Siri kuu kuhusu Escrow zafichuka

Siri kuu kuhusu Escrow zafichuka

print_icon.gif

SIRI kuu ya James Rugemalira, kumwaga mabilioni ya shilingi kwa baadhi ya majaji wa mahakama kuu, viongozi waandamizi serikalini na madhehebu ya kidini, wabunge na viogogo wa Ikulu, zimeanza kufumuka.

Nyaraka mikononi mwa gazeti hili zinaonesha zaidi ya asilimia 90 ya wale waliopewa fedha na Rugemalira, ni wale waliomsaidia “kufanikisha ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 324 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT) na kujinasua katika mikono ya sheria.”

“Rugemalira alishika kila mmoja. Kuanzia Ikulu ya Jakaya Kikwete, TAKUKURU, mahakama, BoT, hazina, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, viongozi wa madhehebu ya kidini na hata baadhi ya mawaziri wa zamani wenye ushawishi serikalini,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi kutoka Ikulu.

Amesema, “…fedha katika akaunti ya Escrow zilihusisha mtandao mpana ulioratibiwa na Rugemalira na Harbinder Sigh Seth (Singasinga).”

Majaji wa mahakama kuu, Aloycious Mujulizi na Eudeus Ruhangisa, ni miongoni mwa waliokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Rugemalira; na walikuwa washauri wake wakuu wa kisheria.

Mawasiliano kati ya Jaji Mujulizi na Jaji Ruhangisa yalifanyika kupitia kwa Rugemalira mwenywe na katika eneo jingine kupitia kwa mkewe, Benedicta.

Jaji Mujulizi na Jaji Ruhangisa walitajwa bungeni na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuwa miongoni mwa vigogo waliopewa mgawo wa fedha hizo na Rugemalira.

Bunge liliagiza majaji hao wachunguzwe na wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria.

Hadi sasa, hakuna taarifa zozote kuwa majaji walichunguzwa na kuchukuliwa hatua.

Rugemalira alikuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa katika kampuni ya kigeni ya IPTL kupitia kampuni yake ya VIP Engineering and Marketing Limited.

Jaji Mujulizi na Ruhangisa walilipwa na Rugemalira kila mmoja Sh. 404 milioni.

Mabilioni ya shilingi yaliyohifadhiwa katika akaunti ya Escrow yalikwapuliwa na Harbinder Sigh Seth, aliyejiita mmiliki wa IPTL kwa msaada mkubwa wa Rugemalira na kile kilichoitwa, “amri ya mahakama.”

Seth alidai kumiliki IPTL kupitia kampuni yake ya Pan African Power Tanzania Limited (PAP).

MwanaHALISI linaweza kuthibitisha kuwa kati ya tarehe 13 na 26 Novemba 2014, kilikuwa kipindi ambacho Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ilimhoji Rugemalira juu ya ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow.

Aidha, ni katika kipindi hichohicho, Rugemalira alikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Jaji Mujulizi na Ruhangisa.

Wengine waliokuwa na mawasiliano na Rugemalira katika kipindi hicho, ni waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo; aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Bernard Membe na aliyekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi.

Aliyepata kuwa waziri wa utawala bora, Mathias Chakawe; aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah; aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali (AG), Frederick Werema na aliyekuwa waziri wa viwanda na biashara, Dk. Abdallah Kigoda, walikuwa pia na mawasiliano na Rugelalira.

Wengine ni naibu gavana wa BoT, Dk. Enos Bukuku; aliyekuwa Mnikulu Mkuu wa Ikulu, Shaban Gurumo; aliyekuwa Kamishna mkuu mamlaka ya mapato (TRA), Rished Bade na aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati wa ujio wa IPTL nchini (1994), Andrew Chenge.

Orodha ya waliokuwa katika mawasiliano na Rugemalira inahusisha pia mawaziri wa zamani, Paul Kimiti na Wilson Masilingi; aliyekuwa mhariri mtendaji wa magazeti ya serikali – Daily News na Habari Leo – Gabriel Nderumaki; aliyewahi kuwa waziri wa nishati na madini, Wiliam Ngeleja na mkurugenzi wa kampuni ya G and S Consultancy Limited, Dk. Gideon Shoo.

Wengine ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Constantine Massawe; Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilain; Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa na aliyekuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Prof. Anna Tibaijuka.

Prof. Tibaijuka alikiri kupokea kiasi cha Sh. 1.6 bilioni kutoka kwa Rugemalira. Hata hivyo, alisema kuwa fedha ambazo alipokea zilikuwa ni mchango wa shule yake ya Barbro Johanssen ya jijini Dar es Salaam na Kajumulo Girls High School iliyoko Bukoba.

