Siri kuu kuhusu Escrow zafichuka

Siri kuu kuhusu Escrow zafichuka

Hivi wale viongozi wa kiroho waliopata ule "mgao" bado waumini wanaenda kukiri na kueleza dhambi zao kwao??
 
Hii sentensi si kweli:
"madhehebu ya kidini", ukweli ni dhehebu moja tu tena ni la kanisa katoliki ndilo lililotumika.

Kwanini mpotoshe na kusema "madhehebu"?

Cc BAK
336_ruge.JPG
Uko sahihi, tena ikihusisha hata benki inajidai ya kanisa. Mkombozi. Wanajidai kuhubiri amani wakati ni walafi wa pesa na inavyoonekana ukabila pia ulitumika.
 
Kuna maeneo mengine huwezi kugusa labda uwe na moyo wa simba........
Kimo hiki magufuli hakiwezi
Sijui nani anamshauri vizuri rais huyu. Kwa ushauri na maoni yangu nahisi bado hajashindwa kuendelea na hao tunaodhani ni vigumu kuwagusa.

Rais aliyeondoka bado ana wafuasi wake wa miaka mingi. Pia bado kuna washabiki wake kwa wingi sana na nadhani inaonekana wazi hata hapa JF. Kuna watu wanapoona amesahaulika, wanaleta topic ya kumsifu. Hata akisafiri bado wanapiga filimbi ili aonekane.

JPM lazima ampe nafasi kiumbe mstaafu apoteze umaarufu na hapo sasa ndo kuna kila sababu ya kuhangaika na akina escrow.
 
"...Every journey taken always includes the path not taken, the detour through hell, the crossroads of indecision and the long way home..."
 
Vijana wa book 7 kwa hili la Escraw na Lugumi hata AIBU hawana! wamejitoa ufahamu kabisa!
 
Jibu lipo kwenye rasmi ya pili ya katiba mpya ndugu yangu,ndo maana wazalendo wa ukweli wa nchi hii tunaona Haya mabadiriko ya mkuu ni usanii tu maana mabadiriko ya kweli ya nchi yetu yapo kwenye rasmi ya pili ya katiba mpya maarufu kama rasmu ya walioba
Magufuli anakazi hii nchi karibia kila MTU ni jipu kwa nafasi yake!!Itachukua miaka 50 nchi yetu kuwa waadirifu secta nyingi
 
Wakati mwingine watu wanalaumu kila mara ooh uzalendo..! Kwa mwendo huu kweli..! Inauma.
 
....
.....Hii inaitwa...eeeh tembeya taratibu mutoto umebeba mayayi
 
Du...hapo Ndio utakumbuka kauli ya nyerere...tunaka rais ambaye atamuonea haya MTU yoyote... Akivunja katiba ya nchi... Na rais analindwa na katiba.....hivyo kama rais anapambana....na kutetea nchi...aapambane na hao...mafisadi...wamedhurumu pesa za wananchi....nataka siku moja....wawajibiswe....rais kamata hao watu...mungu anatuona....mungu atakulinda......
 
Yan ktk hili magufuli ana kazi kubwa sana maana bado amezungukwa na wezi wakubwa ambao bado wapo ktk serikali yake
 
Jamani, tusijekuta hawa watu nguvu zao ni kubwa sana kiasi kwamba tukiwakamata na kuwashtaki nchi itayumba! Nimerejea tu baadhi ya hotuba za waziri mkuu mstaafu wakati akijibu maswali ya papo kwa papo.
Huenda Pinda aliona mbali zaidi yetu. Kama sivyo ni kwani vyombo vya dola vinanusa na kurudi nyuma kwa kasi?
Mwakyembe, tupelekee mswada wa sheria bungeni wa kuleta sheria ya kuwepo kwa wachunguzi, washtaki na waendesha mashtaka huru haraka binge lijalo ili mimi nikapeleleze, nishtaki na niendeshe kesi hii ya kudai pesa zangu zilizochukuliwa na MTU baki tu tena mwenye uraia wenye utata. Wizi huu haukubaliki kwani nchi hii ni yetu site siyo ya kikundi kidogo cha watu.
 
mOTO WA
print_icon.gif

SIRI kuu ya James Rugemalira, kumwaga mabilioni ya shilingi kwa baadhi ya majaji wa mahakama kuu, viongozi waandamizi serikalini na madhehebu ya kidini, wabunge na viogogo wa Ikulu, zimeanza kufumuka.

