Siri Imefichuka! Yesu Kristo sio Nabii Isa

Siri Imefichuka! Yesu Kristo sio Nabii Isa

Status
Not open for further replies.
Kuna watu wanafundisha kwamba jina jingine la Yesu ni Nabii Isa. Ukweli ni kwamba kuna tofauti kubwa kati ya Yesu Kristo na Nabii Isa.

Yesu Kristo ana sifa kuu zifuatazo:

Ni Mwana wa Mungu na pia ni Mungu.
Katika Mt 16:15-17 – Yesu alimwuliza Petro, "Nanyi mwanisema mimi kuwa ni nani?" Petro akajibu, "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai." Yesu alimpongeza kwa kuujua ukweli huo, akamwambia kuwa amefunuliwa na Baba wa mbinguni.

Asiyeamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu hana uzima
Yohana 3:36
"Amwaminiye Mwana anao uzima wa milele; asiye mwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia."

1 Yohana 2:23
"Kila amkanaye Mwana, hana Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia."

Yesu alisulibiwa, alikufa msalabani na kufufuka siku ya tatu ili sisi tupate wokovu.
Ili mtu apate wokovu ni lazima akiri kama ilivyoandikwa katika
Warumi 10:9
"Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka."

Yesu Kristo ni Alfa na Omega; ni wa milele.
Katika Ufunuo 22:13 – Yesu anasema, "Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho." Hakuna nabii yeyote anayeweza kusema maneno hayo.

Yesu Kristo ana mamlaka ya kusamehe dhambi
Katika Marko 2:5-7 – Yesu alimwambia mtu aliyepooza, "Mwanangu, umesamehewa dhambi zako." Mafarisayo walishangaa, wakisema, "Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?"

Katika Ufunuo 19:16 – Yesu anaitwa Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, hadhi ambayo manabii wa kawaida hawakuwa nayo.

Wanaosema kwamba Yesu ni Nabii Isa, waulize: je, wanakubaliana na sifa hizo za Yesu? Watakujibu kwamba Nabii Isa sio Mwana wa Mungu...

Kwahiyo kama wewe ni Mkristo unayeongozwa na Maandiko ya Biblia, usimwite Yesu kwa jina la Isa, kwa sababu majina hayo mawili hayana maana sawa.

Nimekufunulia siri hiyo, usidanganyike tena!
Haikuwa Siri, huu ni ukweli uko wazi kwa zaidi ya miaka 2000 Sasa.
Hiyo Siri aliificha Nani Hadi wewe leo useme Siri imefichuka?
 
Unajua kwa kituruki Yesu anaitwaje?
Wakristo wanaoishi uturuki wanamuita Issa kama ambavyo sisi tunamuita Yesu jina lilitoholewa toka kwenye English Bible Jesus. Kihaulisia ilitakiwa aitwe Yeshua kama ambavyo inatamkwa kwa kiebrania.

Labda tunaweza kusema kwa sisi wakristo kimaandiko Yesu si nabii ni mpakwa mafuta/ mteule wa Mungu aliyepewa mamlaka ya juu zaidi kuliko viumbe wote.
 
Everyone loves Jesus until you define who he is.
 
Hata huyo Yesu wa biblia bado hata hao wakristo wanatofautiana baadhi ya mambo kuhusu huyo Yesu wa biblia, si kwamba wakristo wote wanamtambua na kuamini sawa kuhusu Yesu kuna utofauti.
Naomba kujifunza, weka hizo tofauti?
 
Waturuki wakristo wanatumia jina la Isa kumuita Yesu.
Hakuna kitu kama hicho kaka, Uturuki na Ugiriki ndio mataifa ya kwanza kwanza kuupata Ukristo, in fact makanisa yanayo tajwa na Paulo kama Wakoritho, Thessaloniki, Wagalatia, Efeso yalikua maeneo hayo hayo na hata neno WAKRISTO lilianza kutumika kwenye moja ya miji yao, Antokia. Nabii Issa limeanza kutumika karne 7 baada ya Ukristo kuwepo duniani
 
Ndiyo, kwa kituruki Yesu ni "İsa"
Lakini hiyo ni tafsiri tu ya jina "Yesu" kwa lugha hiyo, linalotokana na lugha za Kiarabu.

Waturuki wengi Wakristo wanapotumia “İsa Mesih” wana maanisha Yesu Kristo, sio “Nabii Isa” wa imani ya Kiislamu.

Na Waislamu wa Kituruki wakisema “İsa,” wana maana ya “Nabii Isa” wa Qur'an.

Nabii Isa katika Uislamu sio sawa na Yesu Kristo katika Ukristo — wanafanana katika baadhi ya mambo ya kihistoria (kama kuzaliwa na Mariamu), lakini tofauti zao za msingi ni kubwa sana kiimani.

Yesu Kristo ni zaidi ya Nabii kwa Wakristo
“Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16)
Point ni kwamba anayekusudiwa ndio huyo huyo mmoja kwa maana hakuna ushahidi kwamba aliwahi kuwepo Yesu na akawepo Isa, maana hata hao wakristo wenyewe hutofautiana kuhusu Yesu na ndio hutumia hiyo hiyo biblia.
 
Sasa maelezo yote ya nini hayo? Yesu alizaliwa kwenye holi la ng'ombe. Nabii Issa alizaliwa chini ya mtende! Si tiyari hao ni watu wawili tofauti?
Upo ushahidi kwamba kuliwahi kuwepo Yesu na Isa kwa wakati mmoja?
 
