Siri ambayo wanaume wengi hawaijui kuhusu wanawake

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,132
Habari!

Kuna mambo hayabadiliki na hayataweza kubadilika karne na karne. Labda binadamu sisi tuliopo tuondoke duniani na kuja kizazi kingine.

Jambo ambalo wanaume wengi hawalijui ni kwamba " wanaume hawachepuki, hawacheat na hawapaswi kusalitiwa na mwanamke"
Suala la mwanaume kuwa na mke au mpenzi mmoja ni maamuzi yake binafsi ambayo yatachochewa na aina ya elimu aliyonayo, dini au utamaduni wake.

Ila ikitokea mwanaume ameamua kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja basi ijulikane kuwa hakuna mwanamke mwenye mamlaka ya kumkaripia au kumshitaki kwa uamuzi wake huo.

Na ikitokea wewe mwanaume umeingia kwenye mgogoro wa kifamilia eti kisa una mchepuko sijui, sijui umeoa mke wa pili basi wewe mwanaume ni dhaifu, dhaifu, dhaifu wa kiwango cha kimataifa.

Karibu mila na tamaduni zote duniani zinampa nguvu mwanaume ya kumiliki mwanamkee zaidi ya mmoja. Dini karibu zote zinampa mamlaka mwanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja.

Nyuma ya shilingi. Mwanamke hapaswi kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja. Na ikitokea umepata viashiria vya usaliti huyo ni wa kumfukuza within a minute.

Huu wivu ambao wadada wanauonyesha ni fake na wanatuigizia. Hakuna uchungu mwanamke anaupata anapojua kuwa umekunywa maji ugenini.
 
Kwa nini unasema kwamba hakuna uchungu mwanamke anaupata pindi anapogundua kuwa kasalitiwa? kwani yeye hana moyo? uchungu unaoupata wewe pindi unapogundua kuwa mwanamke amekusaliti na yeye ndio huohuo hupata pindi anapogundua kuwa umemsaliti.

Tena wengine hulia tu bila kusema lolote kwa waume zao, huishia kuumia ndani kwa ndani na ogopa sana kumuumiza mwanamke siku akiamua kukuumiza na wewe ni hatari sana na hasa pale upendo wa mwanzo unapokuwa umeisha kabisa.
 
Huo ni mfumo dume, kuna mambo mengine lzma uwe analytical, don't generalise wanaume tuko tofauti sana kiuwezo kiakili na kifedha.
Kwanza nikuweke sawa.hakuna mfumo dume duniani bali hiyo inaitwa kanuni ya kimaumbile ..imagine mwanamke anaishi na wanaume wanne ndani !! Hiyo itakuwa nini kama sio unyanyasaji??

Kuwekewa mke zaidi ya mmoja kwa mwanaume ni sahihi kabisa mana imelindwa heshima ya mke .sema tu watu wana vichwa vigumu hawaelewi.
 
Kwanza nikuweke sawa.hakuna mfumo dume duniani bali hiyo inaitwa kanuni ya kimaumbile ..imagine mwanamke anaishi na wanaume wanne ndani !! Hiyo itakuwa nini kama sio unyanyasaji?? Kuwekewa mke zaidi ya mmoja kwa mwanaume ni sahihi kabisa mana imelindwa heshima ya mke .sema tu watu wana vichwa vigumu hawaelewi.
Hawawezi kupingana na asili.

Aliyewaletea hizi dini Yakobo, Daudi, Suleiman n.k walikuwa na wanawake zaidi ya mmoja.

Ila sasa tunaambiwa mke ni mmoja. Source utasikia barua ya Paul kwa TIMOTHEO.
 
Back
Top Bottom