Mambo ya Kuepuka Mwaka 2024

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Sio kila Neno ambalo unaambiwa na Mtumishi au rafiki yako limetoka Kwa Mungu

Utangulizi
Watu wengi duniani Kwa sababu ya kusikiliza maneno ya watu wamepoteza kesho Yao na wengine wamepoteza Maisha Yao kabsa

Sio kwamba kusikiliza ushauri wa watu ni Vibaya , hapana sio kila ushauri unaopokea kutoka kwa watu umetoka Kwa Mungu

Chunga Sana pale unapotaka kufanya maamuzi yanayoweza kubadili atima ya Maisha yako Kwa kusikiliza Maisha ya watu

Wana waisraeli walishindwa kwenda kanaani Yao Kwa sababu walisikiliza maneno ya wale wapelelezi 10.

Kuna watu wameuza nyumba, kuolewa na watu ambao sio sahihi nk Kwa sababu ya ushauri wa watu ambao haukutoka Kwa Mungu

Unapokuwa na Jambo ambalo unatamani Mungu akufanyie unapata kuwashirikisha watu wengi juu ya Jambo lako na wengine wazuri na wengine sio wazuri hata kama ni marafiki zako

Yesu akiwa amekaa na wanafunzi wake anawashirikisha habari za kuteswa kwakwe na kufakwake na kufufuka , katikati ya wanafunzi wake anajitokeza Petro kupinga maneno ya Mungu juu ya Yesu

Kitu ambacho Yesu alifanya ambacho unatakiwa ujue Yesu alijua ushauri aliotoa Petro haukutoka Kwa Mungu ndio maana alimkemea shetani ?

Ulishawai kujiuliza Ayo maneno uliyoambiwa na Mtumishi au rafiki yako wakaribu kama ni ya Mungu au sio?

Biblia inasema watu wangu wana hangamia Kwa kukosa maarifa? Sio kila maarifa ni ya Mungu ndio maana biblia imeweka taadhari ya kuyachunguza maandiko

Ulishawai kujiuliza unakwenda Kwa Mtumishi anakwambia mume au mke ambaye umetunga naye ndoa miaka 10 na Zaid kwamba sio mpango wa Mungu?

Leo kuna watu Kwa sababu ya maneno ya watu wamearibu ndoa Zao, wameharibu kazi Zao , hata kuharibu Maisha Yao , kutokana na maneno ambayo siyo ya Mungu

Biblia imetupa kibali ya kuyapima maneno ambayo tunaambiwa Kwa neno ,Ile Kwamba neno ambalo umeambiwa na Mtumishi liko kwenye biblia ni la kwako Kwa wakati huo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom