayo,kafara hutolewa.Na kadhalika na kadhalika.Ndio maana,kila mwaka Mwenge wa Uhuru lazima ukimbizwe Mkoa wa Kilimanjaro na kufika Wilaya ya Rombo.
Mwenge huu ni wa kuupiga vita. Unaleta laana zaidi ya baraka. Unatubakisha kama nchi kwenye kuabudu mizimu badala ya kusonga mbele kimaendeleo.
Laana za Mwenge huu ndizo zinazotufanya tusieendelee. Ni muda sasa wa kuachana na imani hizi za kishirikina kwa kuachana na Mwenge huu.
Nilifundishwa kazi za mwenge ni kulika maadui wetu wakubwa kama ujinga, maradhi na rushwa sasa nashanga vyote vinazidi kukua inamaana mwenge umeshindwa kuvimulika mika yote 51? kama umeshindwa ni bora ukawekwe makumbusho tutauenzi kwa kushindwa kwake kufanya kazi iliyo kusudiwa.
mimi niliwahi kumuuliza baba nikiwa mdgo ya maana ya mwenge na faida zake,, nikaambulia kofi kali la mdomo na kuniambia unataka tufungwe!! nikashangaa tufungwe??!!!
Mwenge wa UHURU hukimbizwa kila mwaka nchi nzima ukiwa na kauli mbiu mbalimbali, katika mbio hizo mwenge huzindua majengo mbalimbali ya umma kama vile Ofisi, Zahanati na Shule ambapo zaidi ya 95% ya majengo hayo yanakuwa yamejengwa chini ya kiwango. Utasikia ndugu mgeni rasmi ofisi hii imegharimu shilingi milioni 10 wakati ujenzi wake halisi umeghlimu shilingi milioni 2. Hamisi Kagasheki mkoani Kagera aliwahi kuamuru shule iliyofunguliwa na Mwenge ipigwe nyundo yote kabla haijatumika kisa ilikuwa na nyufa za kuweza kupitisha simu ya mkononi.Mwenge wa uhuru una gharama zifuatazo:a)Mafuta ya magari kuzunguka nchi nzima.b)Malipo kwa wanaoukimbiza nchi nzima.c)Magari ya kuzunguka nchi nzima na matengenezo yake ya mara kwa mara.d)Gharama za maandalizi ya kila mahali utakapolala nchi nzima.e)Gharama za walinzi mahali unapolala kila usiku nchi nzima.f) Muda wananchi wanaopoteza kuusubiri na kukesha nao n.kMaswali ninayohitaji wenzangu mnisaidie majibu yaje:a)Mbona kila mwaka mwenge unapozimwa hatujawahi kusomewa mapato ya mbio hizo?b)Tunapata faida gani kutokana na kuukimbiza mwenge kila mwaka?c)Hivi kweli viongozi wa mbio za mwenge wanapozindua majengo yanayotaka kubomoka hawaoni kuwa yako chini ya kiwango?WABUNGE WETU MWENGE HATUUTAKI,,,,,,,,,,,,,. HAUNA TIJA KWETU ..
Wale jamaa zetu siku hizi wanatumia magari aina ya Nissan private No.Huwa wanaichukua hiyo tochi wanaenda nayo chemba kuibadirisha tambi na kuongeza wese,infact mmoja wao ni shemeji yangu alishawahi kuniambaiaga kuwa katika ile tochi kuna siri kubwa sana ya kiuchawi na mizimu iliyoachwa na........ aliniambia kuwa siku tukiupuuza ndiyo itakuwa mwisho wa SISIEMU,
Mimi ndiye bwana mungu wako usiabudu miuungu wengine. Je tochi ile ni sanamu,muzimu,nyoka wa shaba,au Msukule?????????????????????????????????????????????????
Kitu hakiwezi kushindwa ukakienzi mkuu, zaidi zaidi utakidistroy ili usikione klkukumbushe machungu
unachosema mkuu acheche kina ukweli, nakumbuka 2007 nilikuwa najitolea kufundisha shule flani kijijini kwetu, mwenge ukaja kuzindua jengo la bweni la wasichana, nilipewa assignment ya kuandaa ndoo ya mchanga na kuupeleka staff room, baada ya mwenge kufika ulioelekwa ofisini kisha ukazungukwa na wanajeshi, then ulizimwa halafu wakamwaga majivu na(mchanga?) kwenye mfuko, kisha wakaweka tena mchanga kidogo kutoka kwenye ile ndoo kwenye ule mwenge, ukawashwa shuguli za uzinduzi zikaendelea. nilipouliza hakuna aliyenipa jibu zaidi ya kusema kuwa baada ya kuhitimisha mbio za mwenge mchanga ule na majivu yale yaliyokusanywa nchi nzima huwekwa kwenye chombo kimoja na kusemewa vineno hv, then hutupwa baharini, ati ili kudumisha muungano...