Siku za ajabu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2012
- 1,369
- 988
Mungu yupo maombi ndio silaha pekee ya ushindi
Maelezo marefu ila UJINGA tuu ulioandika!
Serikali haina dini vp mbona wasile kiapo kimya kimya wakiteuliwa kwenye nyadhifa mpya? Hujui hata kuwa UPAGANI nao ni Dini?
Chuki za namna hii ndizo pia zilizotumika hata katika tukio la kupigwa Lipumba juzi,mtu anaongea jambo ambalo halina mantiki ila kwa kusukumwa na chuki tu dhidi ya waislam na uislam kwa Ujumla
Utangulizi:
Kwa muda mrefu sasa, wenzetu katika imani wamekuwa wakiishinikiza Serikali iweke katika Katiba ya Tanzania kipengele chenye kuitambua rasmi Kadhi Courts (Mahakama ya Kadhi). Hata hivyo LENGO la uwepo wa Mahakama hizi za Kadhi kwenye Katiba siyo kutambulika kisheria kama wanavyodai, bali ni ili Umma wa Watanzania (wenye dini na wasio nazo) ubebe gharama ya kuziendesha (Operation costs).
Baada ya utangulizi huu, tunaomba kurudi kwenye mada kuu Siri ya Mahakama Ya Kadhi Yafichuka ili ijulikane kuwa Mungu pekee ndiye mwenye siri, na si wanadamu.
Siri ya Mahakama ya Kadhi:
1. Kwamba, baada ya kelele za muda mrefu za Waislamu kudai kuwa Serikali inawaonea, na haiwapi fursa za elimu kwa usawa, Serikali ya Awamu ya tatu (Benjamin Mkapa), aliwapatia bure majengo ya kilichokuwa Chuo cha Tanesco Morogoro, ambapo Waislamu walikifanya kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu Tanzania.
2. Kwamba kwa sasa wahitimu wengi wa Chuo Kikuu hiki wapo mitaani bila ajira (hasa waliosomea Elimu Ahera), na mlango pekee wa kuwapatia ajira serikalini ni kwa kuanzisha MAHAKAMA ZA KADHI, na ambapo kila Kata, Tarafa, Wilaya na Mkoa maelfu ya hawa wenzetu katika imani wataajiriwa.
3. Kwamba utafika wakati ambapo wenzetu katika imani wataamua, ama kupeleka mashauri yao ya ndoa/mirathi kwenye Mahakama za Serikali (ambazo wataziita ni Mahakama za Makafri) au kwenye Mahakama za Kadhi.
4. Kwamba popote pale penye Mahakama ya Mwanzo (kwenye Kata, Tarafa au Mahakama za Wilaya na Mikoa Tanzania), LAZIMA Kadhi awepo pia. Hii inamaanisha kuwa, hata kama Kijiji/Kata au Tarafa haina muislamu hata mmoja (na jambo hali hii lipo maeneo mengi Tanzania Bara), lakini almradi ipo Mahakama ya Serikali mahali hapo lazima Kadhi ataajiriwa kukaa mahali hapo kwa gharama ya serikali, kwa nchi ya TANZANIA ISIYO NA DINI.
5. Kwamba Gharama za Kadhi kwenye haya maeneo (mishahara na marupurupu mengineyo) ni za Serikali ya Tanzania. Maana yake, Serikali itakusanya Kodi za Waislamu, Wakristo na Wasio na dini ili kulipa mishahara ya Makadhi wa Dini moja tu (Islam) kwa sababu inatambuliwa na Katiba ya Tanzania.
HITIMISHO:
1. Kwa sasa Hayupo Mtanzania mwenye imani na wanaoitwa MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, kwa kuzingatia historia yao, na jinsi wanavyopotosha umma kwa minajili ya kuwafurahisha wakubwa zao waliowateua. Kawaida ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kuuwasha moto, lakini ukeshakolea hukaa pembeni kwa kisingizio kuwa Ushauri wangu haukueleweka vizuri.
Ndiyo maana Tunamtahadharisha Ndugu George Masajo (Mwanasheria wa Serikali wa sasa) asiwashe moto wa kuliteketeza taifa la Tanzania na ambao siyo rahisi kuja kuzimika hata baada ya kizazi cha nne kijacho pale machafuko ya UDINI kila kona yakishaanza Tanzania.
2. Rais Mh. Dr. Jakaya Kikwete, kilinde kiapo chako kwa Katiba kwa sababu yatosha sasa kuona unaendelea kuisigina Katiba iliyoweka Tanzania isiyo na dini kuwa taifa la mfano kwa umoja, uhuru, amani na utulivu hapa Afrika. Yatosha kuona mauaji ya maaskofu, mapdri, wachungaji na mashekhe kumwagiwa tindikali.
3. Tunawashauri Wabunge, waachane kabisa na mtego wa CCM wa kujipatia kura kwa gharama ya damu za Watanzania. Ni mtego kwa Wabunge wanaotaka kudumisha madaraka yao kwa kura za Waislamu mwaka huu 2015, hao ndio watajipendekeza kuunga mkono mswada huu wa hatari.
Tanzania ni zaidi ya madaraka / au cheo cha Rais/Mbunge au Mwanasheria Mkuu. Tanzania si jalala la kufanyia majaribiio ya mfumo ambao utatugawa mapande mawili. Wapo watu wanashabikia jambo hili kwa kuwa watafaidika kwa hizi ajira za mfumo wa Mahakama ya Kadhi.
Wapo wanaotolea mifano ya Uganda au Kenya lakini wanasahau hizi ni nchi zinakuja kujifunza kwetu namna ya kujenga umoja wa kitaifa. Waziri Mkuu (Mh. Mizengo Pinda) hata kwa ziara yake Uarabuni, hajaweza kubainisha kama ipo nchi aliyotembelea mwaka jana 2014 yenye mfano wa amani, mshikamano, usawa wa kijinsia kama Tanzania pamoja na kuwepo kwa Mahakama za Kadhi lukuki huko Uarabuni.
Tujikumbushe: Ombi la Kwanza la kupatiwa Chuo Kikuu cha Kiislamu lilifanikiwa (Awamu ya 3), Ombi la Pili la Mahakama ya Kadhi kwenye Katiba (Awamu ya 4), na hatujui Ombi la Tatu la Sharia za Kiislamu kwenye Katiba litamuangukia rais wa Awamu ipi.
Uzoefu ni kuwa Ombi moja la Waislamu huzaa ombi linalofuata kwa mtiririko wake.
Mwisho, Tunaungana na nia njema ya Jukwaa la Wakristo na Wadau wengine, wanaopendekeza Mahakama za Kadhi endapo zikianzishwa kikatiba zijiendeshe 100% kwa gharama ya Waislamu wenyewe. Mungu Ibariki Tanzania iendelee kuwa nchi isiyoegemea Dini au Sera za Udini.
proisra
Umeandika meeengi kama huna ubongo vile. Sema mahakama ya kadhi ianzishwe ila ijigharamie yenyewe ingetosha. Ila ni kwanini ijigharamie yenyewe na inatoa huduma kwa wananchi? Ushani tibua na akili yako ndogo.
Wakatoliki ,waluteri na waangilikana kwa hili la kupinga mahakama ya kadhi hawajafikiria sawa sawa.
Ni wajibu wa serikali kusimamia vyombo vya kutoa haki ikiwa ni pamoja na mahakama ya kadhi.
Serikali ikiiianzisha mahakama hii itakua na uwezo wa kizisimamia vizuri na kuepusha migongano na vurugu miongoni mwa waislam.Na ikumbukwe kuwa waislam wakigombana wenyewe kwa wenyewe hasira zao hufika kwenye kuchoma makanisa kwa sababu kuna kundi kitatuhumu kundi lingine kuwa linatumiwa na kanisa.
Na pia hao wakristo wanaoonea huruma pesa za serikali wakumbuke kuwa kikinuka gharama za kununua mabomu na risasi ni kubwa kuliko kutoa ajira kwa waislam wenye ilm ya sharia ili watoe hukm kwa waislam wenzao kwa mambo ya kijamii.
