Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Ndio amekana sasa. Au unabishana na zitto.
Mbona mnakua kama hamjui kusoma, amekana kukutana na Ben na wala hakufika kwenye hicho kikao na wala haijui hiyo hotel. Amekana nini kingine?
 
Vijana ndani ya Chadema hasa mlioko kwenye uongozi na wale watakaogombea na kupata nyadhifa ndani ya chama nyie ndo mtakaokamata usukani baada ya hao waliopo muda wao kwisha. Tujihadhari na siasa chafu ndani ya chama.
 
Nimependa saana hii... Maana hapa karibuni ilikuwa kila anaye weza anasema ajualo na aaminilo bila kujalisha ni kitu gani na kimetoka wapi. That is to say Zitto alikuwa na wasemaji hadi baaas! Bora umekuja na umeonyesha wazi msimamo wako!

Chadema ilipo sasa inahitaji kujipangua palipo jipanga ovyo kwa kujipanga vilivyo maeneo panguliwa. Na hiyo inawezekana tu pale Viongozi wa juu wapo karibu kwa mshikamano na niya thabiti ya kujenga chama na kuacha ubinafsi pembeni.

Kwa hili nakupongeza sana Mkuu Zitto, habari za Dr. Slaa kutaka kukupa sumu via Ben zipo too low na kutamka kwako inaonyesha wazi kuwa kuna watu ambao furaha yao ni kutokuwepo na maelewano mazuri kati yako na Viongozi wenzako hasa wa juu.

Nimependa pia suala la kuonyesha msimamo wako juu ya wale ambao wametoka Chadema! Inawezekana wanakukubali genuinely but it is high time washikamane na vyama vyao na waache kabisa masuala ya Chadema na viongozi wake kwani haviwahusu tena.

Hongera sana.
 
Mbona mnakua kama hamjui kusoma, amekana kukutana na Ben na wala hakufika kwenye hicho kikao na wala haijui hiyo hotel. Amekana nini kingine?
Sibishani na mtu asiyejua maana ya heading. Heading ndiyo inamaliza yale yoote yanayofuata baada yake. Na heading ya hii thread imeshasema kwamba huo ni uwongo. Wewe unataka kulazimisha nini sasa.
 
Hizo tuhuma zilianzia humu kabla ya kufika huko kwenye magazeti. So na majibu yake si vibaya yakafuata mtiririko ule ule. BTW, JF ni free forum ambayo mtu yeyote anaweza kuposti kitu chochote ili mradi asivunje sheria, kanuni na taratibu za forum.

Na kuna thread ya kuhusu CCM kumuandalia tamko kiongozi mmoja wa upinzani ili kukipaka matope CHADEMA, jana imewekwa humu ndani Press Release ya MTIKILA yani ni balaaa, ilikuwa ikihusu kifo cha Wangwe.Mods naona wameifutilia mbali ile press release.
 
Ukiona mtu anaacha taaluma yake na kuanza kuandika uzushi na vitu visivyo na kichwa wala miguu ujue kuna walakini katika akili yake!Nashukuru kamanda Zitto umeliona hilo na kulisemea maana bila kufanya hivi hawa wanaweza kuja na mambo mengine makubwa zaidi ya kuchafua watu.
 
Asante Mkuu.

Naomba kama unaamini uliyoyasema humu usiishie hapo.Kuna haja ya kulitaka Gazeti la Mtanzania kukanusha habari hizi kwenye Ukurasa ule ule waliotumia kuandika.Uzushi wa namna hii kwenye jamii iliyojaa matatizo, watu wasiofikiri sawa tayari wamehitimisha na kuamini kilichoandikwa ndiyo ukweli wenyewe.Lakini haitoshi hata wale wanaozusha uongo huu kwa sasa wanatumia Gazeti hilo kama ndiyo ukweli wenyewe.

Naomba sana kwa faida ya ukweli na kuitendea Chama chako haki chukua hatua.
 
Zitto karudia tena Hajawahi kukutana na Ben so Ben ajitokeze athibitishe kuwa Zitto ni muongo walishawahi kukutana kupanga mikakati ya kuvuruga chama!
 

:rockon:Kiongozi ye yote shupavu anatakiwa kuwa muwazi kama ZZK. Haijalishi ni kiongozi wa Serikali, siasa, shirika, shule au hata familia. Ukweli na uwazi hupunguza wasiwasi na huondoa malumbano. Pokea hongera zangu ZZK.
:rockon:
 
Kwani alikuwepo wakati hizo mbinu zinapangwa, wewe vipi? Hii siri imetolewa na walio mkamata muuaji, hakuweza kutekeleza maagizo yake kwahiyo alie lengwa atajua vipi?

Sasa basi uyo mliyempa iyo siri amegundua siri yenu ni fake mmeitunga ili kugawa wanachama so amekana uzushi huo, nawashauri rudini studio mkatengeneze you tube nyingine.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Na kuna thread ya kuhusu CCM kumuandalia tamko kiongozi mmoja wa upinzani ili kukipaka matope CHADEMA, jana imewekwa humu ndani Press Release ya MTIKILA yani ni balaaa, ilikuwa ikihusu kifo cha Wangwe.Mods naona wameifutilia mbali ile press release.
Huyo Mtikila naye hajakoma alivyopopolewa mawe kule tarime kwa ajili ya upuuzi wake huo huo. Damu chapa chapa.
 
Kwa hii kauli Muheshimiwa Zitto umeifanya Pasaka yangu kua njema!
 
"makosa ya mtu mmoja yasifanywe ya taasisi" mtu gani huyo? Zitto
 
Last edited by a moderator:
A very Big Shame kwa Gazeti la Mtanzania , naahidi rasmi kwamba kuanzia leo sitalinunua , sitalisoma na wala sitakubali kupokea chapati zilizofungwa kwa gazeti hilo , naahidi kishawishi watu wa familia yangu na marafiki zangu kutolisoma Mtanzania , ujumbe huu wa Zito umfikie pia the so called Majebere ambaye bado anaamini ( kupitia maandiko yake kadhaa ) kwamba Saa Nane anahusika .
 
Zitto karudia tena Hajawahi kukutana na Ben so Ben ajitokeze athibitishe kuwa Zitto ni muongo walishawahi kukutana kupanga mikakati ya kuvuruga chama!
Hiyo ni mada nyingine. Ifungulie thread yake na tutakuja huko kuijadili. Thread hii inahusu kanusho la zitto kuhusu mipango ya kutaka kuuawa kwa sumu.
 
Safi jibu murua
Muda muafaka chapeni kazi kujenga taasisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…