Siri ya Mahakama ya Kadhi yafichuka

Siri ya Mahakama ya Kadhi yafichuka

mkuu FF,eti ni kweli kuwa mwanamke wa kiislamu akiwa hedhini hatakiwi kuhudumia (kama madaktari,manesi,mahakimu,walimu etc)?

Teh teh teh…! Kweli hii dini ni kituko sijawahi ona kumbe ba hilo limo?
 
Hii si nchi ya waarabu na si nchi ya kuendeshwa kwa imani Fulani.Ya kaizari mpe kaizari na ya Mungu apewe Mungu.Hizi ndio indicator za udini sasa.

Cabinet iliyoongozwa na baba wa taifa katika kutafakari ni jinsi gani ya kuunda taifa la umoja ni ya kuheshimiwa sana hiki kipengele cha kinachosema "serikali haina dini " waliona mbali na nitazidi kumuheshimu maisha yangu yote
 
Hivi kwa sasa kesi za ndoa& Talaka pamoja na Kesi za Mirathi zinasikilizwa na mahakama gani? Na kwa sheria zipi? Hivi wanao zisikiliza kesi hizo wanalipwa na nani?? Na zikiondolewa(kutenganishwa) kutoka ktk mahakama hizo au zikisikilizwa na mtalaamu mwengine ni makosa kulipwa na Serikali??? Hivi sheria zilizopo zina tambua ndoa za aina ngapi???

swali dogo tu je waislam wapo tayari kutumia kodi zinazokusanywa kwenye nguruwe kusimamia hizo mahakama yao ya kadhi?????

ndugu zangu sio kila kitu mnachanganya mambo ya dini.
 
Naam, tupo kwenye jihadi, na ambae hayupo kwenye kufanya juhudi kila siku ya maisha yake huyo ana walakin, iwe Muislam au si Muislam.

Wewe hufanyi juhudi katika maisha yako ya kila siku? na umebweteka tu?

naelewa ni ku struggle or resisting,but often mmeigeuza jihad kuwa al-harb.
 
Mimi nashauri ikiwa mahakama za kadhi zitapitishwa basi kila dini na kila kabila liwe na mahakama zake ziendeshwe kwa gharama za serikali ili kuleta usawa kwa kila mtu. Kule kwetu tunahitaji mahakama za kimila nazo zitambuliwe na kuwezeshwa na serikali.

Hii ni Nchi ya kudai Dai , wakiruhusu Mahakama ya kadhi ujue kila Mtanzania atadai Mahakama ya Kabla lake, Dini yake mpaka Mahakama ya Ukoo.
 
onesha kifungu kilicho hainisha kuwa serikali niyadini ya kikristo

Serikali ya Tz haina Dini , wanaotaka Mahakama ya kadhi ndiyo wanaleta choko choko , kwani kila Dini watazidai Mahakama zao na wapagani watadai Mahakama zao , Waganga wa kienyeji na kila ukoo watadai Mahakama zao.
 
Hapo penye wekundu, una uhakika na unachokisema? Msiwe mnapenda kuwaza na kusema msivovijua? hebu nenda Mtaa wa Bibi Titi pale karibu na shule ya Mnazi Mmoja , angalia kuna mitambo ya Tanesco imejengwa pale! uliza kile kiwanja kilikuwa cha nani? ukipata jibu njoo uhororoje hapa!
mkuu nimeongeza kitu kwenye hii post yako asante sana. nilikuwa sijashituka kama lile eneo opposite na DIT limejengwa mitambo na hao wezi waitwao tanesco.
 
Mbona hospital za Makannisa madaktari wanalipwa mshahara na serkali waislam tumenyamaza kwani siyo kodi zetu pia?

hosipitali za makanisa zinajiendesha zenyewe, vyuo vya kidini vinajiendesha zenyewe, nenda SAUT, Bugando hosipital, KCMC ukaone.
 
Kaka 1000 digits nimekuelewa sana, kama ni CCm ndo wamekuwa wakiwa ahidi na kuwa hadaa waisilamu kwa muda wote huo, basi mahakama ya kadhi iwekwe kwenye katiba ya CCM na si katika ya nchi ya Tanzania, hatuwezi tukakubali kila upumbavu wa CCM ukawagharimu Watanzania wote, CCM na viongozi wake wote waliopita na waliopo wanatakiwa kujibu hili kwa waisilamu. It has nothing to do with Tanzania as a nation.