Nyaraka mikononi mwa gazeti hili zinaonesha zaidi ya asilimia 90 ya wale waliopewa fedha na Rugemalira, ni wale waliomsaidia “kufanikisha ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 324 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT) na kujinasua katika mikono ya sheria.”

“Rugemalira alishika kila mmoja. Kuanzia Ikulu ya Jakaya Kikwete, TAKUKURU, mahakama, BoT, hazina, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, viongozi wa madhehebu ya kidini na hata baadhi ya mawaziri wa zamani wenye ushawishi serikalini,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi kutoka Ikulu.

Amesema, “…fedha katika akaunti ya Escrow zilihusisha mtandao mpana ulioratibiwa na Rugemalira na Harbinder Sigh Seth (Singasinga).”

Majaji wa mahakama kuu, Aloycious Mujulizi na Eudeus Ruhangisa, ni miongoni mwa waliokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Rugemalira; na walikuwa washauri wake wakuu wa kisheria.

Mawasiliano kati ya Jaji Mujulizi na Jaji Ruhangisa yalifanyika kupitia kwa Rugemalira mwenywe na katika eneo jingine kupitia kwa mkewe, Benedicta.

Jaji Mujulizi na Jaji Ruhangisa walitajwa bungeni na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuwa miongoni mwa vigogo waliopewa mgawo wa fedha hizo na Rugemalira.

Bunge liliagiza majaji hao wachunguzwe na wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria.

Hadi sasa, hakuna taarifa zozote kuwa majaji walichunguzwa na kuchukuliwa hatua.

Rugemalira alikuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa katika kampuni ya kigeni ya IPTL kupitia kampuni yake ya VIP Engineering and Marketing Limited.

Jaji Mujulizi na Ruhangisa walilipwa na Rugemalira kila mmoja Sh. 404 milioni.

Mabilioni ya shilingi yaliyohifadhiwa katika akaunti ya Escrow yalikwapuliwa na Harbinder Sigh Seth, aliyejiita mmiliki wa IPTL kwa msaada mkubwa wa Rugemalira na kile kilichoitwa, “amri ya mahakama.”

Seth alidai kumiliki IPTL kupitia kampuni yake ya Pan African Power Tanzania Limited (PAP).

MwanaHALISI linaweza kuthibitisha kuwa kati ya tarehe 13 na 26 Novemba 2014, kilikuwa kipindi ambacho Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ilimhoji Rugemalira juu ya ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow.

Aidha, ni katika kipindi hichohicho, Rugemalira alikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Jaji Mujulizi na Ruhangisa.

Wengine waliokuwa na mawasiliano na Rugemalira katika kipindi hicho, ni waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo; aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Bernard Membe na aliyekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi.

Aliyepata kuwa waziri wa utawala bora, Mathias Chakawe; aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah; aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali (AG), Frederick Werema na aliyekuwa waziri wa viwanda na biashara, Dk. Abdallah Kigoda, walikuwa pia na mawasiliano na Rugelalira.

Wengine ni naibu gavana wa BoT, Dk. Enos Bukuku; aliyekuwa Mnikulu Mkuu wa Ikulu, Shaban Gurumo; aliyekuwa Kamishna mkuu mamlaka ya mapato (TRA), Rished Bade na aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati wa ujio wa IPTL nchini (1994), Andrew Chenge.

Orodha ya waliokuwa katika mawasiliano na Rugemalira inahusisha pia mawaziri wa zamani, Paul Kimiti na Wilson Masilingi; aliyekuwa mhariri mtendaji wa magazeti ya serikali – Daily News na Habari Leo – Gabriel Nderumaki; aliyewahi kuwa waziri wa nishati na madini, Wiliam Ngeleja na mkurugenzi wa kampuni ya G and S Consultancy Limited, Dk. Gideon Shoo.

Wengine ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Constantine Massawe; Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilain; Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa na aliyekuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Prof. Anna Tibaijuka.

Prof. Tibaijuka alikiri kupokea kiasi cha Sh. 1.6 bilioni kutoka kwa Rugemalira. Hata hivyo, alisema kuwa fedha ambazo alipokea zilikuwa ni mchango wa shule yake ya Barbro Johanssen ya jijini Dar es Salaam na Kajumulo Girls High School iliyoko Bukoba.

Kwa mujibu wa taarifa, Dk. Hoseah alimruhusu Rugemalira kutafuta msaada popote pale, ikiwa ni pamoja na nje ya nchi na kwamba ofisi yake “ingetoa maofisa kumsaidia.”

