Sipati chaneli ya Russia Today kwenye Azam TV

Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
10,416
15,971
Nimekua nikifiatilia channel hii katika kipindi hiki cha mzozo wa Russia-Ukraine ili kuballance matukio.

Sasa leo najaribu kuangalia haipo hewani na kwenye screen ya tv haileti ujumbe wowote either poor signal au vipi.

Je kwa sisi wapenzi wa Russia Today tv ndio imekula kwetu? Je inaweza kua sababu ni ile mabeberu wanayoisema kwamba RT ina spraed fake news ndio maana Azam wakaipiga chini?

Kwakweli sijapendezwa na hili.

IMG_20220303_141621.jpg
 
BBC,Skynews,CNN wanapika sana habari linapokuja suala Russia na Ukraine.Kuikosa RT kipindi ni balaa kubwa vyombo vya magharibi vinatulisha habari za upande mmoja.

Nashauri tuandamane hadi ubalozi wa USA tukiwa na mabango ya kulaani kitendo cha kuminya uhuru wa habari.
 
Hahaaaa!!mimi toka jana siipati hadi nikapanda juu uangalia kama dish limecheza , kweli mabeberu ni balaaa!!!

Ila ki ukweli hii RT, ilikuwa inaonyesha fake nyuzi tu, jana kuna mama wa kirusi alikuwa akihojiwa yupo moscow, anasema wao wanajua majeshi yao yako ukraine kuwalinda watu na sio kupigana, na ndicho wanachokiona kwenye tv, hayo kuwa wanaua watu ni propaganda za magharibi!!
 
BBC,Skynews,CNN wanapika sana habari linapokuja suala Russia na Ukraine.Kuikosa RT kipindi ni balaa kubwa vyombo vya magharibi vinatulisha habari za upande mmoja.

Nashauri tuandamane hadi ubalozi wa USA tukiwa na mabango ya kulaani kitendo cha kuminya uhuru wa habari.
Hata kama wanapika habari lakini RT, wamezidi, aljazeera tu ndio huwa wanonyesha ukweli, ndio maana sio kwa warabu, au wazungu kote wana mpinga!!!
 
Mimi Jana Nimeangalia Ilipofika saa 3na dakika kazaa Azam wakaizima baadae naangalia kwenye mitandao kumbe wamepigwa marufuku kuonyeshwa inamman Azam walikuwa wamechelewa kuiondoa
 
Satellite nyingi ni za mabeberu, hivyo ni rahisi kuiondoa RT hata kama Azam tv hawajaridhia. Ikumbukwe pia hata hizo kampuni zinazomiliki satellites pia zinaogopa kuguswa na vikwazo iwapo vitaenda kinyume na maamuzi ya Marekani au mataifa yao.
 
Back
Top Bottom