Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Kuna watu wanafundisha kwamba jina jingine la Yesu ni Nabii Isa. Ukweli ni kwamba kuna tofauti kubwa kati ya Yesu Kristo na Nabii Isa.
Yesu Kristo ana sifa kuu zifuatazo:
Ni Mwana wa Mungu na pia ni Mungu.
Katika Mt 16:15-17 – Yesu alimwuliza Petro, "Nanyi mwanisema mimi kuwa ni nani?" Petro akajibu, "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai." Yesu alimpongeza kwa kuujua ukweli huo, akamwambia kuwa amefunuliwa na Baba wa mbinguni.
Asiyeamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu hana uzima
Yohana 3:36
"Amwaminiye Mwana anao uzima wa milele; asiye mwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia."
1 Yohana 2:23
"Kila amkanaye Mwana, hana Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia."
Yesu alisulibiwa, alikufa msalabani na kufufuka siku ya tatu ili sisi tupate wokovu.
Ili mtu apate wokovu ni lazima akiri kama ilivyoandikwa katika
Warumi 10:9
"Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka."
Yesu Kristo ni Alfa na Omega; ni wa milele.
Katika Ufunuo 22:13 – Yesu anasema, "Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho." Hakuna nabii yeyote anayeweza kusema maneno hayo.
Yesu Kristo ana mamlaka ya kusamehe dhambi
Katika Marko 2:5-7 – Yesu alimwambia mtu aliyepooza, "Mwanangu, umesamehewa dhambi zako." Mafarisayo walishangaa, wakisema, "Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?"
Katika Ufunuo 19:16 – Yesu anaitwa Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, hadhi ambayo manabii wa kawaida hawakuwa nayo.
Wanaosema kwamba Yesu ni Nabii Isa, waulize: je, wanakubaliana na sifa hizo za Yesu? Watakujibu kwamba Nabii Isa sio Mwana wa Mungu...
Kwahiyo kama wewe ni Mkristo unayeongozwa na Maandiko ya Biblia, usimwite Yesu kwa jina la Isa, kwa sababu majina hayo mawili hayana maana sawa.
Nimekufunulia siri hiyo, usidanganyike tena!