Sioi Solomon Sumari kugombea Arumeru

Nchi hii sijui tunaipeleka wapi? uamuzi ni kwao wana Arumeru.kama wanahitaji utawala wa ufalme watoto wao wataendelea kuwa mazezeta kwa kutawaliwa na kaukoo ka watu fulani fulani, otherwise mabadiliko makubwa yanatakiwa yafanywe na wao wenyewe kwa faida ya kizazi walichonacha na kijacho!!!!!!!!!! All the best.
 
Sasa hivi kila Jimbo Tanzania hii zipo familia ambazo ndizo WAMILIKI PEKEE wa SIASA na shughuli za kiuchumi za maeneo hayo. Hii imetengenezwa maalum na MAFISADI wa nchi hii. Hata hayo mabadiliko ya katiba ya CCM ni ujinga na kiini macho tu. Wamechelewa.
 
Inatakiwa Tume ya Uchaguzi ambayo iko huru na yenye nguvu za kweli za kusimamia Uchaguzi. Iwe ni tume isiyofungamana na chama chochote, inayoongozwa na sheria na taratibu zisizopindika. Iwe ni tume ambayo kwenye eneo la uchaguzi, inaheshimika, kuogopwa na kuaminika na watu wote.

Kwa sasa hivi, hii Tume ni sawa na kamati za sekretarieti za CCM.
 
Jana nilikuwa usa river,wapiga kura wengi waliosikia kuwa mtoto wa marehemu mbunge Sumari, Sioi Sumari na mtoto wa mkuu wa zamani wa jeshi meja Sarakikya,willy sarakikya ni dalili za kuwadharau watu wengine wa jamii hiyo.wamesema ubunge wa meru si ufalme wa kurithishana kwa familia zilizoshiba wakati wowote.

Wapiga kura wengi unaowasema ni wangapi kwa idadi? Unaweza kweli kuwepo Arumeru kwa siku moja tu na ukaweza kusikia wapiga kura wengi kiasi cha kuhitimisha kama ulivyofanya hapo juu? Mimi naona kama hii hoja imejengeka kwenye hisia zako binafsi zaidi kuliko kwenye maoni ya hao wapiga kura ambao nina uhakika hukuweza kukutana nao wengi kama unavyodai.
 
UTAWALA WA KIFALME!
Hata kama taratibu za kisheria zote zimefuatwa, na fomu zimetolewa, ni ****** sana kumchagua mtoto anayetokea familia hizi kuongoza tena!...Wameru watakuwa wamerogwa na nani hawa?...Hakuna Vijana wengine wasomi Meru, wanaoumizwa na utawala wa Kifalme?
 
Jana nilikuwa usa river,wapiga kura wengi waliosikia kuwa mtoto wa marehemu mbunge Sumari, Sioi Sumari na mtoto wa mkuu wa zamani wa jeshi meja Sarakikya,willy sarakikya ni dalili za kuwadharau watu wengine wa jamii hiyo.wamesema ubunge wa meru si ufalme wa kurithishana kwa familia zilizoshiba wakati wowote.

Tanzania ina rasilimali watu wengi sana wenye uwezo wa kuongoza jimbo hilo. Na hao watoto wa vigogo ni sehemu ya rasilimali hiyo. Lakini hatuwezi kuchagua mtu asiye na sifa tunazozihitaji eti kwa kuwa tu "NI MTOTO WA KIGOGO" na hatuwezi kuacha kumchagua mtu mwenye sifa zoote tunazozihitaji eti kwa sababu "NI MTOTO WA KIGOGO".

Cha msingi ni kuwepo kwa uwanja tambarare wa mapambano kwa watu wote, na tume iheshimu maamuzi ya watu wa Arumeru. Mimi sina Tatizo na watoto wa vigogo wanaojikongoja wenyewe, tatizo ni wale wanaotegemea nafasi za kubebwabebwa
 
Sina shida watoto kurithi wazazi wao kwenye ulingo wa siasa hapa Bongo. La muhimu kwangu hao watoto wana uwezo na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi? Wanagombea nafasi kwa sababu wameguswa na matatizo ya wananchi wa eneo lao au wanalinda hati-maliki? Na wanazijua kero za wananchi?
 
Jana nilikuwa usa river,wapiga kura wengi waliosikia kuwa mtoto wa marehemu mbunge Sumari, Sioi Sumari na mtoto wa mkuu wa zamani wa jeshi meja Sarakikya,willy sarakikya ni dalili za kuwadharau watu wengine wa jamii hiyo.wamesema ubunge wa meru si ufalme wa kurithishana kwa familia zilizoshiba wakati wowote.
hawa madogo wanaishi wapi? wanafikiri bado siasa za kurishishana zinaendelea tu.
 
Hivi kweli baba yako kafa hata siku ngapi bado wewe umeshawahi kuchukua fomu?

Kwa hiyo amefurahia kufa kwa mzazi wake siyo?

Hilo sasa ni jimbo la CHADEMA, Chagueni CHADEMA CHAGUA MAENDELEO.

chadema ikichukua lile jimbo nahama nchi
 
hoja mfu ni ipi kiongozi,
ninani asiyejua kuwa SOLOMONI SUMARI ni mkwe wa LOWASA?tunakumbuka uchaguzi mkuu JEREMIA SUMARI ambae ni baba wa SOLOMONI,alikua hoi anaumwa na aliye simamia na kufanya kampeni ni lowasa,kama aliweza kumfanyia kampeni mtu aliye hoi kitandani na kwamsaada wa kichakacha akashinda,atashindwa kuchakachua kwenye kura za maoni ilimradi mkwe apate??

Kwenye uchaguzi mdogo, huwa hakuna ule utaratibu wa kwenda kupiga kura za maoni kila kata kwa sababu ya ufinyu wa muda na pia gharama za uchaguzi.

Wanaopiga kura za maoni ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo [sawa na jinsi Mchambuzi alivyosema vikao husika vitateua/pendekeza jina la mgombea]. Then litakwenda kwenye vikao vya wilaya na mkoa, finally mwenye mamlaka ya mwisho ya uteuzi ni CC ambayo hupitia madokezo/maelezo ya vikao vya chini ili kufanya maamuzi.

Sasa mbona unarudia nilichosema na kukipinga bila kujielewa?
Mfumo wetu upo wazi kabisa.
OTIS
 
Hivi kweli baba yako kafa hata siku ngapi bado wewe umeshawahi kuchukua fomu?

Kwa hiyo amefurahia kufa kwa mzazi wake siyo?

Hilo sasa ni jimbo la CHADEMA, Chagueni CHADEMA CHAGUA MAENDELEO.

Kufa kufaana.
 
Ni haki yao kikatiba, tuwaache wana-Arumeru waamue wanaemtaka na hii ndo siasa. CDM iwetayari kupambana na yeyote Mpaka ipate ushindi.
 
Ni haki yao kikatiba, tuwaache wana-Arumeru waamue wanaemtaka na hii ndo siasa. CDM iwetayari kupambana na yeyote Mpaka ipate ushindi.

Tatizo siyo katiba wala kurithishana kiti, kilichopo hapa ni kwa interests za nani? Mimi naona EL et al in action
 
Back
Top Bottom