Siri kuu kuhusu Escrow zafichuka

Siri kuu kuhusu Escrow zafichuka

Rugemalira alishika kila mmoja. Kuanzia Ikulu ya Jakaya Kikwete, TAKUKURU, mahakama, BoT, hazina, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, viongozi wa madhehebu ya kidini na hata baadhi ya mawaziri wa zamani wenye ushawishi serikalini,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi kutoka Ikulu.

Hahahhahaha!!! Badala kusema Maaskofu na Benki ya Kanisa Katoliki Mkombozi, mnajifanya kuandika viongozi wa madhehebu ya dini.

Wagalatia bana....
Ikulu si alikuwepo Sheikh Kikwete ?
 
Magufuri sio kuwa anaogopa Escrow,anataka kujiridhisha ni njia gani aitumie kutumbua majipu ya Escrow.Escrow ina ugumu kuitumbua kwa sababu wamo watu mashuhuri kutoka mihimili yote.Pili Escow haikugusa baadhi ya watu au taasisi muhimu za umma kwasababu sio rahisi kuwakamata achilia mbali kuwafungulia mashtaka.Magufuri analijua hilo anasubiri muda muafaka atajibu mapigo.
 
kwani analipwa na serikali huo mashahara?
Mbowe anaendesha gari LA serikali na analipwa mshahara kama KUB.

Pia anapokea ruzuku ya chadema kutoka serikalini.
Kwa hiyo ni vizuri akaweka wazi mshahara.
 
Mbowe anaendesha gari LA serikali na analipwa mshahara kama KUB.

Pia anapokea ruzuku ya chadema kutoka serikalini.
Kwa hiyo ni vizuri akaweka wazi mshahara.
sasa mbona vyama vyote vinapokea ruzuku toka serikalini sasa why umempick only mboe?
 
Sheria zetu zina mapungufu mkubwa sana, mkikurupuka na kupeleka watu mahakamani tutaishia kushindwa.
Magufuli hawezi ingia kwenye mitego hiyo.
Lakini tujifunze kuthamini kazi za wenzetu, Escrow ni Billion 350, then unasema JPM ana deal na vidagaa.
Kweli TCRA over 600 Billion
TRA zaidi ya Trillio 3
MSD over Bill 100
Taratibu tutafika tunapotaka kufika

Umesahau na...mishahara hewa. Zaidi ya Billioni 100 kila mwaka!
 
hiloooo limeumbuka kimbelembele tuu jamvin
hiloooo limeumbuka kimbelembele tuu jamvin

Wakuniunbuwa ni nani na huu aliowapa Ritz umekuwa ugali wa moto wagalatia kuumeza:

Tanzania kumejaa wanafiki sana unataka kuitoa Kanisa Katoliki na kwenye ufisadi wa Escrow?

Maaskofu pamoja na benki ya Kanisa wameshiriki kufanya ufisadi.

Tuwe wakweli
 
Hili la kukamata hawa mafisadi wa Escrow Magufuli analikwepa kiaina kama ugonjwa wa ukoma, Lugumi nayo anaingalia kwa mbali kama hayupo vile pia na masakata ya kutaka kupora makampuni ya PRIDE na UDA ambayo yanafanyika mbele ya macho yetu mchana kweupe na huyu ndiye alidai kwamba anataka kutokomeza ufisadi nchini. Hawakukosea kabisa waliosema CCM ni ile ile hawana jipya.

Nilishasema kama magufuli amezaliwa mwanaume,akamate hawa wa escrow. Otherwise anaonea watu.
 
Mnalalamika nchi imeoza, wakikamuliwa waliooza pia mnalalamika, kila kitu kwenu ni kulalamika, wanafiki wakubwa!
Akamate ESCROW uone kama watu watalalamika. Huko ndiko kwenye mahela, sio huko kwenye mke wa waziri anakoromeana na trafiki
 
"madhehebu ya kidini", ukweli ni dhehebu moja tu tena ni la kanisa katoliki ndilo lililotumika.
Habari zako mama! Kanisa Katoliki lipo pande zote duniani; hadi Iran. Huko hawamjui Ruge
 
Hii sentensi si kweli:
"madhehebu ya kidini", ukweli ni dhehebu moja tu tena ni la kanisa katoliki ndilo lililotumika.

Kwanini mpotoshe na kusema "madhehebu"?

Cc BAK
336_ruge.JPG
Hakuna, katika Kiswahili, neno 'dhehebu'. Neno zima ni madhehebu. Kiambilishi ma- hapo siyo kiishiria cha wingi, bali ni shina la tamko, dada yangu.
Ni kama vile maji, mavu/i, maslahi, mamlaka, maskani,machweo, maisha, mauti....nk
Hivyo: madhehebu ya Kiislamu, Kinaswara, Kihindi, Kikalasinga n.k.
 
