Azam Tv yapewa leseni ya kuonesha chaneli za ndani bure

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,533
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amelieleza Bunge leo Jumanne Mei 14, 2019 kuwa kituo cha televisheni cha Azam jana Jumatatu kimepokea leseni ya kuonyesha chaneli za ndani bure.

Pia, Nditiye amesema katika kipindi cha miezi saba watajenga mfumo wa kurusha chaneli hizo, hivyo wananchi wanapaswa kuvuta subira.

Naibu waziri ametoa kauli hiyo akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, aliyehoji ni kwa nini Azam wananyimwa haki ya kuonyesha channel za ndani bure.

"Je, Serikali haioni kuwanyima haki hiyo wakati wengine wamepewa ni kukiuka ibara ya 18 ya katiba ambayo inatoa haki ya kupata habari, lakini hata Rais wetu anatumia Azam kurusha matangazo yake hivyo tungejitangaza hadi nje," ameuliza Shangazi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula, aliuliza Serikali iwapo haioni kupitia TCRA kuwafungia local channels (chanel za ndani) baadhi ya ving'amuzi ikiwamo Azam TV, DSTV na vingine imewanyima wananchi fursa ya kupata habari.

Naibu waziri amesema Serikali inatambua umuhimu wa wananchi kujua mambo yanayoendelea, hivyo imetoa leseni zenye masharti tofauti.

Amesema kwa sasa matangazo ya umma yanarushwa na TBC1 na TBC3 maarufu safari channel.

Kwa mujibu wa Nditiye, kampuni zinazomiliki ving’amuzi vya DSTV, Zuku na Azam hayakustahiki kutoa huduma ya kubeba chaneli za ndani zisizolipiwa kutokana na masharti ya leseni zao.

Amesema Serikali imefanya jitihada ya kukaribisha maombi ya leseni ya kubeba maudhui ya chaneli za ndani kutoka kwa wanaohitaji kutoa huduma ikiwamo kampuni hizo ili ziweze kupata leseni stahiki.

Mwananchi

===================
MY TAKE

Ni wakati sasa ule ubabe wa soko wa mchina kutoonyesha chaneli za FTA bila malipo uende ukikoma...hawa jamaa kwa ubora nadhani vingamuzi vyao vitanunulika sana.

Hongereni Azam kwa hatua hiyo muhimu angalau tuone chaneli za ndani kwa ubora maana hivi visimbuzi vingine ubora hamna kabisa wengine mara wazime mara wawake...kama hao wengine wanaojinasibu wakubwa ubora picha zina ukunguukungu...

WITO WANGU KWENU AZAM...Mtuletee ving'amuzi vya maana na vya HD viwe na options lukuki ikiwezekana hata kuweka flash na kufanya gaming humo humo dunia ishaendelea fanyeni utafiti vizuri mje na kitu konki...wakenya waje wajifunze Tanzania. Heko!
 
Ina maana wanakuwa na antena kama startimes?
Yes watakuwa na antena maana hilo ni sharti muhimu kwa mux hiyo ndiyo primary way ya kutransmit signal zao ukisoma kwenye zile regulations za digital broadcasting utaona ina maana kwenda setelaiti ni secondary option kwa maeneo ambayo hayafikiki kirahisi kama huko mabonde kuinama
 
Nimemsikia Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano Atashasta Nditiye bungeni leo anasema tayari Azam wamepata leseni ya kuwa MUX wakiungana na akina Startimes Ting na Digitek...nadhani sasa ule ubabe wa soko wa mchina kutoonyesha chaneli za FTA bila malipo unaenda kukoma...hawa jamaa kwa ubora nadhani vingamuzi vyao vitanunulika sana. Hongereni Azam kwa hatua hiyo muhimu angalau tuone chaneli za ndani kwa ubora maana hivi visimbuzi vingine ubora hamna kabisa wengine mara wazime mara wawake...kama hao wengine wanaojinasibu wakubwa ubora picha zina ukunguukungu...

WITO WANGU KWENU AZAM...Mtuletee ving'amuzi vya maana na vya HD viwe na options lukuki ikiwezekana hata kuweka flash na kufanya gaming humo humo dunia ishaendelea fanyeni utafiti vizuri mje na kitu konki...wakenya waje wajifunze Tanzania. Heko!View attachment 1097133
Je tutaanza kuiona Taarifa ya Habari ya Azam Tv?
 
Azam nawaaminia sana hawa wasngeee wanawekeza haswa na hapo hutaona chenga yaani wakiwekeza kwenye jambo wanaweka pesa na matokeo yake ni kupata pesa zaidi. Naomba mzee bahresa alete magari naapa magari yatakufa haya mengine daaah kweli aliyepewa kapewa
Wapo kujenga minara wameahidi ndani ya miezi saba kila kitu kitakuwa sawa.
 
Huyu hapa
20190514_130348~2.jpeg
 
Yes watakuwa na antena maana hilo ni sharti muhimu kwa mux hiyo ndiyo primary way ya kutransmit signal zao ukisoma kwenye zile regulations za digital broadcasting utaona ina maana kwenda setelaiti ni secondary option kwa maeneo ambayo hayafikiki kirahisi kama huko mabonde kuinama
Kwa hiyo sisi wa kijijini haituhusu
 
Back
Top Bottom