Kwa mujibu wa taarifa, Dk. Hoseah alimruhusu Rugemalira kutafuta msaada popote pale, ikiwa ni pamoja na nje ya nchi na kwamba ofisi yake “ingetoa maofisa kumsaidia.”

“Kama una jambo la msingi kufanya nje ya nchi, una baraka zangu zote. Watakapohitajika maofisa wa TAKUKURU kwa ufafanuzi, wako tayari kukusaidia pale uliko,” anaeleza Dk. Hoseah na Rugemalira andishi lake la 16 Novemba 2014.

Dk. Hoseah anamaliza kwa kumueleza Rugemalira, “…nakutakia kila la kheri.”

Rugemalira alikuwa anaomba TAKUKURU kuingilia kati kile kinachoitwa, “mgogoro wa hisa kati ya IPTL na Benki ya Standard Chartered (SCB) ya Uingereza.”

Hata hivyo, Rugemalira anaonywa na Masilingi, ambaye wakati huo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, kuwa mwangalifu na mtulivu wakati suala hilo linaendelea.

Alisema, “mimi nikiwa mwanasheria, ninakushauri wewe na kampuni yako kushirikiana kwa ukamilifu na TAKUKURU. Suala la IPTL ni gumu. Limekuwa na mchanganyiko mkubwa. Akili nyingine haziwezi kulielewa.”

Masilingi anasema, “…nimebaini kwamba TAKUKURU ndio wanaolichukulia suala hilo kwa usiri mkubwa katika hatua za uchunguzi na wenyewe wanaweza kukusaidia kupata hukumu iliyo ya haki.”

Benki ya Standard Chartered ilikuwa inadai na mpaka sasa bado inadai kuwa mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL na fedha zilizopo kwenye akaunti ya Escrow, ni mali yake.

Inadai kuwa kampuni ya MECHMAR ya Malasia ilishindwa kurejesha mkopo iliochukua benki na kwamba hilo ni jambo linalosababisha mitambo ya IPTL iliyopo Tegeta Salasala, jijini Dar es Salaam, kuwa mali yake.

Akihutubia taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, wiki tatu baada ya Bunge kuagiza waliohusika katika wizi wa fedha za Escrow wachukuliwe hatua, aliyekuwa Rais wa Jamhuri, Jakaya Mrisho Kikwete alikiri kuwapo udanganyifu katika kufikia utoaji wa fedha hizo.

Alikiri baadhi ya nyaraka kughushiwa. Akakiri kuwa kampuni ya PAP imekwepa kodi ya serikali na kudai kuwa serikali yake bado inaendelea kuitafuta kampuni ya MECHMAR iliyodaiwa kuuza asimia 70 ya hisa zake ndani ya IPTL.

Rais alikiri kuwa aliyepewa fedha na serikali – PAP – hakuwa na sifa; serikali yake haikufanya uchunguzi yakinifu kuhusu historia, uhalali, sifa na uwezo wa kampuni ya PAP katika uwekezaji wa umeme, ununuzi wa mitambo na mtaji.

Naye mwanasheria wa Rugemalira, Camilo Schutte, katika barua aliyomwandikia Rugemalira, anasema “…baada ya kusoma ushauri wa Masilingi juu ya msaada wa TAKUKURU, itakuwa busara kuomba TAKUKURU kusubiri hukumu kati ya Standard Chartered na IPTL.”

Anasema kampuni ya Rugemalira (VIP) “…inapaswa kuomba TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya sera ya benki ya Standard Chartered kuhusu ununuzi wa madeni ambayo mchakato wake unaweza kuwa na rushwa.”

Camilo Schutte anamueleza Rugemalira katika barua yake hiyo na ambayo imenakiriwa kwa majaji, mawaziri, kiongozi wa TAKUKURU, maofisa wa Ikulu na watu wengine kuwa, “…tatizo la benki ya Standard Chartered, kama zilivyo taasisi nyingine, ni kufanya biashara ili kujipatia faida kubwa.”

Akiandika kwa Dk. Gideon Shoo, mwanasheria wa Rugemalira (Camilo Schutte) anaelekeza kufanyika mambo matatu kwa haraka.

Kwanza kutafuta, kwa “gharama yoyote ile,” watu wote wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii ambao wanapigia kelele ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Miongoni mwa waliotajwa, ni Zitto Kabwe, mbunge wa sasa wa Kigoma Mjini; David Kafulila, ambaye alikuwa mbunge wa Kigoma Kusini; Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose; Wilson Masilingi na balozi wa Finland nchini.

