Sipendi mke wangu atumie mitandao ya kijamii

Sipendi mke wangu atumie mitandao ya kijamii

Pole sana...
Hii yote ni kwa sababu unavyojiona wewe unavyotogoza kiulani kwenye mitandao ya kijamii basi unaona nae mkeo atakua analiwa kiulanini hivyo hivyo...
Cc: mahondaw
Kwa imani ya dini yangu naruhusiwa kuoa wake wanne,kwahiyo sioni kama kuna tatizo kutafuta mwanamke wa kumuoa.
 
Ila wewe kwako utumie tu sawa mwenzio asitumie mfyuuuu
Sio lazima kila anachokifanya mwanaume na mkewe/mwanamke afanye na kinyume chake iko hivyo hivyo. Mke wangu anasuka mimi ninanyoa.
 
Yani nasema kiukweli toka moyoni sipendi mke wangu atumie mitandao ya kijamii. Hata kama mimi mwenyewe natumia na anajua natumia lakini yeye sipendi nimuone anatumia hiyo mitandao. Najua wapo watakaoniona natumia mfumo dume potelea mbali na wala sijali.
Wewe mnyang'anye hiyo Techno yake
 
Mimi Mke nitakayeoa ni Lazima alijue hili
[emoji117]Wanawake ni wengi sana warembo,wenye kujipamba wacha Mungu na wenye tabia njema.
Kwaivo Uhuru atakua nao 100% ila akishavuka mpaka ndo kwaheri .
Na kwakulizingatia hilo, Kwangu mimi Mwanamke ni Msaidizi kama ilivyoamuliwa.
Tuko pamoja mkuu,halafu kuna kikao kinaandaliwa nadhani hiyo itakuwa ajenda mojawapo.
 
Hujatueleza ni Nini kilichokusibu mzee
Hakuna kilichonisibu mkuu. Ila wife anatamani sana na avutiwa mno na mtandao wa facebook. Nimemkataza asijiunge amenielewa lakini kama namuona amekuwa mnyonge baada ya kumkataza.
 
Bro kama hutaki atumie mitandao ya kijamii,,, mtengenezee mitandao ya kifamilia atumie!! [emoji35] [emoji35] Kama huwez hilo mwache aperuzi kwa raha zake [emoji57]
Nashukuru kwa ushauri wako mkuu,nimeelewa nimtie mimba mke wangu alee watoto ama sivyo?
 
Yaani wanaume wa kibongo kwa kujiona miungu watu
Imeandikwa kuwa mwanamke akimtii mume wake ndo sababu ya kupata ufalme wa milele. Unachotakiwa kufahamu na uweze kutofautisha ni mwanaume ameumbiwa na sifa za kiume,hali kadhalika mwanamke ameumbiwa sifa za kike. Na ndio maana anachokimudu mwanamke hata kiwe chepesi kiasi gani maadam kinaendana na maumbile ya mwanamke mwanaume hakimudu kitu hicho katu.
 
Back
Top Bottom