Chamoto
JF-Expert Member
- Dec 7, 2007
- 8,342
- 17,599
Naomba nikujibu hoja zako kama ifuatavyo:
- Huyo babu anatumiwa tu na shetani. Nguvu za giza zikiondoka ndani yake atakuwa mtu "normal" tena atashangaa kwanini alikuwa anapoteza muda wake kugawa vikombe. * Tunachofanya sasa ni kupambana na roho hiyo inayotenda kazi ndani ya babu. Na hiyo roho ya shetani itashindwa tu kwa Jina la Yesu. Time will tell.
- Agizo la kuponya liliishatolewa na Yesu mara moja(Mathayo 10:1) na halitarudiwa kutolewa tena kwa ndoto wala kwa maono. Na agizo hilo ni la kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Mungu hana kigeugeu(Malaki 3:6) Aliyesema ponyeni magonjwa yote hawezi leo kubadilisha kauli yake na kusema ponya magonjwa manne tu. HA-TU-DA-NGA-NYI-KI!!
- Agizo la kuponya linaenda sambamba na agizo la kuhubiri Injili(na kuanzisha makanisa - Marko 16:15-18). Anayesema ametumwa kuponya tu, Mungu amsamehe kwa kuwa hajui alisemalo wala alitendalo.
- Yesu aliwaambia waliopona ukoma waende wakajionyeshe kwa makuhani. Hao waliopona kwa babu nao waende wakajionyeshe kwa madaktari(wapimwe) na ukweli ujulikane maana Waongo ni wengi na wachakachuaji ni wengi.
- Wanaosema watu wanapona kwa babu kwa imani hawajui hata maandiko yanasema nini juu ya imani. Imani huja kwa kulisikia Neno la Kristo(Warumi 10:17). Kama babu anataka tuamini anachokisema, ni lazima ahubiri Neno la Kristo. Watumishi wa Mungu(Mitume: Paulo, Petro...walihubiri Injili na kuwaombea watu). walifanya yote. Yesu alihubiri Injili na kuponya. Alifanya yote. Waganga wa kienyeji ndio wanaofanya moja tu "kuponya" na uponyaji wao ni feki. Shetani ataumbuka tu. Roho Mtakatifu yupo kazini kutujulisha kweli yote nayo kweli itatuweka huru.
Mungu akubariki ndugu, hayo uliyosema ni kweli kabisa yanayo tokea kwa babu hayaendani kabisa na maandiko. kwani tunatakiwa kuutafuta ufalme wake kwanza halafu mengine yote tutazidishiwa. kwa maneno mengine tuponye roho zetu kwanza halafu ndiyo tuponye miili.
Naelewa kuwa kweli itapingwa kwa nguvu zote hapa kwasabubu hiyo ni kazi ya yule mwovu kufanya hivyo kuzuia ukweli. Yeye ni mwongo toka mwanzo na ni baba wa uongo.
Mungu akubariki sana.