Pili, Camilo Schutte anasema, ni sharti mtandao wao ujiridhishe ikiwa watu wanaolizungumzia jambo hilo wanalifahamu kwa undani au wanalijua nusunusu au hawalijui kabisa.

Kwa maoni ya mwanasheria wa Rugemalira, wabunge waliokuwa wameshupalia jambo hilo walikuwa hawana taarifa zozote muhimu kuhusu suala hilo.

Tatu, mwanasheria alimtaka Dk. Shoo kuangalia athari za taarifa zilizosambazwa juu ya ukwapuaji wa fedha hizo, kwa kampuni ya IPTL na Rugemalira binafsi.

“Baada ya kukamilisha haya, naomba unijulishe haraka ili tuweze kupanga mikakati ya kukabiliana na kila tatizo nililolitaja hapo juu,” anaeleza Camilo Schutte.

Kupatikana kwa mawasiliano haya kumekuja mwaka mmoja na nusu baada ya mabilioni ya shilingi kukwapuliwa BoT; na Bunge kuelekeza serikali kufanya uchunguzi.

Aidha, kupatikana kwa taarifa kuwa Rugemalira alikuwa na mawasiliano ya karibu na “kindungu” na mkuu wa TAKUKURU, kumekuja wakati ambapo taasisi hiyo imeshindwa kuanika orodha ya watu walionufaika na mgawo wa fedha hizo kutoka benki ya Stanbic.

Bunge liliagiza serikali kufikisha mahakamani watuhumiwa wote wa Escrow, ikiwa ni pamoja na kufilisi mtambo wa IPTL na kuitangaza benki ya Stanbic kuwa taasisi ya kutakatisha fedha.

Bunge liliagiza pia kuchunguza na kuwajibisha majaji waliotajwa kunufaika na mgawo wa fedha kupitia benki ya Mkombozi na kumfukuza nchini, anayejiita mmiliki wa IPTL, Harbinder Sigh Seth.

Akizungumzia kutajwa kwa Dk. Hoseah na baadhi ya majaji katika mawasiliano na Rugemalira, mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amesema jambo hilo linaongeza shaka juu ya uadilifu wa viongozi wa CCM na serikali yake.

Ameliambia gazeti hili katika mahojiano kwa njia ya simu, “…hili liserikali lote limeoza. Kuanzia Ikulu, mfumo wa mahakama hadi viongozi wa madhehebu ya kidini; kote kumejaa rushwa.”

Lissua ameongeza, “Tulisema ndani ya Bunge, kwamba majaji wamehongwa na hivyo tukataka wachunguzwe, lakini serikali ya CCM imegoma kwa kuwa walioiba waliwajua na walishirikiana nao.”

Mwanasiasa huyo wa upinzani anasema, “utapeli huu ulifanywa na serikali ya Rais Kikwete, BoT, Benki ya Stanbic na PAP.”

Amesema, “…sasa kama kweli wanataka kusafisha nchi, basi waanzie hapo. Siyo kukimbizana na vidagaa. Waanze na maofisa wao wa Ikulu waliokuwa wameigeuza ofisi ya umma kuwa ofisi binafsi.”

Chanzo: MwanaHalisi
Cc.Dr.Magufuli
 
Wacha porojo. Lililohusika ni dhehebu moja la kikristo, Roman Catholic. Benki yao imetajwa na maaskofu wao wawili, Kilaini na Nzigirwa wote hao wa kanisa katoliki.

Madhehebu yepi mengine yaliyotajwa kuhusika?

Msikimbie kivuli chenu.
Ni kweli kabisa ni dhehebu moja tena wawe specific kuwa VIONGOZI WA KANISA KATOLIKI neno madhehebu is to wide and broad wakati ukweli uu wazi
 
..mimi nitaamini kuwa JPM anapambana kweli na wezi wa Mali za umma kama atawakamata mwezi wa escrow na kufungulia mashtaka..maana huo mtandao wa ruge uliwahusisha moja kwa moja vigogo wa serikali....Tunataka tujue wale waliobeba mapema kwenye sandarusi stanbic... Na ile kampuni ya simba trust iliyotajwa kunufaika na escrow..na baadae kutoweka kabisa mitandaoni...tuwajue wamiliki wake....na pia tuone matakwa ya bunge yakitekelezwa jumla...vinginevyo vita ya ufisadi iko biased...na wanaolengwa wanafanyiwa hivyo selectively...
 
Andikeni basi pia waliochukuwa pesa Stanbic kwa malumbesa. Au hao ni untouchable!

