augustino ameri
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 267
- 57
Upo gizani,tena ndani ya chupa unahitaji kukombolewa.
Jaribu kuweka thread ya maana kama huna wacha,ila upuuzi huu hakuna atakayeuamini,Rombo wana matamiko gani ya kuweza kuleta laana kwa nchi,siamini kuwa mtu mzima jiamini.
Wenye nguvu zaidi tumeshazivunja hizo nguvu na laana zinazoambatana nazo na sasa tuko huru ndiyo maana unaona down fall ya uongozi wa CCM. So relax subiri kuijenga nchi yako!.......
mimi nashauri mwenge uwekwe jumba la makumbusho sasa. Wakati mwingine ni kuendekeza ujinga. Msafara wa mwenge unaweza kutumia shilingi milioni 200 kwenda kuzindua au kuweka jiwe la msingi la chumba cha darasa ambalo thamani yake ni sh milioni 6 au 7!
Hauna jipya zaidi ya kuabudu mashetani. Kuna taarifa rasmi kuwa Mwenge huo unapofika Rombo-Kilimanjaro hufanyiwa tambiko mablimbali ili kulinda viongozi wa nchi.
Taarifa zinaonesha kuwa kuna Wazee maalum wameandaliwa kule Rombo kwa ajili ya matambiko haya kila mwaka.Mmoja wa wazee hao aitwaye Mzee Malamsha amenithibitishia hicho.
Kwenye matambiko hayo,kafara hutolewa.Na kadhalika na kadhalika.Ndio maana,kila mwaka Mwenge wa Uhuru lazima ukimbizwe Mkoa wa Kilimanjaro na kufika Wilaya ya Rombo.
Mwenge huu ni wa kuupiga vita. Unaleta laana zaidi ya baraka. Unatubakisha kama nchi kwenye kuabudu mizimu badala ya kusonga mbele kimaendeleo.
Laana za Mwenge huu ndizo zinazotufanya tusieendelee. Ni muda sasa wa kuachana na imani hizi za kishirikina kwa kuachana na Mwenge huu.