“You can fool some people some times but you cant fool all the people all the time” Mwaka 2005( kutokana na maelezo yako). Waisilamu walidanganywa na wakakubali kuiweka serikali ya CCM madarakani, mwaka 2010, wakakubali tena wakarudia makosa, na sasa bado tunawaona wengi tu wakiunga mkono CCM iliyo wadanganya na wengi wako teyari kuipigia kura CCM tena mwaka huu.

Kwanini wewe uwaonee huruma watu wasio jionea huruma, watanzania lazima tukubali kuteseka kwaajili ya shingo zetu ngumu kwa kukubali wenyewe kuiweka CCM madarakani mwaka 2010, na kama kunaupumbavu wa maisha na wahistoria ambao watanzanzania wataufanya ni kuirudisha CCM madarakani tena mwaka huu 2015. Itakuwa ni kilio na kusaga meno.



Kinachonikera ni jinsi serikali ya CCM inavyolihandle jambo hili. Serikali haina maamuzi ya ndio au hapana . Awamu ya kwanza palikua na waislam wengi kuliko ilivyo sasa ukilinganisha na wakristo lakini serikali kwa dhamana iliyopewa na nia safi iliyokuwepo iliifuta mahakama ya kadhi na waislam hawakufanya pingamizi kubwa sana kwani waliamini katika umoja na mshikamano .

Leo hii serikali inakumbatia majizi ya mali za umma.Maisha yanakua magumu ndoa kila siku zinavunjika .Awamu ya kwanza ilijenga shule bora na viwanda vya umma ,mashirika ya umma kama ya uchukuzi na biashara za umma ,vyama vya ushirika ,nyumba za serikali ,mashamba ya ujamaa,Chama kimoja cha wafanyakazi. n.k. Ulikua ni mpango mzuri kwa wakati huo.Watu wote wakaungana.Leo hii viongozi wa umma ni mabilionea lakini wanasema sisi ni wamoja.Wemepora na kuchukua mali za umma pamoja na nyumba za umma.
Kwa nini waislam nao wasidai mahakama yao iliyokuwa imechukuliwa kwa umoja uliokuwepo wakati huo na kwa sababu CCM leo imeshagawanya kila kitu na inazidi kugawa mpaka mikoa kulingana na makabila ili tu kada mmoja apewe ukuu wa mkoa na mwingine apewe wilaya.Hao hao CCM ndio wanaowanunua viongozi wa dini ili kuzidi kuwagawa watanzania wasiwe na agenda na misingi ya pamoja .
Umeona Escrow maaskofu wamepewa chao.Leo wanasema hawataki mahakama ya kadhi ,wangekataa kwanza rushwa ya escrow inayodidimiza uchumi mpaka watu wanawaza kujenga mahakama badala ya viwanda vikubwa.Watu hawajui tena tatizo la umaskini wetu na namna ya kupambana nao.Hivi unafikiri Ridhiwani kikwete au Vita Makamba akiwa na shauri la ndoa ataenda kwenye mahakama ya kadhi kuamuliwa?Umaskini ndio tatizo la msingi.
Sasa kwa sababu serikali iliyoko madarakani imeshindwa kuondoa umaskini ni bora itoe mahakama kwa waislam.Watakapoona kwamba hazina tija sana basi watu wataanza kujenga hoja za pamoja za maendeleo.

Haya mambo ukisema waislam wayaanzishe wenyewe ujue una hatarisha amani ya nchi.Mana ni kweli kuwa hawawezi hata kusimamia huo uanzishwaji wake bila kupigana bakora.Sasa kwa nini serikali iangalie suala linaloweza kuigharimu nchi badala ya kuliratibu na kuliwekea taratibu za kufuata?

Haiwezekani tukakubali mahakama ya kadhi isimamiwa na kuendeshwa na mataifa ya nje.Hapa ndipo machafuko yanakoanzia.

Wakristo wa Meru(KKKT) miaka ya 1988-1990+ walichapana sana kwa sababu ya kugombea misaada toka Ulaya halikadhalika Mwanga(KKKT) miaka ya 2000+ na bado hawajakaa vizuri.
Serikali imara inaweza kusimamia kila kitu kwa faida ya watu wake. Cha msingi ni kuimarisha uchumi na kuwatosa wale wanaojifanya kuwa ni mapanya wanaokwamisha maendeleo.