Tembelea mabenki, watu wanachukuwa na kuweka pesa kwa malori ya deraya na haiwi mwao.

Ni punguani tu ataeona ajabu mtu kutoka benki na malumbesa ya pesa. Ulitaka atoke benki na vinoti vya kujaa mkononi? Hivyo siku hizi si kwa wakala wa mpesa, tigopesa, airtel money.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Nimesoma bandiko zima, hakuna "madhehebu" niliyoyaona isipokuwa dhehebu moja tu tena ni la Kanisa katoliki na maaskofu wake wawili na benki yao ya mkombozi ndiyo waliohusika. Sasa kwanini mjidai ni "madhehebu"?
kwahiyo unakubaliana na watu wanaosema waislamu wote ni ni ISIS?
 
Tembelea mabenki, watu wanachukuwa na kuweka pesa kwa malori ya deraya na haiwi mwao.

Ni punguani tu ataeona ajabu mtu kutoka benki na malumbesa ya pesa. Ulitaka atoke benki na vinoti vya kujaa mkononi? Hivyo siku hizi si kwa wakala wa mpesa, tigopesa, airtel money.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
hawakusoma elimu dunia hao mama
 
print_icon.gif

SIRI kuu ya James Rugemalira, kumwaga mabilioni ya shilingi kwa baadhi ya majaji wa mahakama kuu, viongozi waandamizi serikalini na madhehebu ya kidini, wabunge na viogogo wa Ikulu, zimeanza kufumuka.

Nyaraka mikononi mwa gazeti hili zinaonesha zaidi ya asilimia 90 ya wale waliopewa fedha na Rugemalira, ni wale waliomsaidia “kufanikisha ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 324 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT) na kujinasua katika mikono ya sheria.”

“Rugemalira alishika kila mmoja. Kuanzia Ikulu ya Jakaya Kikwete, TAKUKURU, mahakama, BoT, hazina, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, viongozi wa madhehebu ya kidini na hata baadhi ya mawaziri wa zamani wenye ushawishi serikalini,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi kutoka Ikulu.

Amesema, “…fedha katika akaunti ya Escrow zilihusisha mtandao mpana ulioratibiwa na Rugemalira na Harbinder Sigh Seth (Singasinga).”

Majaji wa mahakama kuu, Aloycious Mujulizi na Eudeus Ruhangisa, ni miongoni mwa waliokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Rugemalira; na walikuwa washauri wake wakuu wa kisheria.

Mawasiliano kati ya Jaji Mujulizi na Jaji Ruhangisa yalifanyika kupitia kwa Rugemalira mwenywe na katika eneo jingine kupitia kwa mkewe, Benedicta.

Jaji Mujulizi na Jaji Ruhangisa walitajwa bungeni na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuwa miongoni mwa vigogo waliopewa mgawo wa fedha hizo na Rugemalira.

Bunge liliagiza majaji hao wachunguzwe na wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria.

Hadi sasa, hakuna taarifa zozote kuwa majaji walichunguzwa na kuchukuliwa hatua.

Rugemalira alikuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa katika kampuni ya kigeni ya IPTL kupitia kampuni yake ya VIP Engineering and Marketing Limited.

Jaji Mujulizi na Ruhangisa walilipwa na Rugemalira kila mmoja Sh. 404 milioni.

Mabilioni ya shilingi yaliyohifadhiwa katika akaunti ya Escrow yalikwapuliwa na Harbinder Sigh Seth, aliyejiita mmiliki wa IPTL kwa msaada mkubwa wa Rugemalira na kile kilichoitwa, “amri ya mahakama.”

Seth alidai kumiliki IPTL kupitia kampuni yake ya Pan African Power Tanzania Limited (PAP).

MwanaHALISI linaweza kuthibitisha kuwa kati ya tarehe 13 na 26 Novemba 2014, kilikuwa kipindi ambacho Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ilimhoji Rugemalira juu ya ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow.

Aidha, ni katika kipindi hichohicho, Rugemalira alikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Jaji Mujulizi na Ruhangisa.

Wengine waliokuwa na mawasiliano na Rugemalira katika kipindi hicho, ni waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo; aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Bernard Membe na aliyekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi.

Aliyepata kuwa waziri wa utawala bora, Mathias Chakawe; aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah; aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali (AG), Frederick Werema na aliyekuwa waziri wa viwanda na biashara, Dk. Abdallah Kigoda, walikuwa pia na mawasiliano na Rugelalira.