Nafikiri sio dhehebu au kanisani katoliki bali viongozi wa kidini wawili kutoka kanisa katoliki ndio waliotajwa kwa majina!!!
Mimi nichangie hivi: Wakatoliki wanauwakilisha Ukristo, Wapentekoste, Wadventista na Walutheri wote hao ni Wakristo. Mmojawapo wa watumishi wa madhehebu hayo akipata shida ni shida ya Wakristo wote. Hatuwezi kusema hiyo ni ya Wakatoliki ama hiyo ni ya Walokole wa Kipentekoste. Ni Ukristo umepata shida. Walipochanganya mambo pale uwanja wa ndege miaka michache iliyopita, wale jamaa wa Sabato Masalia, wakidai wanao wito wa kwenda Ulaya yote kuhubiri, huku hawajazingatia utaratibu ambao wenzao katika Biblia (Akina Nehemia na Ezra) walizingatia ilikuwa ni aibu ya Ukristo si tu ya Wasabato. Kilichowapata ndugu zetu Wakatoliki hao watumishi kimetugusa wote tulio Wakristo. Tunatubu pamoja nao na tunamwomba Mungu kwa ajili yao tunachukuliana mizigo na kuombeana. Ni kweli jukumu la kuwarudi lipo kwa uongozi wa madhehebu yao moja kwa moja, sisi Wakristo tuliobaki hatuwezi kukwepa na kusema "Sio Mimi!" ama "Sio Sisi!" La Hasha! Bali tutasema Mungu tusaidie sisi Wakristo wenye dhambi tusamehe makosa yetu sisi sote na wenzetu hao uturehemu na utusaidie tusifanye hivyo tena. Hapo ndipo neema ya Mungu itakuja. Nawasilisha!
 
Akamate ESCROW uone kama watu watalalamika. Huko ndiko kwenye mahela, sio huko kwenye mke wa waziri anakoromeana na trafiki

Escrow gani tena? PCCB wameshasema zile pesa simali ya umma na wenyewe wamepewa wewe unataka nini? Au kwa vile umeziona nyingi ndio maana hutaki watu wapewe? Akaunti ya Escrow ilifunguliwa kuhifadhi fedha ambazo Tanesco na IPTL walikuwa wameshindwa kupatana kuhusu kiasi gani kilipwe katika capacity charge. Maamuzi yalipofanyika malipo yakafanywa, sasa hebu tufungue macho wizi au ubadhirifu wa Escrow uko wapi?
 
Mbowe anaendesha gari LA serikali na analipwa mshahara kama KUB.

Pia anapokea ruzuku ya chadema kutoka serikalini.
Kwa hiyo ni vizuri akaweka wazi mshahara.
Toka humo we! Hapa wanajadili mambo ya moto yanayounguza moyo wa ngosha wewe unazungumzia mambo ya mshahara! Nenda kwa Ndugai atakuambia
 
Hakuna, katika Kiswahili, neno 'dhehebu'. Neno zima ni madhehebu. Kiambilishi ma- hapo siyo kiishiria cha wingi, bali ni shina la tamko, dada yangu.
Ni kama vile maji, mavu/i, maslahi, mamlaka, maskani,machweo, maisha, mauti....nk
Hivyo: madhehebu ya Kiislamu, Kinaswara, Kihindi, Kikalasinga n.k.
Wacha porojo. Lililohusika ni dhehebu moja la kikristo, Roman Catholic. Benki yao imetajwa na maaskofu wao wawili, Kilaini na Nzigirwa wote hao wa kanisa katoliki.

Madhehebu yepi mengine yaliyotajwa kuhusika?

Msikimbie kivuli chenu.
 
Andikeni basi pia waliochukuwa pesa Stanbic kwa malumbesa. Au hao ni untouchable!
 
Mimi nichangie hivi: Wakatoliki wanauwakilisha Ukristo, Wapentekoste, Wadventista na Walutheri wote hao ni Wakristo. Mmojawapo wa watumishi wa madhehebu hayo akipata shida ni shida ya Wakristo wote. Hatuwezi kusema hiyo ni ya Wakatoliki ama hiyo ni ya Walokole wa Kipentekoste. Ni Ukristo umepata shida. Walipochanganya mambo pale uwanja wa ndege miaka michache iliyopita, wale jamaa wa Sabato Masalia, wakidai wanao wito wa kwenda Ulaya yote kuhubiri, huku hawajazingatia utaratibu ambao wenzao katika Biblia (Akina Nehemia na Ezra) walizingatia ilikuwa ni aibu ya Ukristo si tu ya Wasabato. Kilichowapata ndugu zetu Wakatoliki hao watumishi kimetugusa wote tulio Wakristo. Tunatubu pamoja nao na tunamwomba Mungu kwa ajili yao tunachukuliana mizigo na kuombeana. Ni kweli jukumu la kuwarudi lipo kwa uongozi wa madhehebu yao moja kwa moja, sisi Wakristo tuliobaki hatuwezi kukwepa na kusema "Sio Mimi!" ama "Sio Sisi!" La Hasha! Bali tutasema Mungu tusaidie sisi Wakristo wenye dhambi tusamehe makosa yetu sisi sote na wenzetu hao uturehemu na utusaidie tusifanye hivyo tena. Hapo ndipo neema ya Mungu itakuja. Nawasilisha!
Jf!!! toka lini kukawa na dhambi ya jumla ya waislamu au wakristo?
 
Back
Top Bottom