Sipati chaneli ya Russia Today kwenye Azam TV

Fanya utafiti Azam wanaipata hiyo channel RT kutokea wapi, kama wanaipata thr DSTV, jibu lipo maana DSTV wameifungia hiyo channel na hiyo ndio inapelekea kutokuwepo Azam tv

IMG_1159.jpg

You knw nothing acha ujuaji
 
Naona vuguvugu la Ukraine limegonga hadi Bongoland, sie wapenda na wapembuzi wa habari na mijadala na unbiased news accessors ni maumivu na masikitiko.

BBC, AJ, CNN,SkySports and the likes wanaripoti habari upande mmoja na wanazotaka wao watu wao wasikie hasa katika sakata la Ukraine-Russia.

Wametii wito wa wenye nguvu yaani EUs na US.
 
Ila tuseme tu ukweli, RT nimejaribu kuwafuatilia Youtube, wanachopost ni propaganda tupu, yaani hakuna habari kabisa. Wao wamevamia nchi ya watu halafu wanasema si uvamizi, ni ‘Operesheni ya kijeshi’, ndio kitu gani hicho?
 
Nimekua nikifiatilia channel hii katika kipindi hiki cha mzozo wa Russia-Ukraine ili kuballance matukio.

Sasa leo najaribu kuangalia haipo hewani na kwenye screen ya tv haileti ujumbe wowote either poor signal au vipi.

Je kwa sisi wapenzi wa Russia Today tv ndio imekula kwetu? Je inaweza kua sababu ni ile mabeberu wanayoisema kwamba RT ina spraed fake news ndio maana Azam wakaipiga chini?

Kwakweli sijapendezwa na hili.

View attachment 2137366
Sasa hivo habari wanazolalamikia wa magharibi kumbe ni documentary ya Wanazi walivyoua watu USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unaitaka hiyo chaneli andaa dish la futi 6 na risiva yoyote ya f.t.a halafu tutafutane niktwekee, chaneli yenyewe inazagaa zagaa ipo karibu kila satelite.
 
Fanya utafiti Azam wanaipata hiyo channel RT kutokea wapi, kama wanaipata thr DSTV, jibu lipo maana DSTV wameifungia hiyo channel na hiyo ndio inapelekea kutokuwepo Azam tv
naona mnalishana matango pori na kuaminishana ujinga.

hakuna uhusiano wowote wa dstv na azamtv katika masuala ya channel.

iko hivi, azamtv inatumia satellite ya Eutelsat ambayo headquarter zake zipo paris ufaransa. kiufupi Eutelsat ni satellite ya mabeberu.

mlolongo wa channel zote zinazopatikana kwenye vifurushi vya azam tv, zinakufikia wewe mteja kwenye kiTV chako pale nyumbani, kwa support kubwa ya satellite ya Eutelsat.

kwa mantiki hiyo, linapofika suala la RT, azamtv hawezi kwenda kinyume na msimamo wa mabeberu ambao wengine ndio hao wamiliki wa Eutelsat.

kuna mawili, inawezekana azamtv wameiondoa RT kwenye chanel list ili kukazia misimamo ya mabeberu dhidi ya Russia, au Eutelsat wamei-block RT kwenye satellite yao.
 
Ni upuuzi kumchagulia mtu chakuangalia na Kalipia
Wanaitoa yann kama mtu hataki hayo ma Cnn yao kwann walazimishe
We mwenzetu upo mbali sana kuna mambo huyajui nahisi unadhani bado Nyerere ndio Rais maana sio kwa hii sintofahamu yako,😃😃😃😃
 
Ila tuseme tu ukweli, RT nimejaribu kuwafuatilia Youtube, wanachopost ni propaganda tupu, yaani hakuna habari kabisa. Wao wamevamia nchi ya watu halafu wanasema si uvamizi, ni ‘Operesheni ya kijeshi’, ndio kitu gani hicho?
Ulitaka wasemaje mkuu
 
Kwani ukivamia nchi nyingine kijeshi tunaitaje?
Inategemea na mtazamo wa upande unaolipoti hilo suala:

Mfano uvamizi wa Waisrael wengine waliita kurudi kwenye nchi yao ya asili na wengine ni uvamizi na kukaliwa kimabavu kwa wapalestina.

Indo china wafaransa waliita oparesheni ya kuiondoa ukomunisti wakati wavetinamu waliita uvamizi kutoka Taifa la kigeni.

Marekani kuivamia Iraq wao wakisema wanaenda kwenye campaign ya kutoa siraha za Maangamizi wengine ni uvamizi tu

Afghanistan na ugaidi wakati wengine waliona ni uvamizi tu.

Kwa hiyo Urusi ilikuwa sahihi kuita kampeni ya kijeshi
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom