Sipendi mke wangu atumie mitandao ya kijamii

Sipendi mke wangu atumie mitandao ya kijamii

Ndiyo nalijua hilo ila kwanini wanaume hayo mamlaka mliyopewa juu ya wanawake mnayatumia vibaya? Badala ya kutumia mamlaka yenu kuwalinda na kuwatetea mnayatumia kuwaonea na kuwasaliti vitu ambavyo ni dhambi je Mungu ndivyo alivyotaka hivyo?
itakuwa baadhi yetu na sio wote , ninachoamini ni kwamba miongoni mwenu mmekua na tabia ya kutaka kupambana na mwanaume. mwanaume hanuniwi.
 
Yani nasema kiukweli toka moyoni sipendi mke wangu atumie mitandao ya kijamii.

Hata kama mimi mwenyewe natumia na anajua natumia lakini yeye sipendi nimuone anatumia hiyo mitandao.

Najua wapo watakaoniona natumia mfumo dume potelea mbali na wala sijali.
Kwahiyo hatumii sababu wewe hupendi?

Wanawake wa hivi ni wakuchapwa viboko na kaka zao.

Hivi inakuaje mtu anaruhusu mtu mwingine amfanyie maamuzi ili hali yeye ni mtu mzima?
 
Mfumo dume uliwahifadhi watu wa zamani katika ndoa zao, mfumo dume uliweka heshima katika ndoa kwa muda mrefu, mfumo dume ndo ambao tumeumbwa nao, mfumo dume ndo mfumo sahihi.... vinginevyo ndo unakuta mwanaume anatawaliwa katika ndoa na kisha hiyo ndoa yenyewe haidumu. Ni jambo zuri sana kumfanya mkeo awe utakavyo wewe mana wewe ndo kiongozi wake.
uko sahihi mkuu
 
1.Unahofia nini?..

2.Utamnyima miaka yote ya ndoa yenu?.ana umri gani?.

3.ishu ni mitandao ama ishu ni kuwa na simu?.utamzuilia zama hizi?.
1. Sihofii lakini sipendi
2. ni haki yangu kuwa muwazi kwa mwenza wangu na kumjulisha kila nisichokipenda huenda kinaweza kupelekea ndoa kuvunjika.
3. Ishu ni mitandao ya kijamii simu ruksa kuitumia.
 
Mmhh umemtoa kijijini?
Mana facebook iliingia bongo miaka ya 2007 tukatumia hadi tukaiacha
Kwani kila aliyeko mjini ameshawahi kutumia mtandao wa facebook? Miaka hiyo alikuwa mwanafunzi.
 
Kuna vitu nadhani unaweza mzuia mtu ila kuna vitu naona kama ngumu

Mfano :mtu mzima kutokua na simu miaka hii inawezekana kweli?.
Hapana,simzuii kutumia simu. Namzuia kujiunga kwenye mitandao ya kijamii. Kumzuia mkeo kutumia simu ni kujiingiza kwenye utumwa mkubwa usio na mfano.
Sijaona umuhimu wa mawasiliano ya simu kama ilivyo kwa wanandoa.
 
Anaweza kua anatumia kwa siri kutokana na katazo ulilotoa...anapata hamu kujua hivi fb kuna nini hadi nakatazwa?.

bora anaeijua fb akaikinai..kuliko anaeanza ukubwani namsikitikia..curiosity killed the cat
Mwelevu akikatazwa anakatazika.
 
Wanaume wengi siku hizi wanaishi kwa wasiwasi mno
Yaan wanajiham mno [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwahiyo uko radhi kumuona anakosa furaha ili mradi tu wewe uridhike?
Kupitia mitandao atanisamehe,furaha ataipata kupitia mambo mengine. Furaha yake isigeuke kuwa kero kwangu kwasababu hata mimi nahitaji furaha.
 
Back
Top Bottom