Wengine ni naibu gavana wa BoT, Dk. Enos Bukuku; aliyekuwa Mnikulu Mkuu wa Ikulu, Shaban Gurumo; aliyekuwa Kamishna mkuu mamlaka ya mapato (TRA), Rished Bade na aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati wa ujio wa IPTL nchini (1994), Andrew Chenge.

Orodha ya waliokuwa katika mawasiliano na Rugemalira inahusisha pia mawaziri wa zamani, Paul Kimiti na Wilson Masilingi; aliyekuwa mhariri mtendaji wa magazeti ya serikali – Daily News na Habari Leo – Gabriel Nderumaki; aliyewahi kuwa waziri wa nishati na madini, Wiliam Ngeleja na mkurugenzi wa kampuni ya G and S Consultancy Limited, Dk. Gideon Shoo.

Wengine ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Constantine Massawe; Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilain; Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa na aliyekuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Prof. Anna Tibaijuka.

Prof. Tibaijuka alikiri kupokea kiasi cha Sh. 1.6 bilioni kutoka kwa Rugemalira. Hata hivyo, alisema kuwa fedha ambazo alipokea zilikuwa ni mchango wa shule yake ya Barbro Johanssen ya jijini Dar es Salaam na Kajumulo Girls High School iliyoko Bukoba.

Kwa mujibu wa taarifa, Dk. Hoseah alimruhusu Rugemalira kutafuta msaada popote pale, ikiwa ni pamoja na nje ya nchi na kwamba ofisi yake “ingetoa maofisa kumsaidia.”

“Kama una jambo la msingi kufanya nje ya nchi, una baraka zangu zote. Watakapohitajika maofisa wa TAKUKURU kwa ufafanuzi, wako tayari kukusaidia pale uliko,” anaeleza Dk. Hoseah na Rugemalira andishi lake la 16 Novemba 2014.

Dk. Hoseah anamaliza kwa kumueleza Rugemalira, “…nakutakia kila la kheri.”

Rugemalira alikuwa anaomba TAKUKURU kuingilia kati kile kinachoitwa, “mgogoro wa hisa kati ya IPTL na Benki ya Standard Chartered (SCB) ya Uingereza.”

Hata hivyo, Rugemalira anaonywa na Masilingi, ambaye wakati huo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, kuwa mwangalifu na mtulivu wakati suala hilo linaendelea.

Alisema, “mimi nikiwa mwanasheria, ninakushauri wewe na kampuni yako kushirikiana kwa ukamilifu na TAKUKURU. Suala la IPTL ni gumu. Limekuwa na mchanganyiko mkubwa. Akili nyingine haziwezi kulielewa.”

Masilingi anasema, “…nimebaini kwamba TAKUKURU ndio wanaolichukulia suala hilo kwa usiri mkubwa katika hatua za uchunguzi na wenyewe wanaweza kukusaidia kupata hukumu iliyo ya haki.”

Benki ya Standard Chartered ilikuwa inadai na mpaka sasa bado inadai kuwa mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL na fedha zilizopo kwenye akaunti ya Escrow, ni mali yake.

Inadai kuwa kampuni ya MECHMAR ya Malasia ilishindwa kurejesha mkopo iliochukua benki na kwamba hilo ni jambo linalosababisha mitambo ya IPTL iliyopo Tegeta Salasala, jijini Dar es Salaam, kuwa mali yake.

Akihutubia taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, wiki tatu baada ya Bunge kuagiza waliohusika katika wizi wa fedha za Escrow wachukuliwe hatua, aliyekuwa Rais wa Jamhuri, Jakaya Mrisho Kikwete alikiri kuwapo udanganyifu katika kufikia utoaji wa fedha hizo.

Alikiri baadhi ya nyaraka kughushiwa. Akakiri kuwa kampuni ya PAP imekwepa kodi ya serikali na kudai kuwa serikali yake bado inaendelea kuitafuta kampuni ya MECHMAR iliyodaiwa kuuza asimia 70 ya hisa zake ndani ya IPTL.

Rais alikiri kuwa aliyepewa fedha na serikali – PAP – hakuwa na sifa; serikali yake haikufanya uchunguzi yakinifu kuhusu historia, uhalali, sifa na uwezo wa kampuni ya PAP katika uwekezaji wa umeme, ununuzi wa mitambo na mtaji.

Naye mwanasheria wa Rugemalira, Camilo Schutte, katika barua aliyomwandikia Rugemalira, anasema “…baada ya kusoma ushauri wa Masilingi juu ya msaada wa TAKUKURU, itakuwa busara kuomba TAKUKURU kusubiri hukumu kati ya Standard Chartered na IPTL.”