“Kama una jambo la msingi kufanya nje ya nchi, una baraka zangu zote. Watakapohitajika maofisa wa TAKUKURU kwa ufafanuzi, wako tayari kukusaidia pale uliko,” anaeleza Dk. Hoseah na Rugemalira andishi lake la 16 Novemba 2014.

Dk. Hoseah anamaliza kwa kumueleza Rugemalira, “…nakutakia kila la kheri.”

Rugemalira alikuwa anaomba TAKUKURU kuingilia kati kile kinachoitwa, “mgogoro wa hisa kati ya IPTL na Benki ya Standard Chartered (SCB) ya Uingereza.”

Hata hivyo, Rugemalira anaonywa na Masilingi, ambaye wakati huo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, kuwa mwangalifu na mtulivu wakati suala hilo linaendelea.

Alisema, “mimi nikiwa mwanasheria, ninakushauri wewe na kampuni yako kushirikiana kwa ukamilifu na TAKUKURU. Suala la IPTL ni gumu. Limekuwa na mchanganyiko mkubwa. Akili nyingine haziwezi kulielewa.”

Masilingi anasema, “…nimebaini kwamba TAKUKURU ndio wanaolichukulia suala hilo kwa usiri mkubwa katika hatua za uchunguzi na wenyewe wanaweza kukusaidia kupata hukumu iliyo ya haki.”

Benki ya Standard Chartered ilikuwa inadai na mpaka sasa bado inadai kuwa mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL na fedha zilizopo kwenye akaunti ya Escrow, ni mali yake.

Inadai kuwa kampuni ya MECHMAR ya Malasia ilishindwa kurejesha mkopo iliochukua benki na kwamba hilo ni jambo linalosababisha mitambo ya IPTL iliyopo Tegeta Salasala, jijini Dar es Salaam, kuwa mali yake.

Akihutubia taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, wiki tatu baada ya Bunge kuagiza waliohusika katika wizi wa fedha za Escrow wachukuliwe hatua, aliyekuwa Rais wa Jamhuri, Jakaya Mrisho Kikwete alikiri kuwapo udanganyifu katika kufikia utoaji wa fedha hizo.

Alikiri baadhi ya nyaraka kughushiwa. Akakiri kuwa kampuni ya PAP imekwepa kodi ya serikali na kudai kuwa serikali yake bado inaendelea kuitafuta kampuni ya MECHMAR iliyodaiwa kuuza asimia 70 ya hisa zake ndani ya IPTL.

Rais alikiri kuwa aliyepewa fedha na serikali – PAP – hakuwa na sifa; serikali yake haikufanya uchunguzi yakinifu kuhusu historia, uhalali, sifa na uwezo wa kampuni ya PAP katika uwekezaji wa umeme, ununuzi wa mitambo na mtaji.

Naye mwanasheria wa Rugemalira, Camilo Schutte, katika barua aliyomwandikia Rugemalira, anasema “…baada ya kusoma ushauri wa Masilingi juu ya msaada wa TAKUKURU, itakuwa busara kuomba TAKUKURU kusubiri hukumu kati ya Standard Chartered na IPTL.”

Anasema kampuni ya Rugemalira (VIP) “…inapaswa kuomba TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya sera ya benki ya Standard Chartered kuhusu ununuzi wa madeni ambayo mchakato wake unaweza kuwa na rushwa.”

Camilo Schutte anamueleza Rugemalira katika barua yake hiyo na ambayo imenakiriwa kwa majaji, mawaziri, kiongozi wa TAKUKURU, maofisa wa Ikulu na watu wengine kuwa, “…tatizo la benki ya Standard Chartered, kama zilivyo taasisi nyingine, ni kufanya biashara ili kujipatia faida kubwa.”

Akiandika kwa Dk. Gideon Shoo, mwanasheria wa Rugemalira (Camilo Schutte) anaelekeza kufanyika mambo matatu kwa haraka.

Kwanza kutafuta, kwa “gharama yoyote ile,” watu wote wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii ambao wanapigia kelele ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Miongoni mwa waliotajwa, ni Zitto Kabwe, mbunge wa sasa wa Kigoma Mjini; David Kafulila, ambaye alikuwa mbunge wa Kigoma Kusini; Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose; Wilson Masilingi na balozi wa Finland nchini.

Pili, Camilo Schutte anasema, ni sharti mtandao wao ujiridhishe ikiwa watu wanaolizungumzia jambo hilo wanalifahamu kwa undani au wanalijua nusunusu au hawalijui kabisa.

