Siri kwa wanawake wasaka ndoa miaka nenda rudi

Siri kwa wanawake wasaka ndoa miaka nenda rudi

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
22,475
Reaction score
21,046
Hizi ndo marks (majibu) ya kupata ndoa mapema..........hii inawahusu hadi wale walio kwenye uchumba chronic/sugu
Hamna haja ya kunywa mchina uongeze makalio,wala kuenda kwa sangoma upate ndoa ndani ya siku 3 ,ukiona miaka mvua za masika zinakukatikia hujaitwa Mrs somebody habari

Hii hapa > Mambo ambayo mwanaume anafanya kukutest kama wewe msichana unafaa kuwa mke wake:
1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa.
2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakutest aone kama utasema "Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu".

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia "Baby twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia". Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!!

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!!

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio tule wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana.

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.
9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi.

11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia. Marks hizo.

Shukrani za dhati zimfikie mtungaji wa article hii ndg Masanja Mkandamizaji nawasilisha tujadili
 
Ndoa haisakwi, inakuja tu kwa muda muafaka kama besideis.

Ingekuwa inasakwa, lazima kungekuwa na makampuni ya kusaidia watu kusaka ndoa.

ha ha ha na wanaoenda kwa mganga wanafuata nini?ngoja nikubandikie bango la ndoa week moja tu na lile la kumvuta aliye mbali LOL
hizi ni simple principle bila kukimbilia kwa sangoma unadhani ndoa ni mchezo?
 
Au watu wanahamasishwa kuomba kwenye ibada wakati hayo hapo juu hawawezi kutekeleza,hembu jisaidie na Mungu ndo atakusaidia ,siku hizi hadi wachungaji wanawawinda waumini kwa kuwawaombea wapate ndoa wanaita WAFUNGULIWE
 
He he he, watu wana majanga yao, ndoa inakuwa kisingizio tu.

ha ha ha na wanaoenda kwa mganga wanafuata nini?ngoja nikubandikie bango la ndoa week moja tu na lile la kumvuta aliye mbali LOL
hizi ni simple principle bila kukimbilia kwa sangoma unadhani ndoa ni mchezo?
 
Umemaliza. Wapo ambao hawajishughulishi wakifika kwa wenza wao kisa wanahofia yatawakuta yaliyowakuta kwa wenza wa awali. Wanadai hadi ndoa kwanza ndo wawajibike. Hawafai
 
Ujumbe umewafikia nadhani...wachukue wasome kama notes ikibidi
 
Ukifanya hayo kwa lengo la kuisaka ndoa, halafu usipoipata unaweza ukachizika..!

Kama unafanya, fanya tuu kwa mapenzi uliyonayo kwa huyo bf wako na sio kwa kutegemea ndoa..!
ukifikia steji hiyo hujaona ndoa nenda kwa kiongozi wako wa dini ukafunguliwe usikimbilie kwa mganga
 
Kama ipo ipo tu,however point zipo hapo

Hizo za kama ipo ipo tu ndiyo zile mnazoingia kichwa kichwa hata mwaka hauishi msharudi home na vilio.

Jambo lolote zuri haliji hivi hivi linahitaji maandalizi ya kutosha

Usitegemee kukesha bar ma madisko halafu utegemee kuwa mama mzuri wa familia kesho.

Mtaoshwa sana maji kwa waganga.
 
Nawasikitikia sana mabinti wanao dhani kwamba swala la ndoa pia linabahati nasibu.

Mtapeleka kuku kwa waganga mpaka basi, mtaagizwa kuku wa njano, mkidhani kwamba mnamikosi kumbe maisha mnayakosea wenyewe.

Swala la ndoa ni soma pana sana linalohitaji umakini na usikivu wa kutosha, usitegemee kusinzia wakati wa somo halafu upate 100%, hapo tegemea -0%..
 
Umemaliza. Wapo ambao hawajishughulishi wakifika kwa wenza wao kisa wanahofia yatawakuta yaliyowakuta kwa wenza wa awali. Wanadai hadi ndoa kwanza ndo wawajibike. Hawafai
kisingizio hiko sikikubali kabla ya ndoa mapenzi ndo inabidi yawe ninyongorote niwehushe sana because ndoa is the lastest stage ya relationship
 
Nawasikitikia sana mabinti wanao dhani kwamba swala la ndoa pia linabahati nasibu.

Mtapeleka kuku kwa waganga mpaka basi, mtaagizwa kuku wa njano, mkidhani kwamba mnamikosi kumbe maisha mnayakosea wenyewe.

Swala la ndoa ni soma pana sana linalohitaji umakini na usikivu wa kutosha, usitegemee kusinzia wakati wa somo halafu upate 100%, hapo tegemea -0%..

teh teh sipati picha comment yako akiiona ambaye yuko stage hiyo
 
Back
Top Bottom