Siri kwa wanawake wasaka ndoa miaka nenda rudi

Siri kwa wanawake wasaka ndoa miaka nenda rudi

Ndoa haisakwi, inakuja tu kwa muda muafaka kama besideis.

Ingekuwa inasakwa, lazima kungekuwa na makampuni ya kusaidia watu kusaka ndoa.

never change ur character(temporary) for the sake of ndoa....u pretend to be somebody else ili uingie ndoani,then after few years of marriage unachoka kupretend and ur true colors are starting to show....unaanza kumuumiza mtoto wa watu..no wonder thread za #mke /mume wangu kabadilika siku hizi haziishi#.CHANGE FOR UR BETTER SELF AND NOT BECAUSE U WANT A RING ON UR FINGER.
 
Hizi ndo marks (majibu) ya kupata ndoa mapema..........hii inawahusu hadi wale walio kwenye uchumba chronic/sugu
Hamna haja ya kunywa mchina uongeze makalio,wala kuenda kwa sangoma upate ndoa ndani ya siku 3 ,ukiona miaka mvua za masika zinakukatikia hujaitwa Mrs somebody habari

Hii hapa > Mambo ambayo mwanaume anafanya kukutest kama wewe msichana unafaa kuwa mke wake:
1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa.
2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakutest aone kama utasema "Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu".

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia "Baby twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia". Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!!

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!!

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio tule wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana.

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.
9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi.

11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia. Marks hizo.

Shukrani za dhati zimfikie mtungaji wa article hii ndg Masanja Mkandamizaji nawasilisha tujadili

Mwenye macho haambiwi tazama. On their marks.......
 
Wanawake mnastress,kazi utafute kwa shida na ndoa nayo ikusumbue kha!na hta km utapata hyo ndoa una gerentiiiii ya kuishi kwa furaha,majanga!

Ha ha ha mimi sijasema hivyo au ndo ile amri ya waraishi kwa jasho?au Mwenyezi ataweka uadui wa milele kati ya mwanaume na mwanamke?
 
Hahahaa..... Shindwa kwa jina lako, sifanyi majukumu ya ndoa kabla ya ndoa. Naungana na wengi wasemao kuwa hiko sio kipimo.

Kuna wanaofanya hayo yote kwa ajili ya ndoa ila akifika ndani ndo utaona kila rangi.

Cha muhimu ni Upendo kqa kweli baaaaasssss!!!!!
Hadi mimi niko team #mapenziyakweli lakini ndo nayapenda hayo ili ni propose ring
 
Mbona kila mtu anasema kama ipo ipo tu ni kitu gani hicho kisichotajwa?

Hicho kitu kitakuwa kinakusubilia wewe tu.?

Kitu gani kimejificha nyuma ya hizo sentesi zenu?

Mmejuaje kama kipo kwaajili yenu?

Ukiwaona wanasema hivyo ujue kuwa they are not sure kama wataolewa wanabahatisha na wametendwa sana
 
Mmmmhhh, nyie mabinti wa siku hizi mmetawaliwa na hofu sana, hata ndoa zenu zinakuwa za hofu hofu ndio sababu hazidumu.

Mnakosa vitu vizuri kwa hizi hofu zenu, yani hapa kila mmoja anavyosema utadhani yalisha mkuta kumbe ni hofu hana lolote.
Hofu nyingi sana maana yake wamekosa sifa na vigezo vya soko la ndoa
 
Kama ndoa ipo ipo tu huna haja ya kuisaka kwa tochi!!!
Kuna wanaoolewa wakiwa 20's,wengine 30's,40's mpaka 50's,huna sababu ya kubinuka sarakasi ili kuiwahisha cha muhimu ni subira.
Kuna principle za kuifupisha subira wakati wa Giza totoro la kihoro cha ndoa ndizo hizo hapo juu
 
Kuna principle za kuifupisha subira wakati wa Giza totoro la kihoro cha ndoa ndizo hizo hapo juu

Anayejisikia kufanya hayo ayafanye hayo na zaidi ila iwe kwa mapenzi,akiyafanya ili apate ndoa ni shida maana akiikosa ataumia sana na kuchanganyikiwa na akiipata atajibweteka akifika maana si tabia yake aliyafanya ili jamaa akate shauri,baada ya siku chache jamaa atagundua ule mng'ao aliouona kwa mbali kumbe haikuwa silver ni bati tu!!!
 
Ennie tunamaana upendo wa dhati ndo unazaa ndoa,Mwanamke a play role yake ya kike katika uhusiano,a add value to mans life kinyume na hivyo anaweza wasifikie lastest stage ya realationship(ndoa) because Man has nothing to lose akimuacha
 
Last edited by a moderator:
Valid points kabisa....suala sio kwamba ni lazima mwishoni iwe ndoa ila.ni kipimo cha kujua huyu anafaa kuwa mke au la maana sio wanawake wote.wanafaa kuwa wake

Cc Kongosho

Tobaaaa...!sasa wanawake wengine wameletwa hapa kuja kuwa nani...aisee
 
Last edited by a moderator:
Ennie tunamaana upendo wa dhati ndo unazaa ndoa,Mwanamke a play role yake ya kike katika uhusiano,a add value to mans life kinyume na hivyo anaweza wasifikie lastest stage ya realationship(ndoa) because Man has nothing to lose akimuacha

Hapo ndipo unapokosea mwekundu,kwa nini unadhani mwanamke tu ndio anapaswa ku add value kwa maisha ya mwanaume?
Kama wote mna target ya ndoa basi nyote mfanye juhudi kuiendea,juhudi zote kuzifanya mwanamke wakati mwanaume anapokea tu si sawa. Kuna watu wako kwenye ndoa usafi na mapishi anafanya dada wa kazi na kufua nguo zinapelekwa dry cleaner,kuna wanaofanya usafi kwa pamoja weekends!!!
Hapo kwa bold ipo kwa wanawake pia,kuna wanaume mkiachana ndio kwanza unahisi umetua mzigo.
Kikubwa ni kila mmoja afanye kwa nafasi yake!!!!
 
Last edited by a moderator:
[/B]

Leo tunazungumzia upande mmoja tu assuming that mwingine yuko na nia ame play role yake
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom