Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

ben saanane anatumwa sana kuitafuta roho ya zitto lakini daima zitto hajaonyesha chuki naye, ndio utofauti mkubwa wa akili ya zitto na ben, kwamba ben ni mpika majungu wakati zitto ni mjenga chama

Nimependa sana jinsi ambavyo umeweza kuitolea ufafanuzi wa kina kwani sasa hivi tutashuhudia mizengwe mingi ikipikwa kwa kila aina ya jiko.
Hongera sana ZK.

Huyu Ben Saanane ni Mzigo kwa chadema. Hana heshima wala adabu kwa kiongozi wa chama chake. Na kauli chafu zisizovumilika.

Kwa nini chadema hamumchukulii hatua za kinidhamu? Mbona mnamuendekeze?

Kiongozi asiyejiheshimu anayeamini katika mitandao hapaswi kuheshimiwa na yeyote

vitu vingine vinatia kichefuchefu,ndiyo maana wanasema siasa ni mcchezo mchafu.ninavyomfahamu dr slaa is a highly reputable person.kwanza amelelewa ktk utumishi wa Mungu na siyo zito kabwe.sikubaliani na kauli za zitto ninachojua zito ni mpenda sifa na anataka kujipatia sifa kupitia mgongo wa dr slaa.siamini slaa anweza kupoteza muda wake au kujiingiza ktk tukio kama hilo.mimi ninachokiona ni jinsi zitto anavyotaka kuwaaminisha watanzania kwamba yeye ni mtu maarufu sana hapa tanzania.anajisumbua hii siyo tanzania ya jana labda kama ana agenda yake nyingine aiweke hadhalani.dr slaa ni mcha mungu na ni mwadilifu na siyo zito.dr slaa ameongoza balaza la maaskofu watu ambao ni highly acceptable in a society.taasisi ambayo ni ya kidini na yenye maadili ya hali ya juu.hana shida ya madaraka,ni mzalendo ambaye anachukia na kuyakemea maovu halafu leo hii eti amwue zito for what reasons,for whose benefits.zito ni mtoto mdogo ukilinganisha na dr slaa na ana international exposure hata huwezi kuwaweka ktk mizani moja na zito.nadhani kama ni matamshi ya zito mwenyewe atakuwa amekengeuka na kama propaganda za vyombo vya habari nadhani vyombo hivyo vikafungiwa sababu vinachochea amani ya nchi ambayo Hayati Mwl Nyerere aliijenga kwa gharama kubwa.

Dr SILAA NI MCHA MUNGU!!??? mcha mungu gan anazaa nje ya ndoa? Mcha mungu gani anaiba wake za watu???????????? Kutumia neno mcha mungu ni sawa na kumpka mafuta kwa mgongo wa chupa,,,mimi kwangu namwita MSALITI MUNGU.

ben saanane anatumwa sana kuitafuta roho ya zitto lakini daima zitto hajaonyesha chuki naye, ndio utofauti mkubwa wa akili ya zitto na ben, kwamba ben ni mpika majungu wakati zitto ni mjenga chama
Huwezi kupaka rangi mafuta Zitto ameumbuka,anabomoa chama bila Ben ungekuta anaendeleza libeneke la kuchafua chama ,Zitto yamemushuka hamtamsafisha kwa kumsakama Ben embu fanyeni kazi zingine za ujenzi wa taifa

Dr SILAA NI MCHA MUNGU!!??? mcha mungu gan anazaa nje ya ndoa? Mcha mungu gani anaiba wake za watu???????????? Kutumia neno mcha mungu ni sawa na kumpka mafuta kwa mgongo wa chupa,,,mimi kwangu namwita MSALITI MUNGU.

Dr SILAA NI MCHA MUNGU!!??? mcha mungu gan anazaa nje ya ndoa? Mcha mungu gani anaiba wake za watu???????????? Kutumia neno mcha mungu ni sawa na kumpka mafuta kwa mgongo wa chupa,,,mimi kwangu namwita MSALITI MUNGU.
Ewe mwanadamu imeamuliwa usihesabu makaosa ya mwingine maana nafsi yako yaweza kuwa imekengeuka katika dimbwi la dhambi jililie mwenyewe uokolowe na usihukumu kabla wewe hujahukumiwa ,sara zake ndizo zimefanya wabaya wake wawe wanajikanyagakanyaga tuu

Siku zote nimekuwa sikukubali (kwa kiasi ambacho baadhi ya watu wanakukubali) kwasababu ya kukaa kimya na kutokanusha propaganda za namna hii zilizowahi kutolewa siku za nyuma (kwa mfano udini, ukabila na ukanda) ndani ya CHADEMA...Kwa upande wangu, kukaa kwako kimya ilikuwa inaashiria unakubaliana na uzushi na uzandiki unaoenezwa.Imefikia kipindi sasa kutokana na Nafasi yako ndani ya chama, Dini yako na Kanda yako uwe unakanusha hadharani propaganda za namna hii kwa maslahi yako na chama kwa ujumla.Kwa kufanya hivi utaendelea kutushawishi watu tuliokuwa tumepoteza imani na wewe kama Mpambanaji na Mwana-CHADEMA wa kweli.HONGERA SANA komredi ZITO.

Pole sana masalia... nadhani wewe ndio utakuwa na mzigo kichwani mwako Chadema ipo imara na Ben yupo makini. pole gamba kwa kujiuliza maswali...
Mimi nadhani bila ben sasa hivi ungekuta mambo cdm yamevurugika kabisaaa..nadhani ben ndo katibua mipango yote yao ya kuibomoa cdm ndo maana unaona sasa hivi watu wanahaha ovyoovyo..wanatafuta pa kukimbilia,wanageukana..nadhani ukweli utabaki pale pale kwamba ben is the hero>

Well done Zitto you have made my day salamu kwa wanafiki na wazindiki long live zitto dumu chadema

Ungekua principled ungetaja makosa yangu badala ya kutanguliza emotions.

By the way,nipo busy kushughulikia maswala ya kisheria na kila aliye-play part ni lazima atajutia na kuzilipia hila hizi.Sipendi mambo ya kijinga jinga

Chonde chonde, visihusike vitu vyenye ncha kali au vyenye asili ya ungaunga!

Mimi nadhani bila ben sasa hivi ungekuta mambo cdm yamevurugika kabisaaa..nadhani ben ndo katibua mipango yote yao ya kuibomoa cdm ndo maana unaona sasa hivi watu wanahaha ovyoovyo..wanatafuta pa kukimbilia,wanageukana..nadhani ukweli utabaki pale pale kwamba ben is the hero>

Mkuu berenya, huo ndio Ukweli na daima katika "Ukweli" uongo hujitenga, nadhani kamanda Ben Saanane, ataendelea kuwa Hero. na Mungu azidi kumlinda.

Last edited by a moderator:
SIKU moja baada ya gazeti la Mtanzania kuandika habari likidai kuwa siri ya kumuua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) imefichuka, kiongozi huyo amejitokeza akisema ni uzushi.

Habari hiyo ilidai kuwa ilipangwa Zitto anyweshwe sumu hotelini na kumtaja Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa kuwa ndiye alimtuma kijana Ben Saanane kutimiza mkakati huo.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa kisiasa walisema habari hiyo inayodai tukio hilo lilitokea Mei mwaka jana jijini Dar es Salaam, ilikuwa ni propaganda ya kuhamisha mjadala wa sakata la kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Absalom Kibanda.

Kibanda alitendewa unyama huo Machi 6 mwaka huu, lakini hadi leo vyombo vya dola vimeshindwa kuwakamata wahusika na badala yake yamekuwa yakiibuliwa matukio mbalimbali ili kupoteza ajenda hiyo inayoonesha udhaifu wa kiutendaji wa vyombo hivyo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Zitto alisema habari hiyo imemletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wake wamejawa na wasiwasi kwamba anaweza kuuawa.

"Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi," alisema.