Hakuna kitu kama hicho kaka, Uturuki na Ugiriki ndio mataifa ya kwanza kwanza kuupata Ukristo, in fact makanisa yanayo tajwa na Paulo kama Wakoritho, Thessaloniki, Wagalatia, Efeso yalikua maeneo hayo hayo na hata neno WAKRISTO lilianza kutumika kwenye moja ya miji yao, Antokia. Nabii Issa limeanza kutumika karne 7 baada ya Ukristo kuwepo duniani
Kwahiyo Waturuki wakristo wanamuita Yesu kwa jina gani?
 
Kuongezea hapo mahali alipozaliqa Yesu na Nabii issa ni sehem mbili tofauti kwa hyo haiwezekani.mtu mmoja akazaliwa sehem mbili tofauti Yesu kwenye holi la ng'ombe na Nabii Issa chini ya mtende.
Ni kweli haiwezekani mtu mmoja kuzaliwa sehemu mbili tofauti ila inawezekana kuwepo maelezo mengi tofauti yenye kuelezea kitu kimoja.
 
Hizi dini nyengine sijui zina lengo gani!? majamaa wamekopy kila kitu kwenye bible kisha wamechenji kidogo story ionekane hawajacopy. Yesu na isa ni characters wawili tofauti sababu wamezaliwa sehemu tofauti na mmoja alikufa akafufuka mwengine wa upande wa pili hakufa!

Ukija kwenye uhalisia, Kwenye mapepo ukitaja jina YESU yatapepesuka na kuchapa mwendo hatari! Ila yatajie jina la isa! Jibu unalo.

YESU NI JINA LIPITALO MAJINA YOTE!.
YESU NI NI JINA LINALOISHI!.
Ndio maana nasema mara zote kuwa Yesu ana majina mengi najiuliza ni jina lipi hilo ambalo ndio lenye kutoa mapepo? Kwanini ukitamka Isa mapepo yasitoke wakati wakristo wa wakituruki huko wanamuita Yesu kwa jina la Isa?

Nadhani mlitakiwa mseme majina ya Yesu yanatoa mapepo maana kuna majina mengi ambayo mengine hujawahi hata kuyasikia.
 
Wakristo wanaoishi uturuki wanamuita Issa kama ambavyo sisi tunamuita Yesu jina lilitoholewa toka kwenye English Bible Jesus. Kihaulisia ilitakiwa aitwe Yeshua kama ambavyo inatamkwa kwa kiebrania.

Labda tunaweza kusema kwa sisi wakristo kimaandiko Yesu si nabii ni mpakwa mafuta/ mteule wa Mungu aliyepewa mamlaka ya juu zaidi kuliko viumbe wote.
Sasa inawezakana vp tafsiri ya jina ikaweza kutenda miujiza na kutoa mapepo?
 
Kuna watu wanafundisha kwamba jina jingine la Yesu ni Nabii Isa. Ukweli ni kwamba kuna tofauti kubwa kati ya Yesu Kristo na Nabii Isa.

Yesu Kristo ana sifa kuu zifuatazo:

Ni Mwana wa Mungu na pia ni Mungu.
Katika Mt 16:15-17 – Yesu alimwuliza Petro, "Nanyi mwanisema mimi kuwa ni nani?" Petro akajibu, "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai." Yesu alimpongeza kwa kuujua ukweli huo, akamwambia kuwa amefunuliwa na Baba wa mbinguni.

Asiyeamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu hana uzima
Yohana 3:36
"Amwaminiye Mwana anao uzima wa milele; asiye mwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia."

1 Yohana 2:23
"Kila amkanaye Mwana, hana Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia."

Yesu alisulibiwa, alikufa msalabani na kufufuka siku ya tatu ili sisi tupate wokovu.
Ili mtu apate wokovu ni lazima akiri kama ilivyoandikwa katika
Warumi 10:9
"Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka."

Yesu Kristo ni Alfa na Omega; ni wa milele.
Katika Ufunuo 22:13 – Yesu anasema, "Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho." Hakuna nabii yeyote anayeweza kusema maneno hayo.

Yesu Kristo ana mamlaka ya kusamehe dhambi
Katika Marko 2:5-7 – Yesu alimwambia mtu aliyepooza, "Mwanangu, umesamehewa dhambi zako." Mafarisayo walishangaa, wakisema, "Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?"

Katika Ufunuo 19:16 – Yesu anaitwa Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, hadhi ambayo manabii wa kawaida hawakuwa nayo.

Wanaosema kwamba Yesu ni Nabii Isa, waulize: je, wanakubaliana na sifa hizo za Yesu? Watakujibu kwamba Nabii Isa sio Mwana wa Mungu...

Kwahiyo kama wewe ni Mkristo unayeongozwa na Maandiko ya Biblia, usimwite Yesu kwa jina la Isa, kwa sababu majina hayo mawili hayana maana sawa.

Nimekufunulia siri hiyo, usidanganyike tena!
Haya ila kabla ya yote tukubaliane kwamba mungu ni mmoja hakuzaa wala hakuzaliwa
Na kwamba yesu siyo mungu ndio tuendelee
Na kule israel mnaposema ndio ndugu zenu ukisema yesu ni mungu ni kosa la jinai
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom