THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
Hii inaweza kuwafanya watu wengine waendeshwe na hisia za huruma kwa kufiwa na baba yake hivyo kumpa kura za huruma.Inawezekana kijana anataka kutumia ''APILI TU PITI''.
Kama Marehemu Jeremia Sumari alikuwa ni kipenzi cha wana Arumeru, then, mtoto wake ndie atasimamishwa na CCM na ndiye atakayechaguliwa!. Huu ni ukweli mchungu, ila ndio ukweli halisi!.
Hizi siasa za kurithishana hazikuanza leo. Kwani Abedi Karume anajua siasa gani?. Kisiasa Abedi Karume, si lolote sii chochote zaidi ya jina la Baba yake (wa kufikia?). Dr. Husein Mwinyi ana siasa gani?, ni jina la baba!. Vita Kawawa ana siasa gani?, ni jina la baba na jimbo la baba!. Adam Malima ana siasa gani?, ni jina la baba na jimbo la baba! and the list goes on!.
2015, Ndesamburo hatagombea tena Moshi mjini, wala Mrema hatagombea Vunjo. Hawa wote ni vipenzi vya watu wa majimbo yao, hivyo yoyote watakayemshika kumnyanyua mkono, ndiye atakaye chaguliwa!.
CCM italazimika kumpitisha Sioi sio kwasababu ndio inampenda sana, no!, itampitisha ili kujiokoa vinginevyo jimbo linakwenda Chadema!.
Ni mkwe wa Lowassa huyu, na sidhani kama ccm watampa nafasi maana watakuwa wanazidi kumpa nguvu Lowassa na atakuwa mtandao wake tu kwa vyovyote. wakimpitisha basi watakuwa wamejimaliza pia! Lowassa mjanja sana nadhani angekuwa na binti wengi basi angejiweka mahali pazuri sana kuliko sasa maana huwezi mpinga mkweMtoto wa marehemu jeremiah solomon sumary amechukua fomu ya ugombea ubunge kwa tiketi ya ccm . Kuna uwezakano mkubwa akapitishwa kuwa mgombea wa ccm kupambana na upinzani .
Wewe kuona mtu kachukua fomu na kusema ni urithi waona kuna hoja hapo?
mgombea wa ubunge kwa taratibu za chama chetu ni kupitia kura za maoni zilizowazi.
OTIS
Chama chetu !!! Haa haa haaa! Kumbe kuna watu wana chama chao !!..mgombea wa ubunge kwa taratibu za chama chetu ni kupitia kura za maoni zilizowazi.
OTIS
Anaitwa "Sioi" not "Sio"....
Nguvumali.......Kansa ya kurithishana na kutumia kigezo cha undugu kupeana vyeo/nafasi za kugombea uongozi haipo CCM peke yake....Ipo karibu katika kila chama na ndio kiini cha kudumaa kwa demokrasia na maendeleo ya Tanzania...Japo CCM ndio wanaongoza kwa hili,CHADEMA wanafuatia(hasa kwenye ubunge) watu wamegawana ubunge wa viti maalum kama njugu kisa tu ni ndugu ama wana uhusiano wa karibu...........Inakera na kusikitisha sanahawa watoto wa mawaziri wa ccm, watoto na familia ya Kikwete , hanana kazi ya kufanya ila siasa, hata mtu akisoma taaluma kama udaktari bado tu anadhani kuishi bila siasa haiwezekani.sasa mibaba zao iwe inarecord maridadi, tumemuona hapa juzi mtoto wa MALECELA, KATOKA KUBEBA box huko Marekani kaja kuona umaskini wa wana Mtera , umaskini ambao babake pia ni chanzo,wanakera sana, wanatufanya waTz ni wajinga, walaaniwe hawa watoto, hadi waanzi kujutia umaskini ambao baba zao wametutia katika taifa hili.
So ccm by not having preferential votes to get their candidate is trying to avoid unnecessary costs? CCM is the GRAND OLD PARTY it should know that democracy is never cheap!! Anaefanya vurugu ni nani ; si hao ccm wenyewe na wanashindwa kuthibitiana kwavile hawana nidhamu!