Alifafanua kuwa haijawahi kutokea yeye kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika.

"Pili, siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu (Dk. Slaa) anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti.

"Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuawa na mtu mwingine ndiyo itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndiyo maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuawa. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndiyo furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili, lakini mawazo, fikra na maono yake yataishi tu," alisema.

Aliongeza kuwa haogopi kufa maana maisha aliyoyachagua ndiyo haya ambayo yamejaa vitisho, kwamba muhimu kwake ni kufanya kazi zake kwa bidii, uhodari na uaminifu.

"Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena.

"Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA, maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa," alionya Zitto.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara), alisema chama hicho si pango la watesaji wala wauaji, kwamba kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki.

"Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi. Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama," alisema.

Saanane ang'aka
Naye Saanane aliyedaiwa na gezeti hilo kuwa ndiye alikuwa ametumwa kumdhuru Zitto, alisema amesikitishwa jinsi lilivyoshiriki katika dhamira nzima ya kumchafua.

Akizungumza katika ofisi za Tanzania Daima jana, Saanane ambaye ni mjumbe wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) alisema kutokana na habari hiyo ameamua kukutana na wanasheria wake kuangalia hatua za kuchukua ili ukweli ubainike.

"Nasisitiza sijawahi kupanga kumuua mtu yeyote, sijawahi kutumwa kumuua Zitto Kabwe. Nimesikitishwa kuona chombo cha habari kikitumika kwa maslahi binafsi ya kuchafua watu kisiasa," alisema.

Aliongeza kuwa mara zote alizokutana na Zitto, hawajawahi kufika katika Hoteli ya Lunch Time wakiwa pamoja kama ilivyoelezwa katika gazeti hilo.

Bashe anena
Alipoulizwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd wachapishaji wa gazeti hilo, Hussein Bashe juu ya tetesi za kutumiwa kuyeyusha sakata la kuteswa kwa Kibanda kwenye vyombo vya habari, alisema hawawezi kutumiwa na taasisi yoyote kuzima suala hilo.

"Hilo la namna habari ilivyotoka mimi si mwandishi wa habari, ninachoweza kukuambia ni kwamba magazeti ya New Habari hayawezi kutumiwa na mtu yeyote kuzima au kufifisha suala la Kibanda," alisisitiza.

Alisema kama kuna watu wanafanya siasa rahisi za kuyahusisha magazeti yao na mkakati wa kuzima suala la Kibanda watakuwa wamekosea kwa kile alichoeleza hawezi kuruhusu hali hiyo.

Alipoulizwa atachukua hatua gani kwa mhariri endapo itabainika gazeti hilo kutumika kwa lengo la kuwatoa watu katika kujadili madhila yaliyompata Kibanda, alisema hayo ni masuala ya ndani ambayo hayawezi kuwekwa hadharani pasipo kufuata taratibu.

Habari kutoka Tanzania Daima.

ANGALIZO:
Kuna kauli ambazo zinaonyesha wazi wazi kupingana kati ya Mh. Zitto na Ben Saanane huku Mh. Zitto akidai hajawahi kukutana na Ben Saanane huku Ben Saanane aking'aka kuwa wamekutana zaidi ya mara MOJA.

Kwa mtazamo huu, ni lazima mmojawapo anaudanganya umma kwa kauli zake na kwa mantiki hii, kuna kitu ambacho kitakuwa nyuma ya kauli hizi kinzani.

Sifa ya kiongozi ni kuwa na hekima, busara na kusimama kwenye ukweli, kwa kutokusimama kwenye ukweli, ni nini tujifunze kutoka kwa viongozi wa CHADEMA.

Huyu Ben Saa8 ni mtu hatari sana.

Ndio yule mastermind mpango wa masalia lengo kumuingiza King Zitto , Zitto ashukuru sana hakuwahi kukaa na huyu jama a meza moja. Maana angeweza hata kupiga picha akatumia kama ushahidi wa Zitto kuwa na masalia , hata kama kingekuwa kikao cha harusi.

Back
Top Bottom