Anasema kampuni ya Rugemalira (VIP) “…inapaswa kuomba TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya sera ya benki ya Standard Chartered kuhusu ununuzi wa madeni ambayo mchakato wake unaweza kuwa na rushwa.”

Camilo Schutte anamueleza Rugemalira katika barua yake hiyo na ambayo imenakiriwa kwa majaji, mawaziri, kiongozi wa TAKUKURU, maofisa wa Ikulu na watu wengine kuwa, “…tatizo la benki ya Standard Chartered, kama zilivyo taasisi nyingine, ni kufanya biashara ili kujipatia faida kubwa.”

Akiandika kwa Dk. Gideon Shoo, mwanasheria wa Rugemalira (Camilo Schutte) anaelekeza kufanyika mambo matatu kwa haraka.

Kwanza kutafuta, kwa “gharama yoyote ile,” watu wote wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii ambao wanapigia kelele ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Miongoni mwa waliotajwa, ni Zitto Kabwe, mbunge wa sasa wa Kigoma Mjini; David Kafulila, ambaye alikuwa mbunge wa Kigoma Kusini; Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose; Wilson Masilingi na balozi wa Finland nchini.

Pili, Camilo Schutte anasema, ni sharti mtandao wao ujiridhishe ikiwa watu wanaolizungumzia jambo hilo wanalifahamu kwa undani au wanalijua nusunusu au hawalijui kabisa.

Kwa maoni ya mwanasheria wa Rugemalira, wabunge waliokuwa wameshupalia jambo hilo walikuwa hawana taarifa zozote muhimu kuhusu suala hilo.

Tatu, mwanasheria alimtaka Dk. Shoo kuangalia athari za taarifa zilizosambazwa juu ya ukwapuaji wa fedha hizo, kwa kampuni ya IPTL na Rugemalira binafsi.

“Baada ya kukamilisha haya, naomba unijulishe haraka ili tuweze kupanga mikakati ya kukabiliana na kila tatizo nililolitaja hapo juu,” anaeleza Camilo Schutte.

Kupatikana kwa mawasiliano haya kumekuja mwaka mmoja na nusu baada ya mabilioni ya shilingi kukwapuliwa BoT; na Bunge kuelekeza serikali kufanya uchunguzi.

Aidha, kupatikana kwa taarifa kuwa Rugemalira alikuwa na mawasiliano ya karibu na “kindungu” na mkuu wa TAKUKURU, kumekuja wakati ambapo taasisi hiyo imeshindwa kuanika orodha ya watu walionufaika na mgawo wa fedha hizo kutoka benki ya Stanbic.

Bunge liliagiza serikali kufikisha mahakamani watuhumiwa wote wa Escrow, ikiwa ni pamoja na kufilisi mtambo wa IPTL na kuitangaza benki ya Stanbic kuwa taasisi ya kutakatisha fedha.

Bunge liliagiza pia kuchunguza na kuwajibisha majaji waliotajwa kunufaika na mgawo wa fedha kupitia benki ya Mkombozi na kumfukuza nchini, anayejiita mmiliki wa IPTL, Harbinder Sigh Seth.

Akizungumzia kutajwa kwa Dk. Hoseah na baadhi ya majaji katika mawasiliano na Rugemalira, mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amesema jambo hilo linaongeza shaka juu ya uadilifu wa viongozi wa CCM na serikali yake.

Ameliambia gazeti hili katika mahojiano kwa njia ya simu, “…hili liserikali lote limeoza. Kuanzia Ikulu, mfumo wa mahakama hadi viongozi wa madhehebu ya kidini; kote kumejaa rushwa.”

Lissua ameongeza, “Tulisema ndani ya Bunge, kwamba majaji wamehongwa na hivyo tukataka wachunguzwe, lakini serikali ya CCM imegoma kwa kuwa walioiba waliwajua na walishirikiana nao.”

Mwanasiasa huyo wa upinzani anasema, “utapeli huu ulifanywa na serikali ya Rais Kikwete, BoT, Benki ya Stanbic na PAP.”

Amesema, “…sasa kama kweli wanataka kusafisha nchi, basi waanzie hapo. Siyo kukimbizana na vidagaa. Waanze na maofisa wao wa Ikulu waliokuwa wameigeuza ofisi ya umma kuwa ofisi binafsi.”

Chanzo: MwanaHalisi
Ruge akihamia Chadema hili gazeti litakanusha yote haya
 
pole sana..kiswahili ni chetu ila kinatupiga chenga....neno madhehebu halina umoja chukua kamusi ya TUKI utaona hilo...ni kama neno mafuta utasema umoja wake ni futa?
kweli msaidie maana dada kapata sababu yake ya kuipiga fimbo madhehebu ya kikristu. Hivi tatizo linakuwaje watu wanaoleta dini katika mambo ya muhimu? Hivi ni shule ama ujinga wanaousoma katika madrasa na sunday school. Ndiyo maana mimi siamini hata kama kuna watu walikuja na majina ya Yesu ama Mohamed ni utapeli tu.
 
Usisahau na baadhi ya waumini wao waliohusika mpaka wakasahau kwa kuna mungu na wakakejeli jasho la wananchi na kuliita pesa za mboga.
Hakika hukumu itakuwa juu yao wasipo tubu.
Wewe una matatizo sana, unakumbuka Mwembechai watu walileta mpaka mapanga msikitini unadhani tatizo lilikua nini? Nadhani lile n ni kanisa katoliki linaloadhini asubuhi ama siyo?
 
Tembelea mabenki, watu wanachukuwa na kuweka pesa kwa malori ya deraya na haiwi mwao.

Ni punguani tu ataeona ajabu mtu kutoka benki na malumbesa ya pesa. Ulitaka atoke benki na vinoti vya kujaa mkononi? Hivyo siku hizi si kwa wakala wa mpesa, tigopesa, airtel money.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Akiwasilisha ripoti hiyo bungeni, aliyekuwa Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini alipokea Sh80.5 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye Simon Sh40.4 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira.

Na hizo pesa zote zilipitia kwenye benki ya Kanisa Mkombozi Bank unadhani zilipitia huko kwa bahati mbaya.

Halafu wanaleta double standard kufucha uchafu wa Kanisa kuwa waliochukuwa pesa hizo ni viongozi wa madhehebu ya kidini madhehebu yapi hayo?

Watutajie basi haya madhehebu mengine viongozi wao walikuwemo kwenye mgao wa Escrow.

Hii nchi imejaa wanafiki sana watu wanajifanya wazalendo wanaumizwa na ufisadi kumbe unafiki mkubwa.

Ni punguani peke yake ndiyo anaweza kulitoa Kanisa kwenye sakata la Escrow.
 
kweli msaidie maana dada kapata sababu yake ya kuipiga fimbo madhehebu ya kikristu. Hivi tatizo linakuwaje watu wanaoleta dini katika mambo ya muhimu? Hivi ni shule ama ujinga wanaousoma katika madrasa na sunday school. Ndiyo maana mimi siamini hata kama kuna watu walikuja na majina ya Yesu ama Mohamed ni utapeli tu.
Kukata mzizi wa fitina tutajie basi kiongozi hata mmoja wa madhehebu ya dini aliyepewa mgao wa Escrow.
 
Hata lifti kwenye gari za familia ya rugemalila sitaki,hili zee jizi bila aibu,halafu wanawe hasa Jer*&#~☆♤e anajifanya eti mtafutaji wakati amezaliwa na mwizi mkubwa!
Nyerere angemfilisi huyu chor
 
Ni watu kwenye vichwa vya panzi tu wanaweza kuamini tena yanayoandikwa na gazeti hili hata kama ni ya kweli, simply because halina credibility tena mbele ya watu wanaojielewa save for Nyumbuz.
Hivi kuna tofauti gani kati ya kilichoandikwa humo ndani na yale yale yaliyokuwa yakiandikwa dhidi ya Lowasa, Rugemalila na SINGA SINGA kesho wakija UKAWA nyie ndo hawa hawa ndo watakuwa wakwanza kuwasafisha.
Ni hatari sana kwa taifa kuwa na viongoz wanafiki na wachumia tumbo kama Kubenea!!
 
Akiwasilisha ripoti hiyo bungeni, aliyekuwa Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini alipokea Sh80.5 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye Simon Sh40.4 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira.

Na hizo pesa zote lilipitia kwenye benki ya Kanisa Mkombozi Bank.

Halafu wananaleta double standard kuwa waliochilukuwa pesa hizo ni viongozi wa madhehebu ya kidini madhehebu yapi hayo.

Watutajie basi haya madhehebu mengine viongozi wao walikuwemo kwenye mgao wa Escrow.

Hii nchi imejaa wanafiki sana watu wanajifanya wazalendo wanaumizwa na ufisadi kumbe unafiki mkubwa.

Ni punguani peke yake ndiyo anaweza kulitoa Kanisa kwenye sakata la Escrow.
Na ndio maana hii kesi haieleweki sababu kuna Mkombozi Bank na Mababa Askofu.
 