Tena itakua ni vizuri sana kupunguza malalamiko ya kudhulumiana na rushwa za mahakama hizi za serikali zilizojaa uonevu na sheria zisizozingatia mahitaji ya kiislam katika ndoa zao.
Naunga mkono mahakama ya kadhi kwa asilimia mia moja.
CCM imelikoroga .Ni lazima ilinywe . Waislam wanadai mahakama walitoahidiwa na serikali ya CCM inayoungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wakatoliki ,waangilikana na waluteri ;hasa viongozi wa makanisa haya. Kwa hiyo haya makanisa kupita chama chao cha Christian Councel Motion (CCM) kiliwaahidi waislam mwaka 2010 kuwa kitawapatia mahakama ya kadhi. Sasa nashangaa hao watu ndani ya CCM wanaojenga chuki za kuikataa mahakama ya kadhi.Tena kwa hoja hafifu za gharama za uendeshaji.
Na waislam nao wamezidi unafiki mabilioni ya pesa yanaliwa na mafisadi tangu awamu ya Mwinyi lakini hawajawahi hata kukemea kuhusu ufisadi unaofanya na hii serikali chonganishi.Haya mabilioni kama yangetumika vizuri yangeweza kugharamikia mahakama ya kadhi. Badala yake unamkuta mwanaharakati wa kiislam anatokwa na mapovu akisimulia memorundam of understanding(waraka wa maridhiano) tena unaohusu nchi wafadhili waliogoma kupitisha misaada yao serikalini kutokana na wizi,hivyo wakasema watakua wanasaidia makanisa yenye miradi ya huduma za kijamii.MOU haihusiani na kodi za watanzania ni sawa na MOU ya Tanzania na Kuweit ya kujenga visima na Misikit maeneo yenye waislam ni maridhiano tu na hawalazimishwi na mtu yeyote na haina athari kwa mtu yeyote.
Mahakama ya kadhi kwangu mimi naona yanafaida kwa wale watakaopata ajira lakini kwa yule atakayekuwa ni mpiga debe maskini asiye na hata kibanda cha bata hataona mabadiliko yoyote ya kiuchumi.
Tuwaache wanaotaka mahakama ya kupeana talaka na kugawana mali wapewe tu.
Wakristo jitafutieni miradi mingine ya kimaendeleo nayo ilipiwe na serikali ili ndoa ziimarike kwani umaskini ndio chanzo cha talaka na migogoro ya ndoa.
Cha msingi ni serikali kuanza kutoa ruzuku zilizo sawa kwa taasisi za dini ili wanaotaka mahakama iwe sawa na wanaotaka kuanzisha SACOSS iwe sawa.
Hakuna haja ya kugombana na waislam kwa sababu ya mahakama ya kadhi kwa kisingizio cha gharama.
:llama:Hahaha! heri sisi tusiyo na dini, nyinyi muna MOU "so" munakula bata, wenzenu wanadai angalau mahakama ya kadhi wale miguu munawazuia. hahaha
Wewe nawe akili zake tupu kabisa, yaani kwamaana wakigombana wanachoma makanisa ndo waogopwe wapewe mahakama yao?
Kwahiyo wapewe mahakama ya kadhi kwamaana kuna vijana wao wengi walo soma sheria wapo mtaani unaogopa wataleta vurugu? Kwani hakuna vijana wengine wasio wa imani hiyo waliosoma sheria nao wapo mtaani?
Kwahiyo wapewe mahakama ya kadhi kwamaana mahakama za serikali zina dhuluma na rushwa, kwani kwenye hizo mahakama za serikali hakuna watendaji waimani yao?
1000 digits sikudhani kuwa una akili fupi kiasi hiki.
mbona mkataba wa MOU unawapa fursa wakristo kupewa pesa kuchangia maendeleo yao kama AFYA ,ELIMU KUKOPESHANA kushamiri kwa makanisa hata kama sehemu hakuna wakiristo.pesa za MOU mnazopewa kodi mnalipa peke yenu?
je nwasiokuwa na dini itakuwaje maana nao watataka ruzuku ya mmizimu yao