Wakuu heshima kwenu, Nimesoma comments za wengi humu, nimegundua wengi wetu tunatoa comments kiushabiki zaidi ya hali halisi ilivyo. Wengi wetu tunadhani CDM wanachukua jimbo kirahisi safari hii na hii si kweli hata kidogo. kuna thread moja nilichangia kuhusu Jimbo hili mara baada ya kifo cha Mzee Sumari. nitarudia tena hapa.
Yeyote kati ya CDM na CCM anaweza ibuka mshindi ktk jimbo hili kwa sababu zifuatazo: Wakazi wa jimbo hili wamegawanyika katika makundi mawili yaani Wenyeji na wahamiaji. kundi la wenyeji kama wengi tukikumbuka huko nyuma lina misuguano ya muda mrefu kwenye koo zao (rejea ugomvi wa KKKT 1989/1990), na kwa kawaida ya hawa ndugu zetu ni wagumu kusamehe haraka. kwa hiyo mshindi wa ubunge inategemea sana anaungwa mkono na koo zipi.
Kundi la pili ni la wahamiaji na kwa kawaida wengi wao (80%) wataunga mkono CDM na hawa utawapata sana maeneo ya pembezoni mwa barabara kuu. Technically CDM wakicheza vizuri kete zao wanaweza shinda kwa sababu ukoo wa Nassari (iwapo CDM watamteua) ni moja ya koo zisizofungamana na upande wowote kama ilivyokuwa kwa Sumari. Lakini pia kama CCM nao watazingatia uzaifu wa koo hizi wakaja na jina kutoka kwa wasiofungamana na upande wowote then kazi ipo na ni pevu.
Kumbuka Mzee Sumari hakutaka kugombea 2010 kwa sababu za kiafya lakini wazee wa pale walilazimisha na hata kampeni hakushiriki kwa kiwango kikubwa. CDM wanatakiwa kusahihisha makosa yaliyofanyika 2010, CDM mkoa walijikita sana Mjini na nguvu kidogo walizipeleka kwa Nassari, na hata kuna maeneo mengine nadhani ilishindikana kuweka mawakala, na hapo ndipo CCM ilipiga bao ingawa hata kwa kutokuchakuchua bado nina imani CCM wangeshinda kwa kura chache.
Wapiga kura wa Arumeru mashariki (wenyeji) wengi wao ni wazee hasa kina mama, na kama CCM wataleta jina neutral CDM msitarajie kupigiwa kura na kundi hili. ni wagumu sana kubadilika na kuelimika haraka. Ni matumaini yangu kwamba CCM watakuja na the Kaayas, the Palangyos, the Ayos and the likes, na hapo for sure CDM watapiga bao kama kumsukuma mlevi.