Viongozi wa Kiislam wangekuwemo kwenye mgao huo sipati picha hawa jamaa wangetoa matusi tungekoma humu JF lakini walipewa mgao ni Maskofu imebakia funika kombe...
 
Jf!!! toka lini kukawa na dhambi ya jumla ya waislamu au wakristo?
Wajapani mtu akikosea na kutenda tendo lenye kuleta kashfa, kashfa hiyo si yake pekee yake ni ya familia yote ya ukoo wote. Ndugu zetu hao huenda mbali hata kujiua kurejesha heshima ya familia. Maana yangu ni kuwa ukiwanyonyeshea kidole wale ndugu waliohusika katika shida ya Escrow wanyonyeshee kidole kama watu binafsi waliotenda makosa kama watu binafsi na kuwajibika binafsi na siyo kwa sababu wanaabudu katika dhehebu fulani la dini. Ukiwatambua kwa udini wao basi na sisi tutachambua kwa mantiki kama hiyo niliyoianisha hapo mwanzo. Mara ngapi hapa tumesoma wananchi wakisikitika juu ya kukamatwa kwa Watanzania na madawa ya kulevya Uchina na kukiri wazi kuwa hiyo ni aibu ya taifa??? Hivi tunajadili mada kwa makini ama tunacheza tu? Kwa taarifa zipo dhambi za jumla kwa mfano rejea Akan wa Biblia (Joshua 7:1 - 26 soma kisa chote). Mtu huyu pekee alifanya dhambi nayo ikawagharimu Israel wote kushindwa vita kule Ai "1 Lakini Waisraeli hawakumtii Mungu. Alikuwepo mtu kutoka katika kabila la Yuda aliyeitwa Akani mwana wa Karmi, mjukuu wa Zimri, kitukuu wa Zerah. Akani alichukua vitu ambavyo vilitakiwa kuharibiwa. Hivyo BWANA akawakasirikia sana Waisraeli.(Joshua 7:1). Ukianza kuzungumzia dhambi unaingia katika uwanja wa kithiolojia siyo siasa tena na hoja zinazohusika zitajibiwa kithiolojia mtu atachagua ni thiolojia ipi atakayotumia kuleta mirejesho yake; Je ni thiolojia ya Biblia (Ya Kikristo) ama ni ile ya KiVeda ama Ramayana (ya Kihindu). Je atatumia kihunzi cha kidini toka mafundisho ya Sidharta Sakyamuni (Gautama Buddha) ama yale ya Kung Fu Tze (Confuscious). Ulileta suala la kithiolojia na sisi tuliona vema tulielekee namna hiyo hiyo. Vielelezo ni vingi ambavyo tungeweza kuvitumia kuthibitisha ya kuwa kosa la mmoja laweza kuathiri wengi na haki ya mmoja inaweza kuokoa wengi soma Yeremia 5:1 Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo. Unakumbuka maneno ambayo Yesu aliwajibu wale ndugu waliokuwa wakimsakama yule mama? Soma Yohana 8: 3 - 7 : - "Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. 4Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. 5Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? * 6Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 7Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe." Ombi langu tukijadili siasa tuijadili katika viwango na mantiki za kisiasa tukihama na kuingia katika maudhui ya kidini mchangiaji anapata haki ya kutoa majibu ya kidini yaani ya kithiolojia na hapo ndipo mitazamo inakinzana. Nadhani ndivyo nilivyofanya na ikaonekana niko nje kabisa ya fikra za kisiasa.
 
Blind reference to issues! Kwa hiyo msukuma mmoja akikosa ni kosa la wassukuma wote? Injinia mmoja akiharibu basi ni mainjinia wote? CDM mmoja mwezi basi ni CDM wote? Where is your generalization ends? Wholesome conclusion based on "on surface analysis" ends up with laughing materials like yours. Anyway it was a good collection of words for nothing!
 
Nimeeleweka! Usihamaki! Eleza hoja za ziada kama unazo. Lakini nimeeleweka na walionielewa hasa kutoka mrengo niliouletea mchango wangu!
 
Mkuu sina hamaki! Nilikunajaribu kupata ufahamu wako kwa ulichoandika. Mjapani kuna cultural influence tofauti kabisa na mataifa mengine! Hiyo theological evidence sijaona uchambuzi wa kunishawishi. Nini mipaka ya hiyo dhambi ya jumla, kama ipo! Tunajaribu kuwa wataalam wakati hatuna uelewa wa swala lenyewe. Ndio maana layman kama mimi common sense inaniambia hapana huna huo umahiri!
 
Back
Top Bottom