Hili la kadhi CCM itajiju yenyewe kwa kujifanya ndumilakuwili .Kwa maaskofu inataka kura na kwa waislam pia inataka kura za kitapeli. CCM
Ichague moja kufa kwa ajili ya Taifa au taifa life kwa ajili ya CCM.!!Tusubiri tuone mwisho wa tamthilia hii ya CCM na kujipatia kura kwa njia ya udanganyifu.
 
mi ni muslim ila kwa hili suala la mahakama ya kadhi ilipwe na serikali sioni kama ni sahihi.

Wote tunafahamu pesa ya serikali inapotoka ni pamoja na kukusanya kodi za beer, kumbi za statehe na mambo mengine ambayo dini/ Quran hairidhii yaani pesa zake zinatokana na haramu.

Mi nachoona hapa muslims tuache kutafuta manufaa yetu ya kidunia kwa mlango wa dini( uislamu), ambapo tunajua fika kuwa dini inakataa!!

Yaani pesa za beer au pesa za haram zimlipe sheikh kisha sheikh aende kuhukumu kwa kutumia Quran/hadith?! kweli???hebu tufikirie tena jamani isije ikawa tunapalilia dunia na kujichochelea kuni akhera.

Ni hayo tu.

watu wote tungekuwa na upeo kama wako haya mabishano yasingekuwepo
 
Ziendeshwe kwa kodi za kitimoto na pombe?
Inafaa wazianzishe kivyao na kuzihudumia kivyao.
 
Kumbe kuwa na University nyingi sio kuwa na maarifa munazidi kuawa na chuki katika nafsi zenu,uislam uyakuja kusima na kuwa dola,hii ni ahadi ua Allah hilo halina ubishi,ulimwengu lazima urudi katika asili yake

Inamaana Abu bakri al Baghdadi ndo atakuwa Raisi wetu? Mswalie mtume shekhe. Tutachinjwa wote maana wakristo hatutakiwi
 
wananchi inaowatolea huduma ndio waigharamie. Wasiwe waktisto ama wapagani. Nafikiri hapo umeelewa. Sidhani kama zile sharia zitawasaidia napadre, wachungaji na waumini wao wala wapagani na mizimu yao. Over.

miislamu bwana vichwa vikubwa ubongo hamna kitu
 
Kwani hao waislam hawalipi kodi?

Hata kama wanalipa, sawa na madhehebu mengine, iweje sasa kodi ya madhehebu mengine pia itumike kuhudumia kundi moja la jamii? Mahakama zipo tayari ambazo kodi ya kila mwananchi inatumika kuziendesha kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. Hiyo ya Kadhi ni jambo binafsi linaloihusu imani ya kundi moja ndani ya jamii hivyo basi na muliendeshe kidini hivyo hivyo na sadaka zenu, wengine haliwahusu. Haina tofauti na kutumia kodi ya Mtanzania kujenga barabara Kenya! Inaingia akilini hiyo?
 
Ziendeshwe kwa kodi za kitimoto na pombe?
Inafaa wazianzishe kivyao na kuzihudumia kivyao.

Pesa ya kitimoto ndiyo inafaa kuwalipa mishahara Si wanataka walipwe na Serikali ? Wafugwe Kwa wingi Kwa Ajili ya kuchangia bajeti ya mishahara yao.
 
Hata kama wanalipa, sawa na madhehebu mengine, iweje sasa kodi ya madhehebu mengine pia itumike kuhudumia kundi moja la jamii? Mahakama zipo tayari ambazo kodi ya kila mwananchi inatumika kuziendesha kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. Hiyo ya Kadhi ni jambo binafsi linaloihusu imani ya kundi moja ndani ya jamii hivyo basi na muliendeshe kidini hivyo hivyo na sadaka zenu, wengine haliwahusu. Haina tofauti na kutumia kodi ya Mtanzania kujenga barabara Kenya! Inaingia akilini hiyo?
Ngoja Kodi za sigara, Pombe na kitimoto zitawalipa mishahara , wao wameng'ang'ania Upande wao pasipo kufikiria pesa za kuwalipa zinatokana na nini .
 
Hivi nyinyi wagalatia nani ka wadanganya kua yake majengo ya muslim univasity mkapa kayatoa bure

Amini nawaambia ukweli wa jambo hili ni serikali ya irani na serikali hii ndio wanatambuaa

Mkiaambia hayo majengo ililipa madeni
 
Back
Top Bottom