Siri Imefichuka! Babu wa Loliondo ametumwa na Shetani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri Imefichuka! Babu wa Loliondo ametumwa na Shetani

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by mediaman, Mar 20, 2011.

 1. mediaman

  mediaman Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio kweli kwamba Babu wa Loliondo ametumwa na Mungu kutumia dawa hiyo kuwaponya watu. Huyo Babu ametumwa na "mungu wa dunia hii(shetani) ili kuwadanganya watu waache kumtumaini na kumwamini Mungu wa kweli ili hatimaye waangamie siku ile ya mwisho. Soma 2 Wakorintho 4:4 na kisha tafakari kwa makini hoja zifuatazo utathibitisha ukweli huo.
  Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu. Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
  Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
  Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
  Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
  Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
  Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
  Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
  Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
  Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
  Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
  Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?

  Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
  Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
  Jamani Watanzania "Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo"
  Siri imefichuka! Hoja hizo na maandiko hayo ya Biblia yanathibitisha wazi kwamba huyo Babu hajatumwa na Mungu. Ila ni shetani anamtumia kuwadanganya watu. Tusikubali kudanganywa. Hata waganga na wachawi wa leo na wao huwaambia wateja wao kwamba wanaponya au kufanya miujiza kwa uweza wa mungu. I dare to talk openly Huyo mungu wanayemtaja ni mungu wa dunia hii (shetani). Mwenye masikio na asikie.
   
 2. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo la kukariri maandiko bila kuchanganua maana yake ndiyo imekupelekea kuandika UPUPU HUU!
  Unaonekana kabisa una matatizo ya akili, nakushauri ukanywe kikombe cha babu ndio utapata ufahamu wa kuandika maada yako kwa usahihi.
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  mods please delete this therad
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Utakufa na kijba cha Roho yako baba, babu we endelea na tiba jinsi mungu alivyokufunulia, inaonekana maandiko ya kwenye biblia yanatafsiriwa kila mtu kivyake, isije ikawa wewe ndo umetumwa na sh........ utuzuge km wewe haikufai kaa kimyaaaaaaa
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hata kiwembe ni shetani ... ukitumia vibaya kinakukata .... kama umekunywa dawa ile kwa imani za kishetani itakuponya kishetani shetani .... yawezekana wewe ni cashier wa shetani
   
 6. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Siri yenyewe iliyofichuka ipo wapi sasa??
  Kama huna cha kupost ni bora usome comments za wenzako tu...this iz ''Holy Crap''
   
 7. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kwa nini waifute?

  una maana kila thread usiyoipenda ifutwe?

  !!!!!!!!!
   
 8. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Tatizo la kusoma biblia kama novo! Kaisome tena...otherwise crap
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,819
  Likes Received: 10,108
  Trophy Points: 280
  Kama ni mwenye dhamboi sijui, kama ni wa shetani au mungu sijui, ila nalikua kipofu na mimi sasa naona, the rest are details,
   
 10. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wewe unayeyafahamu maandiko vizuri yufafanulie sasa, sio kuponda tu na huleti wazo lolote la maana
   
 11. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ha ha haaaa, yaani huyu mu**ni kazama jamvini kuja kumshambulia babu tu:lol::lol:, huyu sio 'ka-toetoise' kweli??? Haya mambo ya imani magumu sana, ni kama vile mimi nisivoweza kwenda huko hata bure lakini siwezi kuwakataza wengine wenye imani zao kwenda....
   
 12. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyu lazima either atakuwa ka-tortoise mwenyewe au mfuasi wake tu.... sababu hii thread yote ame-quote aliyosema huyo mkuu :lol:!!!!
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Elli

  umesema ipasavyo ... busara na ufikiri makini ni maneno machache kama uliyoandika na siyo mlolongo wa longo longo
   
 14. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  hiyo siri iko wapi? kama huu sio wehu ni nini? Hiyo bible mnaisoma kukariri kama kasuku tuuu ? Hamjui lazima mfundishwe na wataalam? Bravo Babu
   
 15. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Umejisajili LEO! wewe lazima utakua member ukaamua kuja kivingine.
  kama kweli unajiamini ungekuja na ID yako ya zamani.
  wasi wasi wangi unamponda babu na ID moja huku ukimsifia na nyingine.
   
 16. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mtoa mada amejiunga tarehe 20th March 2011.

  Labda yeye katumwa na Mungu kuja kuwahabarisha wanaJF.
  Ila habari za Loliondo zimezidi sasa, can't we talk about other issues?
   
 17. m

  mareche JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wajameni napita tu nitarudi badaye
   
 18. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mediaman
  Join Date : 20th March 2011

  Posts : 4
  Thanks 0
  Thanked 1 Time in 1
  Post
  Rep Power : 0
  Nadhani umejiunga ili umshambulie babu, shetani anaponya watu ili iwaje waendelee kumuasi au wamtukuze Mungu? Kila dakika iendayo kwa Mungu shetani anaombea watu wafe halafu leo awaponye ili wakemee mapepo tena mkuu, waangamize silaha zake?!
  Halafu acha kumtukuza Ibilisi wewe? Mbona makanisani watu wameombewa mpaka lakini bado hali ni ile ile, na kama ni roho ya shetani fungeni mkemee ili Mungu amuumbue mtumishi feki vinginevyo wewe ndiyo utakuwa mtumshi feki unasumbuliwa na wivu wa kihuduma!
  Nyie wenyewe kila kukicha kunyoosheana vidole mara fulani ni mtume feki mara anatumia nguvu fulani yaani ili watu wachanganyikiwe.
  Duuuuh kweli njia iendayo uzimani ni nyembamba sana.
   
 19. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  WanaJf, huyu jamaa kaingia leoleo humu na kaanza na hii post ya kumponda babu...inawezekana ni kati ya hawa maaskofu wanaompinga babu na ameona sehemu ya kuuguza machungu yake ya kukimbiwa na waumini ni hapa kweny jamvi la JF. Anaamini kuwa labda mawazo yake yatafika mbali zaidi kama akiyapitishia JF na aliamini kuwa atapata support kubwa katika hili...imekuwa vinginevyo maana kila mtu anaona thread yake kama CRAP!!! Pole sana askofu unayetapatapa.....siyo makosa ya babu...labda ni makosa ya Mungu! lkn kumbuka kuwa kazi ya Mungu haina makosa...sasa sijui umlaumu nani kwa ujio wa huyu babu!!!
   
 20. S

  SeanJR Member

  #20
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli siri imejulikana kwamba wewe mediaman na babako shetani mna mkakati wakupotosha jamii kwa kukariri baadhi ya mistari,Jesus aliponya hata kwa tope na kwa neno! Unavyosema hakutumia gome la mti,em' soma Ezekiel 47:12 na kama haitoshi soma ufunuo 22:2!!
   
Loading...