Kwa maoni ya mwanasheria wa Rugemalira, wabunge waliokuwa wameshupalia jambo hilo walikuwa hawana taarifa zozote muhimu kuhusu suala hilo.

Tatu, mwanasheria alimtaka Dk. Shoo kuangalia athari za taarifa zilizosambazwa juu ya ukwapuaji wa fedha hizo, kwa kampuni ya IPTL na Rugemalira binafsi.

“Baada ya kukamilisha haya, naomba unijulishe haraka ili tuweze kupanga mikakati ya kukabiliana na kila tatizo nililolitaja hapo juu,” anaeleza Camilo Schutte.

Kupatikana kwa mawasiliano haya kumekuja mwaka mmoja na nusu baada ya mabilioni ya shilingi kukwapuliwa BoT; na Bunge kuelekeza serikali kufanya uchunguzi.

Aidha, kupatikana kwa taarifa kuwa Rugemalira alikuwa na mawasiliano ya karibu na “kindungu” na mkuu wa TAKUKURU, kumekuja wakati ambapo taasisi hiyo imeshindwa kuanika orodha ya watu walionufaika na mgawo wa fedha hizo kutoka benki ya Stanbic.

Bunge liliagiza serikali kufikisha mahakamani watuhumiwa wote wa Escrow, ikiwa ni pamoja na kufilisi mtambo wa IPTL na kuitangaza benki ya Stanbic kuwa taasisi ya kutakatisha fedha.

Bunge liliagiza pia kuchunguza na kuwajibisha majaji waliotajwa kunufaika na mgawo wa fedha kupitia benki ya Mkombozi na kumfukuza nchini, anayejiita mmiliki wa IPTL, Harbinder Sigh Seth.

Akizungumzia kutajwa kwa Dk. Hoseah na baadhi ya majaji katika mawasiliano na Rugemalira, mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amesema jambo hilo linaongeza shaka juu ya uadilifu wa viongozi wa CCM na serikali yake.

Ameliambia gazeti hili katika mahojiano kwa njia ya simu, “…hili liserikali lote limeoza. Kuanzia Ikulu, mfumo wa mahakama hadi viongozi wa madhehebu ya kidini; kote kumejaa rushwa.”

Lissua ameongeza, “Tulisema ndani ya Bunge, kwamba majaji wamehongwa na hivyo tukataka wachunguzwe, lakini serikali ya CCM imegoma kwa kuwa walioiba waliwajua na walishirikiana nao.”

Mwanasiasa huyo wa upinzani anasema, “utapeli huu ulifanywa na serikali ya Rais Kikwete, BoT, Benki ya Stanbic na PAP.”

Amesema, “…sasa kama kweli wanataka kusafisha nchi, basi waanzie hapo. Siyo kukimbizana na vidagaa. Waanze na maofisa wao wa Ikulu waliokuwa wameigeuza ofisi ya umma kuwa ofisi binafsi.”


Chanzo: MwanaHalisi
MOTO WA ESCROW JPM HAUWEZI
escrow JPM
 
Sakata la Escrow laielemea Tanesco

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

UAMUZI wa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICSID), kulitaka Shirila la Umeme Tanzania (Tanesco) kuilipa Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) Dola za Marekani milioni 148.4 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 320 imelielemea shirika hilo.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa imeibua upya mgogoro wa kisheria kati ya Tanesco dhidi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kupitia uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kuzidiwa huko kwa Tanesco kunatokana na kauli ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kurusha mpira kwa Tanesco, huku akisema shirika hilo ndilo lenye kesi na wanatakiwa kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu sakata hilo.

Kutokana na uamuzi huo MTANZANIA ilimtafuta Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba ambaye yupo mkoani Kagera katika ziara yake ya kuangalia athari za tetemeko la ardhi ambaye hakupokea simu wala kujibu ujumbe mfupi wa simu aliotumiwa.

Taarifa kutoka ndani ya Tanesco zinaeleza kwamba timu ya wanasheria wa shirika hilo wamekuwa katika vikao vizito kujadili suala hilo.

“Si hao pia wapo wanasheria nguli pamoja na wale wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanajadili suala hilo na namna ya kuliendea. Ila naamini baada ya kukamilika kwa kikao chao dira inaweza kupatikana.

“Ila ninachotaka kukuambia suala hili ni zito kwetu na hakuna namna nyingine zaidi ya kujiandaa kwa wanasheria wa Tanesco pamoja na wale wa wizara kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu,” alisema mtoa habari wetu.

Uamuzi wa benki hiyo kulipwa ulitolewa wiki iliyopita na mahakama hiyo, ambapo Tanesco imetakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha ambacho kinajumuisha riba ya deni la tozo ya uwekezaji.

Suala hilo limeibuka ikiwa imepita miaka mitatu tangu Serikali kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kuruhusu kufanyika kwa malipo ya Dola za Marekani milioni 200 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 300 kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Fedha hizo zilitolewa na kwenda kwa Kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) kwenda kwa mmiliki wake, Harbindar Singh Sethi mwenye makazi yake hapa nchini na Afrika Kusini.

Katika kesi hiyo Tanesco ilikuwa inawakilishwa na mawakili wa kampuni za R.K Rweyongeza & Advocates na Crax Law Partners.

Prof. Muhongo bungeni

Novemba 27, mwaka 2014, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alijibu hoja ndani ya Bunge la 10 na kusema kuwa mjadala wa Escrow, mengi yalisemwa huku akishukuru uchunguzi wa CAG, TAKUKURU.

Alisema miaka ya 90 nchi ilikuwa na upungufu wa umeme kutokana na upungufu wa maji kwenye mabwawa, ambapo 1994 serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa IPTL ilikuwa iliyokuwa ikimilikiwa na VIP ya Tanzania iliyokuwa na asilimia 30 na Mechmar ya Malaysia yenye asilimia 70.

Alisema Tanesco na IPTL walisainiana mkataba wa miaka 20, hata hivyo uzalishaji haukuanza mara moja kutokana na mgogoro ulioibuka baina yao (Tanesco na IPTL) .

Mwaka 2002 IPTL ilianza kuzalisha umeme na mkataba ukaanza kuhasabiwa hapo, lakini kutokana na mgogoro ikafunguliwa akaunti ya Escrow na mwaka 2004 Tanesco ilifungua shauri kupinga tozo la Capacity Charge

“Taarifa hiyo sio kweli kwani Tanesco haijawahi kufungua kesi yoyote dhidi ya Standard Charted kama ilivyosemwa na PAC. Kesi hiyo ilifunguliwa na Standard charted na ilikuwa haihusu capacity charge.

“Uwiano wa mtaji ni 70 kwa 30 na uamuzi haujabadilishwa na mahakama yoyote. Mwaka 2004 Kampuni ya Mkono & CO advocates iliishauri Tanesco iendelee kupinga Capacity Charge London. Hata hivyo, Tanesco haikuishauri Tanesco kufungua kesi Tanzania wala mahakama ya Kimataifa.

“Hadi 2013 Jaji Utamwa anatoa hukumu ya mgogoro wa wanahisa wa IPTL kulikuwa hamna kesi yoyote kuhusu tozo ya IPTL,” alisema Profesa Muhongo ndani ya Bunge.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa Serikali ilichukua tahadhari zote ambapo kwa mujibu wa kinga IPTL itawajibika yakitokea madai yoyote na ilipitiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Inaelezwa kuwa Agosti 2005, benki ya SCB-HK ilinunua kwa bei yapunguzo ya dola za Marekani 76.1 kutoka Benki ya Malaysia ya Danaharta baada ya kushindwa kurejesha deni la muda mrefu kutoka IPTL.

Bei halisi ya deni hilo ilikuwa ni dola milioni 101.7 kwa mujibu wa ushahidi uliopo ambapo IPTL ilikopa dola milioni 100 mwaka 1998 kutoka kwa ubia wa mabenki ya Malaysia ili kujenga mtambo wa kufua umeme wa megawati 100 wa Tegeta.

Chini ya makubaliano hayo SCB-HK ilipewa kandarasi kadhaa ikiwemo haki ya kulipwa deni la 1997, ambapo mkataba wa utekelezaji na hatia ya makubaliano ya dhamana iliyosainiwa na kati ya IPTL na Serikali.

SOURCE: Mtanzania
 
Uko sahihi, tena ikihusisha hata benki inajidai ya kanisa. Mkombozi. Wanajidai kuhubiri amani wakati ni walafi wa pesa na inavyoonekana ukabila pia ulitumika.

Mnaingiza udini sasa, ina maana mkombozi haina Wateja Wa dini nyingine? Ishu ni kwamba serikali lazima itoe huo mzigo iwape wenye nazo! Nyie wabongo mna mambo, fanyeni kazi majungu punguzeni, huyo mzee RUGEMARILA namfahamu fikaa, ni mtu anaependa kujituma tangu akiwa BOT! Acheni story za mtaani!
 
Back
Top Bottom